JE KUJIUZULU KWA WATENDAJI
WETU WA NGAZI ZA JUU NI SOLUHISHO LA TATIZO?
Taafsiri
ya kujiuzulu kwa maneno ya kawaida ni
kuacha (Dhamana) ya utendaji ambayo kiongozi ambaye amepata shinikizo la Kujiuzuru
analazimika kuachia madaraka ikiwa ni sehemu ya uwajibika wa pamoja kiserikali kutokana
kushindwa kutekeleza majukumu ambayo kiongozi muhusika alitakiwa kuyatenda au
kuyasimamia kulingana na kiapo chake cha kazi.
Katika nchi ambazo zimeendelea kiuchumi na kisiasa dhana hii ni jambo la kawaida na hutekelezwa bila shinikizo kubwa sana. Kinyume chake Katika nchi nyingi za zinazoendelea Tanzania ikiwamo tunajua utekelezaji wa dhana hii huwa mgumu sana na ukitendeka inakuwa baada ya shinikiza kubwa wakati mwingine kutoka kwa wananchi hii inatokana sana na kulindana kisiasa.
mheshimiwa edward lowasa alilazimika kujiuzuru
JE KUKIMBILIA KUJIUZURU NI
SOLUHISHO LA TATIZO?
Kwa nchi yetu Tanzania Pengine
kama wanazuoni wengi walivyowahi sema kuwa "Kukimbilia kujiuzulu siyo
suluhu sana ya tatizo. Kwasababu kama ni hivyo, watu wanaweza kuharibu mambo
kwa makusudi wakitegemea watajiuzulu na kukaa pembeni." Kwani dhana hii ya
kujiudhulu haihusishi adhamu ya ya moja kwa moja kama ya kushitakiwa kwa
utendaji huo mbovu uliobainishwa. Tatizo langu daima ubaki kuwa je
tunapomshinikiza kiongozi kujiudhru tunakuwa tayari tumeshabaanisha tatizo, na
hata akichaguliwa kiongozi mwingine kushika nafasi anajua anatakiwa kufanya
nini? Je tatizo ni mtu au ni mfumo? Kama ni mtu basi ni sahihi kumshinikiza
kiongozi mwenye dhamana kuachia ngazi; lakini kam tatizo ni mfumo wa utawala
nina mashaka kama kweli kujizuru kunasaidia kuondoa tatizo linalopigiwa kelele
kwa wakati husika.
Tatizo linalokabila taifa
letu kwa sasa mfumo wetu wa utawala umevamiwa na ufisadi. Swali la kujiuliza ni
moja tu je huu ufisadi ni utamaduni wetu? au ni ugonjwa tu umeingia ambao
unatakiwa kutibiwa mara moja kwa njia ambazo wengi wamezisema na wengine
kuzitumia ? tupende au tusipende inaonekana ni mfupa uliotushinda Jibu lipo
wazi tunajua tatizo lakini hatujui chanzo cha tatizo
MHESHIMIWA DR.IBRAHIM MSABAA ALILAZIMIKA KUJIUZURU;
Mheshimiwa Mtei aliwahi
sema kuwa “Nilifanya kazi Mwalimu Nyerere, alikuwa kiongozi ambaye hasiti
kuwachukulia hatua viongozi waliokuwa wakimwangusha katika utendaji wake,” nafikiri
itakuwa ni vyema kwa viongozi wetu wa ngazi za juu kama wataweza kuwachukulia
hatua za uwajibikaji za haraka sana watendaji wote wabovu wanao haribu mfumo
mzuri wa utawala, na hatimaye kulipeleka taifa letu katika nyia ambayo sisi
hatuko tayari kwenda huko kwa manufaa yao binafsi.
TUKITAFAKARI SAKATA LA
KUZAMA MELI MV.SKATIG JE TATIZO NI WAZIRI AU MFUMO MZIMA?
