UPDATE/TAARIFA MPYA kutoka kwa bw. Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi, Zanzibar:
Mzee mmoja mkazi wa Kitopeni mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar Bw. Ali Khamis Ali (65), ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiojulikana.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja, ACP Ahmada Khamis, alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 8.00 mchana huko kwenye eneo la Kitope mashambani.
Alisema Marehemu Mzee Ali ambaye pia ni imamu wa Msikiti wa Kitope mkoani hapo, alikuwa amekwenda shambani kwake kukagua mazao yake ikiwemo minazi.
Amesema alipofika shani hapo aliwaona vijana waliokuwa wakiangua nazi na wengine wakiwa chini ya mnazi wakiziandaa ili kuondokanazo kwa maana ya kuziiba.
Kamanda Ahmada amesema baada ya Marehemu kuwabaini wezi hao, inaonekana kuwa alianza kupandana nao lakini walimzidi nguvu na kumchona na kitu hicho chenye ncha kali ambacho kinaaminika kuwa ni kisu.
Amesema eneo la tukio walikuta rungu na ala la kisu ninachoaminika kumuulia marehemu. Amesema eneo la tukio hilo pia kulikuwa na damu nyingi na lilikuwa limevurugwa kutokana na mapambano.
Kamanda alisema baadhi ya wananchi wameitambua rungu hiyo kuwa ilikuwa ya marehemu aliyokuwa akiitumia kwa kulindia mazao yake ambayo mara kwa mara yamekuwa yakiibwa na wezi.
Kamanda Ahmada amesema kuwa pamoja na marehemu huyo kuuawa lakini inaonekana pia mmoja wa wezi hao wa mazao naye amejeruhiwa katika mapambano hayo kwani kulionekana michirizi na matone ya damu ya mtu aliyeondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.
Amesema uchunguzi wa tukio hilo umeanza na amewataka wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona watu ama mtu mwenye majeraha ili akamatwe kwa kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Ahmada alisema kuwa mauaji hayo ni ya kuwania mali na ametaka kutohusishwa na hisia za imani yoyote ama za kisiasa, kishirikina, wivu wa kimapenzi, kulipiza kisasi ama imani za kidini.
“Haya ni mauaji ya kawaida na hayana hisia zozote. Ni mauaji kama mauaji mengine yanayotokea katika maeneo mengine ya nchi yetu.” Alisema Kamanda Ahmada na kuwaonya wananchi kutoweka hisia tofauti na tukio lenyewe.
Amewaomba pia Waandishi wa Habari kutowema maoni yao binafsi wanaporipoti taarifa za tukio hilo ili kuepuka kuwatia hofu wananchi.
Nukuu ya taarifa via Said Powa blog inasema:--
Imam wa Msikiti wa Mwakaje huko mkoa wa Kaskazini, Unguja, Zanzibar ameuawa jana baada ya kupigwa na kukatwa kwa mapanga hadi kufa.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya saa 8 na kumtaja aliyefariki kuwa ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.
Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada alisema tukio hilo limetokea majira ya saa 8 mchana wakati Sheikh Khamis akiwa shambani kwake la minazi huko Kidoti ambapo walipotokea watu kadhaa na kumpiga mapanga sehemu za shingoni mwake na kusababisha kifo chake muda mfupi.
Alisema baada ya tukio hilo, watu walimchukua na kumkimbiza hospitali lakini kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki dunia wakati akiwa njiani. Mazishi ytafanyika baada ya kuchukuliwa vipimo na wataalamu wa afya.
Kamanda Ahmada ametoa wito kwa wananchi kutopuuzia taarifa za watu ambao wanawashuku na wenye kuleta maafa yakiwemo mauaji hapa nchini, kwani kuwaficha wahalifu ni kuendeleza utamaduni usiofaa katika jamii ambayo imeanza kuharibika kutokana na mauaji hayo yanayoendelea kila kukicha.

Hili ni tukio la nne ndani ya miezi mitatu kwa viongozi wa dini kudhuriwa na/au kuuawa.
- Novemba 2012: Sheikh Fadhil Suleiman Soraga kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya wakati akifanya mazoezi nyakati za asubuhi karibu na nyumbani kwake Magomeni.
- Desemba 2012: Padre Ambrose Mkenda alipigwa risasi na kurejuhiwa vibaya na watu wasiojulikana wakati alipokuwa anaingia nyumbani kwake huko Tomondo, Unguja.
- Februari 2013: Parde Evaristus Mushi aliuawa huko Beit El Raas wakati akikaribia Kanisani kuongoza ibada.
- Februari 2012: Sheikh Ali Khamis liuawa huko shambani kwake Kidoti, Mkoa wa Kaskanizini Unguja.
- source: wavuti.com
No comments:
Post a Comment