TUMEJIFUNZA NINI KUTOKANA NA UCHAGUZI MDOGO ARUMERU MASHARIKI?
- Siasa zisizo na mvuto wa maendeleo ya kuwakomboa watanzania;
- siasa za kupakana matope badala ya kunadi sera za kuwakomboa watanzania.
- Kampeni zilizojaa matusi au maneno yasiyofaa kwa tija ya maendeleo ya mtanzania
- Malumbano, vijembe, matusi na kashfa kati yamiongoni mwa vyama vinavyoshiriki.
- Tumeona aina ya viongozi wabunge ambao tunawategeme watuvushe kwenye maisha bora na kutujengea mazingira ya maisha bora katika karne ya teknolojia na sayansi kwa mwendo huu ni ndoto kufika huko.
KAMPENI NI NINI?
Kwa kifupi, Kampeni zilianza zamani. Katika vitabu tumesoma kuwa
zilianza enzi za wanafalsafa mahiri duniani Socrates na wenzake.
Wakati huo ilikuwa ni njia mbadala ya kumwondoa madarakati
kiongozi asiyefaa.
Katika Tanzania yetu tunaweza kujifunza jinsi Mwalimu Nyerere
alivyofanya kampeni ya kudai uhuru kwa kuunganisha nguvu za watanzania wote
kuonyesha na kuwashawishi wananchi wazawa kukubali kuwa mkoloni mtawala wa
wakati huu alikuwahafai kwa maendeleo yetu na kwa uhuru wetu. Kwa mtazamo
chanya hizo zilikuwa kampeni kwa vile zilihusisha kuwashawishi wananchi kuunga
mkono juhudi za wapigania uhuru kumwondoa mkoloni.
Kampeni kama wengi walivyowahi
sema ni wakati ambao vyama vinavyowania uongozi katika ngazi yeyote ile
vinatakiwa kunadi sera za vyama vyao kwa ajili ya maendelo ya mwananchi wa
kawaida; kwa maneno mengine ni fursa njema kueneza sera bora za Kujinadi kunajumuisha kutaja sifa zako na uwezo wako kwa nini
utakuwa kiongozi bora kuliko mpinzani wako na hivyo unastahili kura zao
Kujinadi pia kunajumuisha kutaja mapungufu ya mpinzani wako kwa
nini hana sifa ya kuwa kiongozi bora na hivyo hastahili kura yao.
Busara ya kawaida inatueleza kuwa watu wanahitaji taarifa za
msingi kuhusiana na msimamo na sera za mgombea. Wanahitaji kampeni yenye
taarifa nyingi za kuelewesha kwa kina masuala muhimu yanayogusa vipaumbele na
kero zao.
Tatizo ni nini? Kwa nini kama taifa tunaendlea na kampeni chafu
kila wakati?
Vyama vingi vya siasa vinafikiria kuwa siasa chafu matusi ni
tiketi bora ya ushindi; vyame vingi vya siasa ushindani wao wanajipima kwa kupiga
kampeni chafu badala ya kueneza sera na kuwaacha wananchi wapime.
Viongozi wengi wa vyama wanashindwa kujenga hoja za kweli kuhusu
mapungufu ya chama kingine; wanakosa vielelezo vya hoja zao; namna gani
atatekeleza ahadi za kumkwamua mwananchi wa kawaida na kivipi anaona mapungufu ya kiutekelezaji na uwezo mdogo wa
kiongozi anayeshindana naye?
kampeni nyingi zinazofanyika ni si za kupata viongozi bora bali bora viongozi. Uthibitisho wa hoja hii kampeni
hazizingatii maadili, na uadilifu wa kiongozi mtarajiwa maana yake mtu yeyote
anaweza kuwa kiongozi.
Je nini tumejifunza katika Mwelekeo wa kampeni Arumeru
Mashariki?