MHESHIMIWA HAMAD MASOUD ALILAZIMIKA KUJIUZURU KUFUATIA AJALI YA MELI MV.SKATIG
Katika sakata hili
wanazuoni wengi wamebainisha tatizo ambalo tunakabiliwa nalo kama taifa sio
swala la kujiuzuru kwa viongozi, tunatakiwa kwanza tuimarishe mfumo wetu wa
utendaji kwa maneno mengine mfumo ambao tunao wa kiutawala ni dhaifu. Na
kielezo kimoja kati ya vingi ni pale viongozi wetu wanaziona nyadhifa zao ni
sawa na hati milikizao! Hivyo kwao hawawajibiki
kuishi au kuongoza kulingana na maadili ya uongozi. Wamesahau kabisa kanuni za
uongozi kuwa “Cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu kwa faida yangu binafsi
au kwa faida ya familia yangu”.
DR.Bana,Mallya na Prof.
Mpangala kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam waliwahi sema kuwa tunatakiwa kubadilisha
mfumo hasa kwa kujenga utamaduni wa kujiuzuru Bali kuimarisha maadili ya kazi na uongozi kwa watumishi wa
serikali na pale kosa linapofanyika wahusika
wafikishwe mahakamanimara moja.
Emmanuel Mallya alisema licha
ya kuwa mabadiliko yamefanyika lakini sio suluhisho kutokana na nchi kuwa na
mfumo mbovu wa utawala.
Alisema mawaziri
waliokumbwa na kashfa mbalimbali walitakiwa kusimamishwa kazi ili wachunguzwe
na kama ingebainika hawana hatia wangerudishwa kazini. “Kama wangekutwa
na hatia wangefunguliwa mashitaka, hii ingewafanya wengine kuogopa kutafuna
mali za umma kwa kuhofia kuwa watasimamishwa kazi na kuchunguzwa”
Dk Bana alishawahi sema kuwa dawa ni kubadilisha mfumo mzima wa utawala.
Katika kufanikisha
kuboresha mfumo bora wa utawala mti ukigolewa ungolewe wote pamoja na mizizi
yake; watendaji wote katika kila ngazi wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kufanya
hivi tutaweza kukomesha tabia ya ubinafsi inayoota mizizi ndani ya Taifa letu
na kuleta kichefuchefu katika kuimarisha maadili ya kazi na maadili ya uongozi.
Kwa msingi huu tunarudi pale pale kuwa “Kujiuzulu siyo utatuzi wa tatizo”,
Pamoja na kauli ya waziri
wa uchukuzi wa jamuhuri ya Muungano mheshimiwa Dk Mwakyembe kuhusu ajali kuwa “Watanzania
hawana sababu ya kumtafuta mchawi wa ajali hiyo kwani imetokea kwa bahati
mbaya… Tukubali kwamba ajali hii ni bahati mbaya. Maofisa wetu
wametuthibitishia bila kuwa na shaka kwamba meli ilikuwa nzima na haikuzidisha
abiria, kujiuzulu siyo suluhisho, tushikamane katika kipindi hiki kigumu.”
Lakini je anakubali kuwa
meli hiyo ilikuwa sio chakavu na kama kiongozi wa ngazi ya juu anatoa ushauri
kuwa ilikuwa sahihi kwa taifa kutumia meli ambayo ilishasimamishwa kufanya kazi
huko marekani? Na hivyo usajili wake ulukuwa sahihi? Na kama hivi ndivyo kwa
nini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeisimamisha meli pacha nyingine ambayo
haikuhusika na ajali?
Nakubaliana sana na
maelezo ya Kepteni Magamba alisema kuwa anayepaswa
kulaumiwa katika ajali hiyo ni kiongozi wa safari za meli. Kiongozi huyo (Port
State Controller) hupokea taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa na kuruhusu
meli iondoke au isiondoke. Kiongozi huyo husimamia usalama wa meli ndani na nje
ya bahari kwa kushirikiana na eneo meli inapoelekea. “Meli kabla ya kuondoka
lazima ifuate taratibu zote, nahodha hupata kibali kutoka Sumatra (clearance)
na kuipeleka kwa ‘Port State Controller’ ambaye tayari anakuwa ameshapata
taarifa za hali ya hewa,” alisema Magamba.
