WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, April 4, 2012

MHESHIMIWA LIVINGSTONE LUSINDE KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI ARUMERU MASHARIKI


Je Mheshimiwa Lusinde alikuwa amesahau kuwa siasa ni Mchezo mchafu ambao unachezwa kwa mbinu ya hali ya juu, mpinzani wako anatafuta kila mbinu ili utereze tu nayeakumalize,bila kuchafua mazingira ya uadilifu na demokraisa ya kweli?

Itakuwa ni vyema kama atakumbuka maneno ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake ya kuwaaga wabunge mwaka 2010 aliwahi sema kuwa Nawashukuru kwa ushirikiano wenu na msaada wenu kwangu na kwa Serikali yetu.  Bunge letu limekuwa kielelezo kizuri cha ustawi wa demokrasia nchini.  Mmetoa hoja nyingi nzuri za kukosoa na kuishauri Serikali.  Ingawaje kuna baadhi ya nyakati maneno yalivuka mipaka ya staha,  lakini, napenda kuamini kuwa ilikuwa ni kwa nia njema!  Isitoshe elimu haina mwisho na wakati mwingine kukosea ndiyo kujifunza”.
narudia tena maneno hayo hayakustahili kusemwa na kiongozi kama yeye mwenye heshima kubwa ndani ya Taifa na chama chake; maneno yake yalivuka sana mipaka ya staha ambayo rais wetu alishawahi sema;
lakini pamoja na hayo yote tunamshukuru kwa kujitokeza hadharani kwa kupitia Clouds Redio katika kipindi cha Jahazi na kukiri kuwa alikuwa ameshindwa kuvumilia kwa namna alivyochokozwa na kutukana na upande wa pili; huu ni uungwana hata kama taifa litapokea msamahaa huu kwa hisia tofauti;
kwa wanasiasa wote na wale wote wanaopenda siasa, siasa inahitaji uvumilivu mkubwa sana, na kuweza kushinda ushindani ni nguvu ya hoja inatakiwa zaidi na sio ubabaishaji, siasa zilizo jaa ubabaishaji mwisho wake ni jazba na matusi na hatimaye mapigano

BAADA YA UCHAGUZI PICHA NA MAELEZO KWA HISAN YA MJENGWA BLOG. 
Mimi Mwanakijiji Ana Haya Kwenye Facebook Yake...

"Livingstone Lusinde akizungumza kwenye Clouds FM Jahazi anaomba radhi, msamaha kwa kauli na maneno ya matusi aliyoyatoa kwenye kampeni kule Arumeru Mashariki. Anasema ni maneno tu ya jazba ambayo hayana ukweli wowote. Kwa ufupi anasema anajutia kauli zake hizo. Asamehewe?"
Mungu Ibariki Tanzania

3 comments:

  1. ni jambo la busara sana wanasiasa wasiendelee kudharau kura ambazo tunawapigia kuwaweka madarakani, kwa kushindwa kututatulia mahitaji yetu ya msingi; hizi sera za matusi na za ubabaishaji sisi kama wananchi hatuzihitaji sera za matusi ambazo hazina faida kwa taifa;
    wanansiasa tafadhali sana tusaidie sisi wananchi kututoa katia lindi hili la umasikini,

    ReplyDelete
  2. KAMA NI MIMI HUYO NI KIONGOZI WA JAMII YA KAMA YA KITANZANIA.
    'aVULIWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE MADARAKA
    TUTAWASIKILIZIA WABUNGE WETU KWENYE BUNGE LIJALO KAMA WATALIJADILI SUALA HILO NA KULIPATIA UFUMBUZI.
    IKIWA WATAKAA KIMYA BASI HAYO YATAKUWA MAFUNZO YATOLEWAYO KATIKA VYUO VYA CCM

    ReplyDelete
  3. Yaani huyu fala ni bonge na mburula. Tatizo shule hakuna kabisa. Mabaamedi wengi wamemzidi shule angalao wamemaliza form IV. Nina wasiwasi kwamba hajui hata kusoma na kuandika huyu mbuzi.

    ReplyDelete