Jambo la kwanza linalosikitisha kwa wengi walioshiriki kufanya
kampeni ni vyama ambavyo vinadadi
wagombea wake ktutumia muda mwingi sio katika kunadi sera zenye tija kwa
wananchi wa Arumeru bali vinatumia na kupoteza muda mwingi kuendeleza malumbano
yasiyo na maana, na kwa msingi huu ni kumnyima haki ya msingi ya kujua na
kutafakari sera ambazo angeweza kuziona pengine zitaweza kufaa katika kumsaidia
kumletea maendeleo. Katika hilo kwa kweli tunahitaji viongozi ambao wangekuwa
(great thinkers) kwa maendeleo ya wananchi sio viongozi ambao wanaweza kusimama
kwenye jukwaa na kudadi maneno kama “kudadadeki”
Vyama vya siasa nchini vinashindwa kuelewa kuwa siasa sio ugomvi
wala sio vita, siasa ni nguvu ya hoja; siasa ni mchezo wa masumbwi na unatakiwa
ufuate sheria za mchezo na sio kucheza kinyume cha utaratibu. Na jambo moja
kubwa katika siasa ni mchezo ambao unafanyika chini ya demokrasia.
Kinachoendelea Arumeru mashariki sijui ni democrasia gani inatumika, iliyokosa
maadali ya kunadi sera:
Kampeni za matusi zinajenga misingi ya vurugu na mwisho wa siku kura zitapigwa sio
kwa kupima sera bali upenzi wa vyama kitu ambacho kama tutakuwa wakweli
kinarudisha nyuma maisha bora kwa kila mtu: je hilo ndilo tunalolitamani
liendelee katika nchi yetu?
Kisiasa, kampeni ni
jitihada au mpangilio maalumu unaofanywa na chama au vyama kwa lengo la
kushawishi mchakato wa utoaji maamuzi katika kundi fulani. Katika nchi
zinazofuata mifumo ya kidemokrasia, kampeni za kisiasa mara nyingi humaanisha
kampeni za uchaguzi.
Je ni chombo gani
kinachosimamia maadili ya kampeni wakati wa chaguzi?
Je ni kweli kuwa chaguzi
zetu zimetawaliwa na hujuma na chama chenye nguvu ndicho daima kinachoshinda?
Je ni kweli kuwa wakati wa
chaguzi hakuna uwanja sawa wa kisiasa kutoka kwa vyombo vya kusimamia na
kuratibu uchaguzi?
Ndipo tunapofika kwenye
hoja ya msingi na kufikiria kuwa utawala wa sheria katika chaguzi ni dhaifu na:
Je vyombo hivyo havina
meno binafsi na haviko huru vya kutosha?
Kwani tunasikia malalamiko
daima kuwa chaguzi zinatawaliwa na rushwa na hujuma nyingine miongoni mwa vyama
husika?
Je tume ya uchaguzi na
msajili wa vyama wanawezaje kuimarisha demokrasia ya kweli katika kufanikisha
kampeni huru na zenye tija kwa wananchi?
Tukururu inawajibikaje
katika mazingira haya ina msaada wowote au inaangalia upepo unavyovuma?
WAJIBU WA
MWANANCHI WA KAWAIDA KATIKA KIPINDI HIKI NI NINI?
Nafikiri kama nilivyowahi
kuandika katika moja ya makala yangu wananchi wanahitaji sana elimu ya uraia,
ili waweze kuepuka hujuma na sera uchwara
zinazotolewa na wanasiasa kwa faida zao binafsi nakuwa na uwezo wa kuzidhibiti kampeni za matusi na sinazoweza
kuhatarisha amani ya nchi.
