WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, August 3, 2012

NINI MATOKEO YA MGOMO WA WALIMU ?


  • Kufuatia maafikiano hafifu kati ya walimu na serikali, Je malengo ya serikali ya elimu bora kwa vijana wetu yatatimia?
  • Nafikiri ni pigo kwa kwa vijana wetu ambao wanategemea elimu bora kwani wataishia kupata "BORA ELIMU"
  • JE SERIKALI YETU WASHAURI WA VIONGOZI WETU WA JUU WANAWAJIBIKA VIPI KATIKA USHAURI?
  • NAFIKIRI TATIZO KWA MIGOMO MINGI INAYOENDELEA NI KUKOSEKANA KWA EFFECTIVE COMMUNICATION.
  • JE TUNATUMIA SIASA ZAIDI KATIKA KILA TATIZO?

ELIMU NI HAKI YA MSINGI KWA WANAFUNZI WETU.
Jedwali hapo chini linaonyesha matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha nne, matokeo haya yameleta simanzi kwa wananchi wengi ambao wameyaita ni janga la taifa letu kutokana na ukweli kuwa kiwango cha kufeli kimekuwa ni kikubwa mno katika matokeo haya ya kidato cha nne ya  mwaka 2010-2011;


DARAJA
WANAFUNZI
I
5363
II
9942
III
25083
IV
136,633
0
177,021

Maswali mengi yameulizwa kwa nini taifa limefikia katika hali kama hii; je lawawama ziende kwa serikali kwa kushindwa kutoa kipaumbele katika mfumo mzima wa elimu ya watoto wetu? Au ni tatizo la wanafunzi wetu (watoto wetu) kuto kuwa makini katika masomo yao (lack of seriousness)? Lakini tatizo hasa nini wakati taifa linafahamu wazi kuwa ELIMU NI HAKI YA MSINGI KWA KILA RAIA WA TAIFALETU.


Taifa lazima likubali kuwa wakati tukiwa katika wimbi la hili la mgomo wa walimu kwa sababu yeyote ile, hasa ile ya masilahi bora ya walimu wetu na mazingira mazuri ya utendaji kazi;
Ni ukweli ambao haufichiki kuwa Tanzania haitaweza kuendelea na kustawi bila kuwa na elimu nzuri kwa watoto wetu ambao ndio msingi wa kesho wa mustakabli wa taifa letu. Hata kama tutakataa kwa msingi wowote ule ukweli utabaki pale pale kuwa  elimu yetu tukilinganisha na mifumo ya elimu ya nchi nyingine hasa zile ambazo zimeendelea na hata pengine zinazo endelea kama Tanzania au zinazotuzunguku mfumo wetu wa elimu sio mzuri

Serikali inanadi vipi sera za elimu bora?

Serikali inatueleza kuwa katika miaka 50 ya uhuru imefanikiwa kupanua fursa za watoto na vijana wetu wengi sana kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.


Je serikali imeboresha vipi masilahi ya walimu ambao wamesaidia sana katika kufanikisha malengo ya sera za serikali katika kipindi hiki cha miaka hamsini ya uhuru?
  
Na kwa kutambua mafanikio haya yote  serikali bado inaendelea kutoa kipaumbele cha kwanza kwa bajeti ya elimu ili iweze kuajiri walimu wengi zaidi, kuongeza vitabu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Tatizo je ajira za walimu zinaendana na hali halisi ya ustawi wao kuwa na maisha bora kwa kutoa elimu bora? 

serikali imekuwa ikitueleza kuwa inaendelea kuongeza matumizi ya teknohama katika utoaji wa mafunzo pamoja na kujenga uwezo wa wanafunzi na waalimu kiteknolojia ili kwenda sambamba na karne hii ya utandawazi.  


Aidha, inaendelea na mpango wake wa kujenga maabara za sayansi katika sekondari zetu zote. 

Serikali imesisitiza adhima ya kuchuakua hatua thabiti za kuboresha maslahi na mazingira ya kufanyia kazi ya walimu na watumishi wa sekta ya elimu.  

Serikali imekusudia kutenga pesa za kutosha katika kufikia malengo haya.


swali hapa je pesa zinazotengwa zinakizi haja ya hali halisi ya majengo na vifaa vya kufundishia kwa shule zetu? je wananfunzi wanapata nafasi ya kuweza kusaidiwa na walimu kwa ukaribu "one by one"

Tatizo liko wapi?


