Maggig
Mjengwa aliwahi andika huko nyuma kuwa “Watanzania leo tumekuwa ni watu wa kulalamika tu hata kwa yale
ambayo kimsingi ni wajibu wetu wananchi kuyafanya. Kwa tunavyoenenda, hata aje
malaika kutuongoza, bado naye atapatwa na wakati mgumu”.
Ninapata
wakati mgumu sana kutafakari na kuielewa dhana hii, je tumeingiliwa na mdudu wa
aina gani katika fikara zetu na katika maisha yetu ya kila siku? Kama ni kweli
hii ina maana kuwa tunatawaliwa na maisha ambayo hayana matumaini.
Swali
ambalo je woga huu wa mabadiliko ni kwa watanzania wa kawaida tu au hata
viongozi wetu? Je ndugu yangu mjengwa alikuwa ameyaongelea mabadiliko gani? Ilinifikirisha
zaidi pale aliposema hivi “Tumekuwa kama watu wa taifa la kusadikika
... “Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka…
Tumekwisha umwa na nyoka wa matendo yetu mabaya ya zamani”.
Kumbe woga wetu wa
mabadiliko unatokana na kutokujiamini kwetu kwa sababu ya matendo yetu mabaya.
Ni matendo gani ambayo yanatupa sisi wananchi wa Tanzania wakati mgumu wa kuamua kubadilika?
Jambo hili la
mabadiliko ya matendo yetu nakubaliana nawe kuwa kwa kweli lazima itamfanya mtu
kuogopa mabadiliko kwa kufikiria masilahi binafisi kwani akifanya mabadiliko
yanaweza kumweka katika wakati mgumu. Mara nyingi maba
Uadilifu na uaminifu.
Kwamba mtu ukiamua kuisimamia “ndiyo”, basi aisimamie bila kutetereka, na
akiamua kuisimamia “siyo” vile vile aisimamie bila kuyumba. Na kwamba mtu
akiisimamia “ndiyo” ukijua kwamba ni “siyo” ni unafiki na uovu. Vilevile
akiisimamia “siyo” ukijua kwamba ni “ndiyo” ni unafiki na uovu!
Mtu mwenye msimamo, uadilifu na uaminifu daima anakuwa mbali na unafiki
na uovu. maana ina msingi chanya wa kuendesha maisha katika jamii yoyote ile.
Jamii fulani na kuishi akizungukwa na historia, utamaduni na desturi za
watu wake. Privatusi karugendo aliwahi kuandika katika moja ya makala zake kuwa “Katika
familia zetu, katika jamii zetu na katika taifa letu, tunahitaji msimamo,
uadilifu na uaminifu. Hatuwezi kujenga familia, jamii na taifa imara bila kuwa
mbali na unafiki na uovu. Bila kujenga utamaduni wa “ndiyo” kuwa ni “ndiyo na
“siyo” kuwa ni “siyo”, hatuwezi kupiga hatua ya maendeleo bila
kuizingatia falsafa hii”. Kwa
msingi huu kuwa ni kweli kuwa bado tunakazi kubwa kuyakubali mabadiliko
kutokana na ualisia wa maisha yetu na jamii inayotuzunguka.
Je woga wa
kuogopa mabadiliko unatokana na sisi kama taifa kuwa waoga wa kufikiri? Au ni
uvivu wa kusoma na kujua nini kinaendelea ndani ja jamii yetu. Lakini katika
hili la kutokukubali mabadiliko linanipa wakati mgumu sana pale ninapoona na
kuelewa kuwa hata waandishi wetu wa habari “ media crew” pale wanaposhindwa
kuhimili wimbi hili ukizingatia kuwa wao ndio walitakiwa kuwa viongozi wa
kuwaelimisha watu kuhusu namna na mbinu za kuyakubali mabadiliko,
Katika siku za
karibuni kumekuwa na malalamiko ya wanahabari kuegemea jamii Fulani na
kuisaidia iendelee kuogopa mabadiliko; lazima tufike mahali tuweze kuiambia
jamii yetu kuwa umesahau kuvaa nguo.Kutokana na
jamii inayotuzunguka hakuna mtoto mwenye ujasili ambaye atamwambia mama yake
leo “ mama angalia mfalme hajevaa nguo” kwani hata watoto wetu wadogo
wameshaambukizwa woga wa kuogoma mbabadiliko;
Tatizo hata
wasomi wetu katika hoja zao hata kwenye forum zinaonyesha kuwa “wakati mwingine” zinaogopa mabadiliko hivyo
wataendelea kungangania au kushabikia hoja Fulani za mtu au kikundi Fulani cha
watu hata kama mwisho wa siku hazina mwelekeo wa mabadiliko ambayo yatalisaida
taifa katika mabadiliko na maendeleo ya jamii.
