TATIZO
LA AJALI ZINAZOENDELEA NA KUPOTEZA MAISHA YA WATANZANIA WENGI;
TATIZO LIKO WAPI?
NI
UBUTU WA SHERIA?
UBOVU NA UFINYU WA BARABARA ZETU
KIBURI
CHA MADEREVA?
UBOVU
WA MAGARI NA UBABE WA WAMILIKI?
Nilishawahi kuandika huko
nyuma kuwa Taifa la Tanzania limeendelea kushuhudia mwendelezo wa ajali
nyingi za barabarani ambazo zimeendelea kupoteza nguvu kazi ya taifa
hili. Kwa ujumla ajali hizi zimekuwa zikitokea kila kona wakati mamlaka
za kisheria; zikiendelea kuhimiza kuwa zitahakikisha kuwa zitakomesha vifo
vinavyoyokana na ajali hizo.husika kutekeleza yafuatayo;.
Kuimarisha doria katika njia kuu,
Askari wa Usalama Barabarani kuimarisha shughuli za
ukaguzi wa magari mabovu, na
kuweza kusimamia sheria ipasavyo
bila tama ya kupokea rushwa na hivyo
kuwatendea haki abiria.
Kuimarisha elimu kwa wananchi na wadau wengine juu
ya
umuhimu wa kuisaidia Serikali
kwa kutoa taarifa kwa
vyombo vya dola kuhusu madereva
walevi, wanaoendesha
mabasi yao kwa kasi, madereva wanaotiliwa mashaka kuhusu
ujuzi wao wa kuendesha, na pia kukataa kupanda magari
mabovu au yaliyojaa kupita kiwango kinachohitajika, ”sit level”
Kuendelea kuboresha sheria za Usalama Barabarani ili
zichangie katika kudhibiti shughuli za usafiri na
usafirishaji,. Kutoa elimu
kwa madereva ili wazingatie sheria
za kanuni za kazi zao,
Kukagua leseni za madereva ili kubaini wale abao wanatumia leseni
feki kuhakikisha kuwa ni za
halali,
Kuwashirikisha wenye magari ili washiriki kikamilifu katika
kuhakikisha kuwa wanaajiri wadereva waaminifu na wenye
kuwajibika.
Pengine swali
ambalo daima ninajiuliza pamoja na malengo
mazuri yaliyoainishwa hapo juu, kwa nini
serikali
imeshindwa
kabisa kisimamia utekelezaji wa sheria na sera
zake za usalama barabarani kwa raia wake kwa
muda
mrefu?
Je serikali
haina askari wa usalama barabarni wa kutosha
kukabiliana na tatizo hili?
Je ni tatizo
ni la wamiliki wa biashara hii wamefanikiwa
kuiteka idara nzima ya usalama barabarani?
Je madereva
wanaoendesha magari hayo wanafahamu fika
maadili ambayo wanapaswa kuyafuata kulingana
na sheria
za usalama barabarani wakati wa
kuendesha magari hayo?
Tathimini ya
muda mrefu kutoka vyanzo mbalimbali inabaini
kuwa licha
askari hawa kuwapo na tunaambiwa kwa kiasi
kikubwa ajali
zinazotokea zinasababishwa na madereva
wazembe ambao
wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za
usalama
barabarani.
Tunajua,
kwamba madereva wengi wa mabasi ya abiria
wanaendesha wamelewa. Je hakuna sheria
inayowabana kama katika nchi nyingine kuhusu kilevi? Je, dereva huyu
aliyekunywa pombe kabla ya kuanza kuendesha nap engine wakati wa safari
ataweza kuendelea kuwa na maarifa yake ya kawaida na uwezo wake wa kawaida
kumudu gari na mazingira ya barabara yanayomkabili?
Inafahamika wazi mara
nyingi askari wa usalama barabarani wanabariki mwendo kasi wa madereva
kwa kupokea rushwa; je taifa linakubaliana na tabia hii izidi kuendelea?
Tunawaacha wakimbize magari wanavyotaka mpaka lini?. Je tumeshindwa kabisa
kusimamia “Speed Limit” ni ukweli ambao huupingiki kuwa Madereva wa mabasi
wengi wanakimbia kupita speed waliyopangiwa. Je ni kweli kuwa serikali kupitia
wizara yake kweli imeshindwa kuwadhibiti hawa madereva ambao ambao tunaweza
kuwaita wahuni na wenye viburi kwani wamekuwa wakiendesha vyombo
hivi vya moto kwa mwendo kasi, usiofuata taratibu za usalama barabarani na
matokeo yake kusababisha ajali mbaya ambazo matokeo yake ni vifo vingi vya
watu. Lo imefila wakati sasa serikali iamke na kusema basi inatosha kwa sasa
hasa kwa kuanzaia na askari wake wa usalama barabarani wanaelezwa kuchangia
uwepo wa ajali kwani wamekuwa wakiruhusu makosa kutendeka kwa sababu tu ya
kuchukua rushwa ndogondogo.