  • Msongamano wa wanafunzi katika shule zetu ambao hauendani na bajeti inayotolewa, vifaa vya kufundishia; vyumba vya kusomea ambavyo vitaweza kuwagawanya wanafunzi katika idadi ambayo ni rahisi kufundishika na kuelewa na kusaidiwa; Hivyo hushusha kiwango bora cha elimu;    

·        Ubovu wa huduma za jamii kama barabara, hospitali, maji safi na salama; ukosefu wa mishahara mizuri ya kuwamotivate walimu zaidi  kuingia katika taaluma hii; ni kweli kuwa  elimu ni silaha pekee ambayo inaweza kutusaidia kubadilisha dunia na maisha yetu, kwa msingi huu wale ambao wana elimu  sio tu elimu bali elimu bora  wananafasi kubwa ya kufanikiwa;

Je sisi wazazi na wanafunzi tunataka nini?

Taifa linahitaji utekelezwaji wa haki hii ya msingi kwa vijana wetu yaani:

Elimu bora ambayo inatokana na walimu bora ambao wameshiba na wameridhika ma maisha yao kwa kupata haki zote wanazostahili kupata na wanawajibika kwa moyo bila mashaka


Mitaara ya elimu itayarishwe iendane na masomo yanayolingana na hali halisi ya maendeleo ya dunia ya sasa pamoja na masomo ambayo yanawavutia wanafunzi kujitafutia zaidi jitihada za kusoma?


Sababu nyingine zinazowafanya watoto wetu wasifanye vizuri shuleni ni pamoja na wanafunzi kuchukia shule kutokana na sababu za kitaaluma na kimazingira, shule zetu nyingi zina kosa vifaa muhimu ya kufundishia na kujifunza shule kama inakosa vitabu vya kiaada vifaa vya mahabara je unategeme kuwa kutakuwa na ubora wa elimu hapo? Mimi nasema hapana na tusitegemee miujiza kutoka katika shule zetu za serikali ambazo watoto wetu wengi ndiko wanakosoma.


Pale tutakapo amua kuacha maneno na kuanza kutekeleza maneno yetu kwa vitendo ndipo tutegemee kuona: watoto wetu wakifikia malengo yao ya elimu kupitia elimu bora na kufanikiwa kuondoa umasikini kwa kiwango kikubwa sana.

Pengine kwa akili tu ya kawaida tunaweza kusema kuwa serikali yetu inahusika katika kuharibu mfumo mzima wa elimu, kwa nini nasema hivi kwa msingi huu mmoja mkubwa elimu inapasa iwaguse na kuwahusu moja kwa moja watoto wetu; mahitaji yao yanatakiwa yatiliwe mkazo kwanza kabla ya mambo mengi ya serikali,


Inatakiwa mtoto wa kitanzania kwenda katika shule nzuri inatakiwa iwe ni haki yake ya kikatiba, watoto wafundishwe na walimu ambao ni wazuri ambao wanapokea mishahara mizuri na wanavifaa vizuri vya kufundishia

KWA NINI SHULE BINAFSI ZINAFANYA VIZURI?


Nini kinatokea katika shule za binafsi wana walimu wazuri ambao wanlipwa vizuri na wanavifaa vya kutosha sasa nini tutegemee kutoka kwao ni daraja la kwanza na watoto wakifeli ni daraja la pili;    

Wazazi nao wanamchanga mzuri sana  katika maendeleo ya watoto wao, wazazi wahusishwe katika maswala ya watoto wao mzazi ajue ratiba ya maendeleo ya motto wake na ahusike katika maisha ya kawaida ya watoto wao; tukifanikiwa kufanya kama wenzetu wan chi zilizoendelea tutasonga mbele, ni kitu kizuri kuona wazazi wakishiriki moja kwa moja katika maisha ya kawaida ya watoto wao na motto sipomwona mzazi wake katika maswala mbalimbali ya shule anasikitika na mzazi nina muuma pia.

Shule zetu zisijikite sana katika maandalizi ya mitihani tu zijikite vile vile katika kuwasaidia watoto wetu katika kujiandaa na maisha yao.

JE WANAFUNZI WANAOSOMA SHULE ZA KATA WANA HAKI SAWA NA WALE WA MIJINI? JE TUNAJADILI PIA MATOKEO YA SHULE ZA KATA/VIJIJINI?

