TUME YA
KURATIBU KATIBA MPYA YAAPISHWA RASMI NA MHESHIMIWA Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Safari ya mchakato wa
katiba mpya yanazidi kuendelea vizuri, baada ya tume ambayo ilikuwa imetangazwa
na Rais wa Jamuhuri ya Tanzania kukamilisha viapo vyao na kukabidhiwa dhana rasmi
za kazi zao.
Kama ilivyowekwa bayana na
Rais Jakaya Kikwete akiunda Tume ya Katiba ambayo ndiyo itakayoratibu maoni ya
wananchi kasha kuyapeleka kwenye Bunge la Katiba.
Wajumbe hao wa tume ya mabadiliko ya Katiba
walioapishwa na Rais Kikwete ni pamoja na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph
Warioba, Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Augustino Ramkadhani
pamoja na wajumbe wake ambao ni Profesa Mwesiga Baregu, Riziki Shahari Mngwali,
Dk. Sengodo Mvungi, Richard Lyimo , John Nkolo, Alhaj Said EL- Maamry, Jesca
Mkuchu, na Profesa Palamagamba Kabudi. Wengine ni Humphrey Polepole, Yahya
Msulwa, Esther Mkwizu, Maria Kasonda, Al-Shaymaa Kwegyir na Mwantumu Malale
pamoja na Joseph Butiku.
Wengine ni Dk.Salim Ahmed Salim, Fatma Said Ali, Omar Sheha Mussa, Raya Suleiman Hamad, Awadh Ali Said, Ussi Khamis Haji, Salma Maoulid, Nassor Khamis Mohammed, Simai Mohamed Said, Muhammed Yussuf Mshamba, Kibibi Mwinyi Hassan, Suleiman Omar Ali, Salama Kombo Ahmed, Abubakar Mohammed Ali, Ally Abdullah Ally Saleh. Pamoja na Katibu wa tume hiyo Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu wake Casmir Sumba Kyuki.
Wengine ni Dk.Salim Ahmed Salim, Fatma Said Ali, Omar Sheha Mussa, Raya Suleiman Hamad, Awadh Ali Said, Ussi Khamis Haji, Salma Maoulid, Nassor Khamis Mohammed, Simai Mohamed Said, Muhammed Yussuf Mshamba, Kibibi Mwinyi Hassan, Suleiman Omar Ali, Salama Kombo Ahmed, Abubakar Mohammed Ali, Ally Abdullah Ally Saleh. Pamoja na Katibu wa tume hiyo Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu wake Casmir Sumba Kyuki.
Macho ya watanzania kwa
sasa yanaelekezwa kwao, katika kuivusha salama Tanzania katika kulipatia taifa
katiba Bora itakoyoweza kudumu kwa kipindi kirefu bila malalamiko, kwa msingi
huu naungana na wanahabari wengine walio wahi kuandika kuwa “Sina shaka na Jaji
Warioba hasa kutokana na uzoefu wake katika masuala ya sheria na utendaji wake
katika tume kama hizo”.
Kama mheshimiwa Rais
Kikwete, alivyosema “pamoja na kazi hiyo wamewataka Watanzania kutambua kuwa
kazi ya tume hiyo ni kuratibu maoni ya Katiba mpya, na sio ya kujadili kuwepo
au kutokuwepo Muungano ila ni mchakato wa kupata katiba bora itakayoendesha
Taifa la Tanzania. Itafanya kazi ya kukusanya maoni kuhusu katiba na maslahi ya
Wananchi wa pande mbili zinazounda muungano”.
- “Kuzinduliwa rasmi kwa tume hii ya kuratibu maoni ya kupata katiba mpya ya nchi ni ishara tosha ya Taifa letu kuingilia katika historia iliyotukuka kwa kuanza safari mpya ya kuelekea kuzaliwa kwa Katiba mpya itakayotokana na maoni ya Watanzania wenyewe”.
- “Mwalimu Julius K. Nyerere, alisema mawazo hayapingwi kwa rungu bali hujibiwa kwa mawazon yaliyobora zaidi. Ni vema mtambue kuhamaki si jibu ila jambo jema ni kutoa mawazo yako yaliyobora zaidi. Kama Watanzania tutaifanya kazi hii kwa moyo tutafanikiwa kupata katiba iliyo bora itakalolilea Taifa letu katika miaka 50 ijayo,”
JUKUMU LA
WANANISHI NI LIPI?
- Kuhakikisha kuwa kila mmoja kwa uwingi wetu tuhakikishe tunatoa maoni kwa faida ya vizazi vyetu;
- Huu sio wakati wa kununuliwa na wana siasa katika ushawishi usio na faida kwa jamii ya Mtanzania
- Tuhakikishe kuwa maoni yetu yanasikika na yanatekelezwa Kama tume haitafanikiwa kuwafikia huko mliko msibweteke tafuteni njia mbadala wa kuhakikisha kuwa maoni yenu yanasikia.
KAZI YA
TUME NI IPI
- Kazi ya tume ni moja tu kufanya kazi hii katika maadili ya kweli bila upendeleo wa chama Fulani cha siasa au kikundi Fulani chenye uwezo au matakwa ya dini Fulani; tume iwatumikie wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
JUKUMU LA VYAMA
VYA SIASA
- Wakati huu wa mchakato wa kuratibu maoni vyama vya siasa vijitahidi kuacha kuwachanganya wananchi kwa kuwachakachua kimawazo ili kuhari au kudhoofisha nia njema ambayo iko ndani ya utaratibu mzima;
- Vyama vya siasa viwahamasihe wanachama wao katika kujumuika kutoa maoni na kuwaelimisha zaidi umuhimu wa kuchangia katika kutoa maoni.
- Ni matumaini yangu kuwa tume itaweza kukusanya maoni kwa kwa mapana na kwa uwezo wa hali ya juu kutoka na jinsi tume hiyo ilivyoundwa na umahili na uzoefu wa wajumbe wa tume hiyo.
MUNGU
IBARIKI TANZANIA NA IWEZESHE KUPATA KATIBA BORA KWA MAENDELEO YA WANANCHI WAKE
No comments:
Post a Comment