Kwa nini serikali
imeshindwa kusimamia sheria ya kutowaruhusu madereva matumizi ya simu za
mikononi wanapokuwa wakiwaendesha raia; ni vigumu sana kufanya mambo
mawili kwa wakati mmoja uwe makini barabarani na hapo hapo utumie simu kuongea
na mtu mwingine; Ni busara ya kawaida tu dhamana ambayo umebeba kama
dereva ni zaidi ya Kuongea kwenye simu za mikononi kwa hiyo tabia hii
haifai kabisa kwa dereva wa gari la abiria aendeshapo gari. Hii ni hatari
kwa abiria na watu wengine watembeao kwa miguu. Matokeo yake baada ya
kujenga madereva wanaleta kilio na hasara kubwa kwa taifa taifa
letu na familia zetu kwa mambo tunayonaweza kuyazuia bila gharama yoyote .
Je serikali kupitia
wizara inakubali kuwaona askari wake wakikwepa maadili na kiapo chao cha kazi
kwa kujihusisha na rushwa na kuhatarisha usalama wa watu wake; Tumke sasa kwa
usalama wa watu wetu na kupinga kwa kauli moja mwendo kasi unaoendana na
kutojali sheria na alama za barabarani .
Ni ukweli ambao
haufichiki kuwa hata sheria zetu zinatoa mwanya mkubwa kwa mahakama kuwatoza
faini ndogo badala ya kifungo au adhabu kubwa ambayo itakuwa pigo kwa dereva
mna mmiliki wa biashara hiyo. Wote ni mashahidi wa jinsi ambayo watu ambao
wamesababisha ajali kwa uzembe wa kujitakia, tena ajali ambayo imesababisha
vifo vingi , lakini wamekuwa wakipigwa faini ya Sh50,000 na kuachiwa
huru. Je nchi nyingine wamefanikiwa namna gani kudhibiti ajali hizo za
uzembe? Kwa nini tusijifunze kutoka huko?
Pamoja na kwamba ajali
haziwezi kuzuilika jumla,lakini tuzipunguze.Ajali ya gari inapotokea sio dereva
tu ndiye wakulaumiwa,ang alia hali za barabara zetu zilivyo,hali ya
hewa,abiria nao je wanaelewa sheria za barabarani ili kumkemea dereva
anapovunja sheria hizo.Jambo la msingi ni kuelimisha watanzania wote wajue
sheria za barabarani.
Tuangalie sheria Namba 30
ya Mwaka1973 na marekebisho yake ya mwaka 1996 inayohusu ni jinsi gani magari
yanatakiwa yawe yakiwa barabarani. Pamoja na tatizo la madereva
tuzinagatie vile vile tatizo la ubovu wa magari amabayo vile viel huwa ni
chanzo cha ajali nyingi;
je wamiliki wanatoa
kipaumbele gani katika kuhakikisha kuwa magari yao yako katika hali nzuri ya
kusafirisha abiria kwa usalama?
Kwani nini gari bovu
ambalo halina break nzuri linaruhusiwa kusafiri? Kama dereva ambaye anajali
akatae kuendesha mpaka litengenezwe; uungwana wa wamiliki utaweza kuepusha
ajali nyingi ambazo zinaweza kuzuilika kwa kutumia muda wa ziada kutengeneza
gari na kuhakikisha kuwa liko salama kwa matumizi ya wananchi; kama
wamamiliki watalazimisha matumizi ya gari bovu hatulidanganyi jeshi la
polisi bali tunajidanganya sisi wenyewe na hatimaye kupoteza nguvu kazi ya
taifa.
Pamoja na tatizo kubwa
la uchakavu wa miundombinu, ikizingatiwa kuwa barabara nyingi
haziko katika hali nzuri sana au nyingine pamoja na kutengenezwa hivi karibuni
bado hazijeweza kusaidia kupunguza vifo kutokana na pengine kuwa chini ya
kiwango na kusababisha ajali haraka.
Tunaomba serikali
ikishauriana na wataalamu wake kuangalia namna ya kuepusha janga
hili kwa kuwa na usimamizi ulio bora na kurekebisha mapungufu yatokanayo na:Inasikitisha sana katika kipindi kifupi ajali ambazo zimeuwa raia ambao hawana hatia zimeongezeka sana; Tunahitaji kubadilisha mbinu za kukabiliana na ajali hizi ambazo zinaendelea kutokea sasa kwa kasi hii ya ajabu.
Barabara mbovu; Magari
mabovu; Mwendo wa kasi; Udereva mbaya; Usimamizi dhaifu wa sheria; na Watembea
kwa miguu wasiojali. Rushwa katika utoaji leseni za udereva umetajwa katika
orodha ya sababu za ajali chini ya kifungu cha Usimamizi dhaifu wa sheria. Kuruhusiwa
kwa magari mabovu.
Safari bila ajali zinawezekana kabisa
No comments:
Post a Comment