Elimu ya uraia
itawasaidia kuwajengea wananchi uwezo wa maamuzi na kwa uwezo huu wananchi
watakuwa na nguvu na kuwashikisha adabu wanasiasa
uchwara wasio na hoja, ili vyama vinapokuja kwenye uchaguzi vijipange. Ndio maana wakati mwingine naashiria kusema
kuwa hata kinachoendelea bungeni wakati mwingine chimboko lake ni hili
wanasiasa wetu wanakosa hoja za nguvu za kumkwamua mwananchi hawajipangi sawa sawa
ni sawa na hoja zinazo kurupushwa kutoka usingizini.
Je makapeni manager vya vyama wanakazi gani katika kuhakikisha
kuwa wanadadi sera zinazotakiwa?
Katika kampeni nyingi nafikiri wamekuwa wakifanya kazi za uenezi
zaidi na sio kuvisaidia vyama vyao katika ushindani wa hoja nzuri na nzito nz
zenye mvuto wakati wote wa kampeni;
Kampeni manager ndio dira ya kutumainiwa katika chaguzi yeyote;
ni viongozi ambao wanatakiwa watembee mbele zaidi kimawazo, kifikra na
kimwelekeo; wao ndio marubani wa ushindi;
Katika nchi za wenzetu kutokana na ushindani wa hoja makapeni
manager wanakuwa makini ukiaukwaji wa maadili, lugha za matusi automatically
zitamwajibisha kichama na kuachia nafasi yake yenye heshima kubwa;
Tumeona katika chaguzi zetu nao hushindwa kuzuiaa na kuratibu
mchakato mzuri unaofaa wa uelezaaji wa sera bora kwa jamii.
Kampeni yaweza kuwa ni kuwaelezea wananchi mambo utakayowafanyia
na namna utakavyotekeleza. Hii ni pamoja na kueleza ilani yavyama vyao,
vipaumbele vyao, huduma za afya na utakavyokomesha rushwa na maisha bora kwa
mtanzania
Makapeni Manager wa vyama “Pengine” wanafikiria zaidi kuwa kuzungumzia mabaya ya wenzao badala ya sera ndiyo kufanikisha mchakato mzuri na utakaowezewsha chama chao katika mbio za uchaguzi ambao unaoshindaniwa.
Makapeni Manager wa vyama “Pengine” wanafikiria zaidi kuwa kuzungumzia mabaya ya wenzao badala ya sera ndiyo kufanikisha mchakato mzuri na utakaowezewsha chama chao katika mbio za uchaguzi ambao unaoshindaniwa.
KAMA TAIFA NINI KIFANYIKE KUEPUSHA HALI KAMA HII KUENDELEA
KUJITOKEZA TENA NA TENA?
Kwa ujumla, suala hili la kampeni linahitaji msukumo mkubwa na labda mapinduzi fulani kwa sababu hivi sasa Watanzania hawamchagui kiongozi wala chama kwa sababu ya sera zake au uchapakazi wake bali wanafuata ushabiki tu. Kwa msingi huu wananchi watendelea kubariki na kushangilia matusi kwa vile tu yanakikashifu chama na watendaji wa chama tofauti hata kama hakutakuwa na tija yeyote katika maisha yao, kama Mheshimiwa waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba alivyowahi sema kuwa “Siasa nyingine zinajenga chuki, siasa za kinafiki siwezi kuziunga mkono, tufikie wakati tutofautishe mambo binafsi na mambo ya umma,”
Kama taifa hakuna kisichowezekana katika kuleta mageuzi ya kweli
ya kufanya kampeni za kiustaarabu, zenye maadili na zenye tija kwa Taifa tuwe wazalendo wa kweli kukubali kuwa tunaweza
kufanya kampeni ambazo hazitahusisha matusi, BALI KAMPENI ZILIZOJAA NGUVU YA HOJA NA USHINDANI WA KWELI KWA
MAENDELEO YA TAIFA.
bravo men nimeipenda hii kazi na uchambuzi stahiki, ni kweli kama taifa tunahitaji kubadilika kwa maendeleo ya Taifa na sio kikundi kidogo cha watu. keep it up
ReplyDelete