Kama mwandishi
mmoja alivyowahi kuandika kuwa “jamii imeshatambua kwamba
mito,maziwa,bahari,mabwawa,madini, ardhi ni vyanzo vya kuletea maendeleo kwa
jamii yao lakini jamii hiyo haitumii rasirimali hizo kujiletea maendeleo, basi
tatizo ni udhaifu wa kufikiri uliomo kwenye jamii husika”.
Taifa letu kwa
sasa kiuhalisia liko kwenye mtikisiko mkubwa sana kuanzia kwenye maadili ya
kijamii hadi kwenye nyanja kuu ya siasa. Mtikisiko huu kwa kiasi kikubwa
unasababishwa na kukosekana kwa misingi sahihi ya wapi jamii yetu inaelekea. Pamoja
na hilo hata watendaji wetu katika nyadhifa mbalimbali wamekuwa na ufinyu na
mwelekeo wa ubinafsi zaidi na utumiaji wa madaraka kwa manufaa binafsi na
hawako tayari kuwajibika na kukiri kuwa wamekosea. Daima wanajiona nje ya
mzingo wa matatizo haya yanayoikabili jamii yetu,hivyo wanafanya hujuma kwa
kudhani wao wako sehemu salama,Lakini hali halisi inaonesha wanajidangaya. Wanasafiria
katika chombo kwa nje wao wenyewe wanakiona kuwa ni salama sana lakini wamesahau
kuwa “Taifa ni kama chombo cha safari baharini,kikizama hakuna
kinachosalia, wakati mwingine hata waogeleaji hodari na mahiri hunaswa na
wadudu bahari”.
Taifa letu kwa
hivi sasa limekumbwa na tatizo na
viongozi wetu ambao wamepewa dhamana ya kuongoza idara za serikali kwa
kushindwa kuishi kulingana na viapo vyao vya kazi na kuishia kuwa ni sehemu ya
Ufisadi amboo unatafuna nchi yetu. Katika mjadala huu mkuu na mzito ambao
baadhi ya wabunge wamekasirishwa na tabia hizi za hawa watendaji wakuu na
kuwataka wajiudhuru, kwa kukiuka maadili ya uongozi “matumizi mbaya ya pesa za
walipa kodi” kama mbunge wa Njombe alivyosema “Mheshimiwa Naibu Spika,
inashangaza na kusikitisha kuwa nchi inatafunwa. Wanaofanya haya ni mawaziri
wetu. Nchi inakufa na tuelewe kuwa Tanzania sio mali ya CCM, ni ya Watanzania
wote.“Mawaziri wetu wamekuwa mchwa, wanaangamiza nchi na leo nitamtaja waziri
anayeongoza kwa kutafuta fedha za Watanzania. Ni Waziri wetu wa Fedha, Mustafa
Mkulo. Ameuza viwanja, amelidanganya Bunge baada ya kuivunja CHC,”- Deo
Filikunjombe ( CCM)
Hili
likifanikiwa tutakuwa tumeanza kuondoa woga wa mabadiliko, kama mawaziri
watajitafakari kuwa ni mchwa na wamekosa maadili yamekumbwa na wimbi la rushwa
basin a wakaamua kujiuzuru hata kama wataona wanaonewa lakini wakaamua kukaa
pembeni ili uchunguzi ufanyiki itakuwa ni dalili njema ya mabadiliko.
Wasipowajibika
bunge linataka kumuwajibisha Mtoto wa Mkulima “ waziri Mkuu Mheshimiwa Pinda atawajibishwa na bunge kama taratibu
zitatimia.
Je kweli tatizo ni Waziri Mkuu? Au Tatizo ni
jamii ambayo imetulea? Je tatizo kulipa fadhila baadaya uchaguzi kwa wale
waliotoa msaada? Au tatizo na ukosekanaji wa Maadili ya uongozi kwa watendaji
wetu? Au tatizo ni viongozi wetu kuto mwanini Mungu hivyo kukosa kabisa
ubinadamu? Je tatizo ni umasikini wa viongozi wetu kabla ya kuingia madarakani
hatima ya uroho na ulafi wanaishi kuwa mafisadi?
Nini hasa tatizo letu na kuogopa mabadiliko? Chama
kingine kikishika madaraka nitafungwa au kunyogwa? Je jibu la maswali haya ni lipi?
Nafikiri ujasiri utatusaidia sisi kuweza kufanya
maamuzi sahihi ya mabadiliko; hivyo tunamwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu kuwa MKALI
katika utendaji wake na kama mheshimiwa Pinda atapigiwa kura naungana na Maggig Mjengwa kuwa
“kupigiwa kura ya
wabunge kukosa imani nae ina maana pia kuwa wabunge hawana imani na bwana
mkubwa aliyemteua Pinda”.
No comments:
Post a Comment