Kikwazo kukubwa sana cha uadilifu na uwajibikaji ni matumizi mabaya ya
ofisi kwa masilahi ambayo hayagusi maisha ya wananchi, rushwa na matumizi
mabaya ya pesa ni miongoni mwa malalamiko makubwa katika hoja hii.
Rushwa ni miongoni mwa matatizo yanayoikabili dunia nzima kwa ujumla.
Mataifa mengi yamekuwa yakipambana na tatizo la rushwa ingawa nchi
zinatofautiana katika viwango vya rushwa. Tatizo la rushwa linaigusa jamii
katika viwango tofauti na katika mazingira tofauti. Rushwa na matumizi mabaya
ya ofisi yako katika viwango vyote vya maisha ya binadamu. Kwa sasa taifa letu
linaangalia sana rushwa katika ngazi ya viongozi wakubwa na waandamizi wa
serikali ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaoongoza na kutegemewa sana kwa
kuwaletea wananchi maisha bora.
“Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika
kupambana na hali hii mara baada ya Uhuru mwaka 1961 ni:- Mwaka 1966
Serikali iliunda Tume ya Kudumu ya Uchunguzi ikiwa na lengo la kuhakikisha
viongozi wa Serikali hawatumii vibaya madaraka waliyokabidhiwa na umma kwa
manufaa yao binafsi. Mwaka 1971, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
lilitunga Sheria ya Kuzuia Rushwa Na.16/1971. Kutungwa kwa sheria hii
kulifuatiwa na kuundwa kwa Kikosi cha Kuzuia Rushwa mwaka 1975, ili kuimarisha
zaidi mapambano dhidi ya rushwa, Bunge iliifanyia marekebisho Sheria ya Kuzuia
Rushwa Na. 16 ya 1971, mwaka 1991 ikaundwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa kwa lengo
la kuzuia vitendo vya rushwa. Mwaka 2007 baada ya kutungwa Sheria ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Na 11/2007 na kufutwa Sheria ya Kuzuia Rushwa Na. 16/1971
jina la taasisi lilibadilika na kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU). Hivyo TAKUKURU ilianzishwa rasmi Julai, 2007 na kurithi kazi zilizokuwa
zinafanywa na chombo hiki kwa majina ya awali.”
Pamoja na upango huu mzuri
wa serikali katika maandishi na katika kimantiki tatizo liko wapi kwa vilio vya
wananchi kuhusu matumizi mabaya ya ofisi za viongozi wetu waandamizi? Je
mazingira haya mazuri ya sheria ya kumlinda mwananchi na mali zake ni sawa na
uamuzi ambao hauna usiammiaji mzuri?
Je tatizo ni
serikali au usimamiaji wa sheria husika?
Je ofisi
husika hazina meno ya kutosha kutenda kazi?
Au ni tatizo
la kulindana sana kwa masilahi binafsi?
Tatizo ni watu au mfumo uliopo ambao unatoa fursa kwa
viongozi na watendaji kuwajibika kwa waliowateua
Watanzania wengi leo hii wanajiuliza
hivi taifa hili sasa linao viongozi wanaojua wanatakiwa kufanya nini?
Au vyeo ambavyo watu
wanavyo wamepeana tu kwa “ MUHALI” na kwa msingi huu haiwasumbui nini
kinachoendelea hivyo hawawajibiki kwenye nafasi katika kuwasaidia Watanzania.
Hoja na matukio
ya kujikanganya kutoka watendaji serikali waandamizi mawaziri na manaibu
mawaziri pamoja na repoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kama waandishi wengine walivyowahi andika na
kuelezea huko nyuma linalifikisha taifa katika ombwe la uongozi.
“Ukiwa na chombo baharini kinapita katika dhoruba kali, halafu
nahodha na mabaharia wanajshughulisha na mambo mengine lile la hatari lililoko
mbele yao hawalijali, chombo hicho ni lazima kiseree na kupotelea majini”.
Viongozi wetu
wanapaswa kujifunza katika nchi za
wenzetu kasoro zinapojitokeza katika wizara yako kama tuhuma hizo ni za kweli
au la wajibika kwanza kupisha uchunguzi huru wa tuhuma hizo kwa vile wewe
mwenyewe umeshindwa kuwajibika na umekaribisha zengwe hivyo wajibika.
Uwajibikaji wa
viongozi wetu ni tatizo nakumbua Raisi Mstaafu Mkapa aliwahi waita mawaziri ni sawa na "askari wa
miavuli"; siamini mawaziri wetu ni askari wa miavuli hawaziwezi dhoruma za
angani pengine hawana ustadi wa kuruka kwa kutumia miavuli wao; askari wa miavuli
lazima ajue utaratibu mzima wa kutumia huo mwavuli ukikosea tu unakupeleka
ndiko siko wengi wnaishia huko.
Nafikiri zile kongamano ambazo serikali imekuwa ikiwafanyia kuwanoa ubongo hazijawa effective kwa mawaziri wote kwani wengi wanalalamikiwa kwa utendaji wa uwajibikaji wa chini ya kiwango.
Kipimo kimoja
kikubwa cha uongozi bora ni uwezo wa kusimamia rasilimali za wananchi,
uadilifu, uwajibikaji, uzalendo na kumcha Mungu; kiongozi akiwa na vitu hivi
huzaa hekima ua uwajibikaji wa kweli na uzalendo wa kupenda nchi yako na
kusimamia rasilimali zake kwa faida ya Taifa.
Inaoneka kuwa baadhi ya viongozi wetu kutumia nguvu zao sio kuondoa umasikini bali kuongeza umasikini
kwa mtanzania wa kawaida.
Kweli naamini
madaraka matamu, watu wanayatafuta kwa gharama pengine ili kukizi masilahi
binafsi, ndio yanafuata masilahi ya taifa.
Amani yetu
ambayo tunamshukuru Mungu kwa zawadi hii pekee kwa ambayo watanzania wamejaliwa
kwa misingi mizuri ya waasisi wetu Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na
Maheremu Mzee wetu Abeid Aman Karume kwa uadilifu wao na mapenzi yao kwa taifa
la Tanzania, tusipikuwa makini tuaipoteza kutoka na baadhi ya viongozi wa sasa
ambao wanatumia vyeo na madaraka kwa masilahi binafsi ambayo inajenga chuki
miongoni mwa wananchi.
Changamoto ya
amani yetu ni kwa watendaji wote wa serikali hasa
watendaji waandamizi kuwa wakweli
ili waweze kusikia sauti ya wanyonge, na kupitia rasilimali za taifa wasaidie katika
kujenga jamii inayozingatia na kuheshimu haki msingi za binadamu. Kashafa ufisadi,
rushwa, uzembe na kutowajibika mesomo hii tuweze kuipunguza katika midomo ya
wananchi na katika maandiko yetu. Hilo linawezekana kama viongozi wetu watakuwa
wakweli kulingana na viapo vyao kabla ya kuingia katika ofisi husika. Kwa kufanya hivyo tutaweza
kuondoa ombwe la uongozi.
tunahitaji tanzania ambayo iko tayari kwa mabadiliko kutoka hasa kwa viongozi wetu , viongozi wasifanye Tanzania yetu kuwa shamba la bibi. tumechoka tumechoka
ReplyDelete