Je shule zetu za vijijini zinafikiwa vipi katika maendeleo ya elimu?
Tunafahamu kuwa wazazi wetu wengi ambao wako vijijini hawawezi kuwasaidia watoto wao kwa vile hata wenyewe wahajeelimika vyakutosha na hata wakati mwingine wanaona aibu kujadili mambo ya shule kwa vile hawajui;

Matokeo yake wanafunzi wengi wanajikuta wakishiriki zaidi katika shughuli za kilimo ( Elimu ya Kujitegemea na kuwafanyia walimu wao kazi majumbani);


NINI KINAWAFUKUZA WALIMU WAZURI KAMA WAKO KATIKA SHULE ZA KATA/VIJIJI?

Kutokana ubovu na huduma duni za jamii si rahisi kuwapata walimu bora kwenda kufundisha vijijini wengi watapendelea kubaki mijini;

Hata serikali inajikuta katika wakati mgumu wa kupeleka huduma kama vitabu, nafasi nyingi ambazo zimezcha wazi kutojaza mara moja, hata pale zinapojazwa zinakuwa na walimu ambao sio wazoefu na wazuri kitaaluma.


Ni mara nyingi sana walimu ambao wanfundisha katika shule za vijijini wanaweza wakawa wanafundisha muda mfupi ukilinganisha na wenzao wa mijini kutoka na sababu kama vile wanatakiwa kutembea umbali mkubwa kwa ajili ya kwenda kutibiwa, kuchukua mishahara, kwa ajili pengine ya kwenda kwa ajili ya mafunzo ya  au kutembelea familia zao;


Walimu wengi wanakuwa hawana nyumba za karibu na shule pengine na wakati mwingine inawapasa kutembea kwa miguu umbali mkubwa kwenda kufundisha asubuhi hali hii inaweza kusababisha kuanza vipindi kwa kuchelewa;
Swala la ukaguzi na utendaji wa walimu ni tatizo pia kutoka na tatizo sugu la usafiri hata wakaguzi hawatembelei shule hizo kuona maendeleo yake mara kwa mara;


HITIMISHO


Lazima tukubali kuwa kuwa na walimu bora ambao wanavifaa vinavyotakiwa kwa ajili ya elimu bora huleta tofauti kubwa sana kwa wanafunzi wetu na sifa kubwa kwa taifa letu; taifa lisipokuwa tayari kubadilika tutaendelea kunyosheana vidole kuhusu matokeo ya wanafunzi wetu kila mwaka kama jedwali la hapo chini linavyoonyesha, kwa ujumla ni aibu kubwa kuona watoto wetu wanafeli kwa kiasi kikubwa namna hii, na kubaliana na wengi ambao wamediriki kusema kuwa hili ni janga la kitaifa ni vyema kama tulitafutia ufumbuzi wa haraka; washauri wa serika li yetu mnashauri nini?



Na lazima tukubali kuwa elimu bora kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu ni haki ya kila mwanafunzi katika jamii hii ya kitanzania; viongozi wetu wanapaswa kulijua hilo na kulielewa hilo na kulitekeleza kwa moyo wote na kwa faida ya wote;


Swali la kujiuliza ni hili pamoja na faidia zote zitokanzao na elimu, kwa nini serikali yetu bado haioni faida ya kuwekeza zaidi katika elimu na kuwawezesha walimu kimafao zaidi? 


“Imesahau kuwa Elimu ni mtaji wa msingi kwa jamii?” Je serikali inaogopa kuwekeza kwenye elimu kwa sababu ya ushindani kutoka kwa wananchi katika kuwaongoza? Ni ukweli kuwa jamii ikiwezesha kwa elimu bora matokeo yake ni kuwa hawatakuwa tayari kukubali kuburuzwa na kudanganywa danganya pengine na sera ambazo hazieleweki;


pamoja na kauli ya Mheshimiwa Raisi kuwa serikali haiwezi kuyatekeleza madai ya walimu; lakini bado serikali yetu inanafasi ya kukaa na walimu na kuangalia namna mbadala ambayo inaweza kuwamotisha walimu katika kazi yao hii ngumu. lakini kama serikali yetu itatumia kauli za vitisho na za kukatisha tamaa, hata walimu wakirudi kufundisha basi tutegemee matokeo mabaya katika mitiani inayokuja. Mungu liepushe Taifa na mporomoka wa elimu bora kwa vijana wa Taifa hili.

No comments:

Post a Comment