KWA NINI KAMA TAIFA BADO
TUKO KWENYE MFUMO MBOVU WA UWAJIBIKAJI?
Kama alivyowahi sema Mwenyekiti
wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliitaka Serikali kuangalia upya uwajibikaji,
utendaji na mwenendo wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra) akidai kuwa taasisi hiyo imeshindwa kuwajibika ipasavyo kudhibiti
vyombo vya usafiri.
Mwenyekiti wa APPT Maendeleo, Peter Mziray alisema: “Lipo tatizo katika uingizaji, ukaguzi na usajili wa vyombo vya usafirishaji wa majini… Serikali na mamlaka zinazohusika na usajili hazifanyi kazi kwa kuzingatia umuhimu wa kazi waliyopewa na matokeo yake ndiyo kuruhusu vyombo vibovu kubeba roho za watu.”
Lazima tukubali kuwa tuko
katika mfumo mbovu wa uendeshaji wa shughuli za serikali mfumo mzima ni mbovu
(the whole system is dysfunctional). Na kama tukigundua hivi kama taifa
tutakuwa tumefanikiwa kuondoa tatizo la utendaji katika shughuli za serikali.
Mimi binafsi bado nafikiri kuwa watendaji wetu wakuwa kwa namna moja au
nyingine wanatakiwa kuwa kama Marehemu Park Rais wa Korea ya Kusini ambaye alikuwa
anahakikisha kuwa watumishi wote ambao wamepewa dhamana lazima watekeleze
wajibu wao na kama wakishindwa wanawajibishwa mara moja. Mfano mwingine
tusiende mbali wanatakiwa kuwa kama Marehemu Baba Wa Taifa Julius Nyerere au
Marehemu Sokoine ambao walikuwa hawana mchezo na maadili ya watumishi ambao
wako chini yao; tukiiga mifano yao tunaweza kama taifa kubadilisha kabisa mfumo
wa uwajibikaji.
Viongozi wetu wengi hivi
sasa uwajibikaji wao ni wa maneno tu, ni mahodari wa kusema lakini ni wabovu wa
vitendo kwa kiasi kikubwa. Kama alivyo wahi sema baba wa Taifa Hayati mwalimu
Nyerere kuwa kwa nchi ili iweze kuendelea inahitaji: Ardhi, siasa safi na uongozi bora; hivi vitatu vikikamilika tunazungumzia uwajibikaji wa kweli na
sio wa kuoneana aibu; kwa sasa taifa letu au linakosa viwili kati ya hivyo
vitatu na mafanikio yetu yanabaki kuwa ngonjera;
Kama tutafanikiwa
kubadilisha mfumo wa utawala na usimamizi wa shughuli za kila siku za serikali
hata inapotokea kiongozi ambaye amepewa dhamana anawajibishwa italeta tofauti
ya uwajibikaji; kwa hivi sasa kijiuzuru kwa viongozi wetu inabakia katika
nadharia ya siasa zaidi ambayo bado haibadilishi mwelekeo wa uwajibikaji wa
kweli;
Nafikiri ni wakati muafaka
kwa viongozi wetu wa juu
kufikira zaidi jinsi ya kurekebisha mfumo wa uendeshaji wa serikali kwa manufaa ya wananchi wake.
kufikira zaidi jinsi ya kurekebisha mfumo wa uendeshaji wa serikali kwa manufaa ya wananchi wake.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
nakubaliana na mawazo yako kwa hivi sasa tanzania inahitaji viongozi walio komaa kimaadili, kwani ukiwa unajua wajibu wako hasa kwenye dhamana ambayo unayo na kuto kuoneana haya na kubebana kisiasa na fikra za kukosa kura wakati wa uchaguzi tutaifikisha nchi yetu kwenye nchi ya ahadi iliyojaa maziwa na asli kwa wananchi ambao wengi ni wanyonge hata hawajui kesho watakula nini.
ReplyDelete