WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, April 10, 2012

THE LEGACY OF STEVEN CHARLES KANUMBA R.I.P



               
 "UPENDO MIONGONI MWA WASANII TANZANIA"

"Maneno yangu ya mwisho, hata tukiwa na uwezo wa kuhamisha milima kama hatupendani katika tasnia ni kazi bure,kile kilicho moyoni ndio kioneshe usoni na si vinginevyo".

Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga  ni mtoto wa tatu katika familia yao akiwa na dada zake wawili. Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na  sekondari ya Mwadui, na badae  alimaliza elimu yake ya awali ya sekondari “ o-level” katika shule ya Dar Christian Seminary. Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.


Kanumba alianza kujishughulisha na sanaa ya uigizaji mapema sana akiwa bado mdogo, kwa kujiunga na vikundi vya uigizaji kupitia luninga kabla katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam. Baada ya kukomaa Kaole; baada ya kujiamini kuwa anaweza alianzisha kampuni  yake mwenyewe ya filam.

JE KANUMBA AMEACHA NINI KWA WASANII WENZAKE?

  • Kupitia upendo, uadilifu na ushirikiano Kila binadamu anauwezo wa kufanya mabadiliko na maendeleo ndani ya jamii husika na hata kugeuza jangwa kuwa nchi ya kijani iliyojaa neema za kila aina.

  • Kanumba katika kipindi cha uhai wake amefanikiwa Kuelimisha, kufundisha, kuburudisha, kwa kutumia sanaa kama kioo cha jamii. 
  • Marehemu kanumba alikuwa ni mtu wa watu alikuwa ni msanii pekee aliyepiga hatua na kuishi maisha ya wasanii wa kimataifa jambo ambalo tunafikiri haliwezekani kutokana na mazingira ambayo tunaishi.
  • Marehemu kanumba ametufundisha kuwa mafanikio vile vile yanachangiwa na kuwa mcheshi, tabia ya kupendana na kuwajali wale unaofanya nao kazi ili ujumbe uweze kufika vizuri kwa jamii.





  • Marehemu kanumba ametamani sana wasanii wenzake wawe na umoja ambao daima utakuwa unaotawaliwa na Upendo, l
  • Kwa msingi huu legacy ya Kanumba ni upendo upendo na msamaha pale mnapokoseana.

Mwenyezi Mungu umempenda zaidi Ndugu yetu kanumba Kama yeye Mwenyewe alivyonukuu katika kazi zake Zaburi ya 121


 Ni kweli kuwa Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasnia ya filamu Tanzania. 

No comments:

Post a Comment