Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (Mb) akimuelekeza jambo Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo. Mh Philipo Augustino Mulugo kabla ya kuanza kutangaza matokeo ya kidato cha nne mbele ya baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali, kwenye makao makuu ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam
TATHMINI YA
UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
8.1 Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i) Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;
(ii) Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na
(iii) Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.
8.2 Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:
(i) Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule. Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.
(ii) Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.
(iii) Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.
(iv) Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.
(v) Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.
Source: http://www.wavuti.com/

UCHAMBUZI WA UKADIRIFU:
ELIMU NI HAKI YA
MSINGI KWA WANAFUNZI WETU.
Jedwali hapo chini
linaonyesha matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha nne, matokeo haya yameleta
simanzi kwa wananchi wengi ambao wameyaita ni janga la taifa letu kutokana na
ukweli kuwa kiwango cha kufeli kimekuwa ni kikubwa mno katika matokeo haya ya kidato
cha nne ya mwaka 2012
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
Daraja | Idadi ya Wavulana | Idadi ya Wasichana | Jumla |
I | 1,073 | 568 | 1,641 |
II | 4,456 | 1,997 | 6,453 |
III | 10,813 | 4,613 | 15,426 |
I-III | 16,342 | 7,178 | 23,520 |
IV | 64,344 | 38,983 | 103,327 |
0 | 120,664 | 120,239 | 240903 |
Maswali mengi yameulizwa
kwa nini taifa limefikia katika hali kama hii; je lawawama ziende kwa serikali
kwa kushindwa kutoa kipaumbele katika mfumo mzima wa elimu ya watoto wetu? Au
ni tatizo la wanafunzi wetu (watoto wetu) kuto kuwa makini katika masomo yao
(lack of seriousness)? Lakini tatizo hasa nini wakati taifa linafahamu wazi
kuwaELIMU NI HAKI YA MSINGI?
Ni ukweli ambao haufichiki
kuwa Tanzania haitaweza kuendelea na kustawi bila kuwa na elimu nzuri kwa
watoto wetu ambao ndio msingi wa kesho wa mustakabli wa taifa letu. Hata kama
tutakataa kwa msingi wowote ule ukweli utabaki pale pale kuwa elimu yetu
tukilinganisha na mifumo ya elimu ya nchi nyingine hasa zile ambazo zimeendelea
na hata pengine zinazo endelea kama Tanzaania au zinazotuzunguku mfumo wetu wa
elimu sio mzuri
Serikali inanadi vipi sera
za elimu bora?
Serikali inatueleza kuwa
katika miaka 50 ya uhuru imefanikiwa
kupanua fursa za watoto na vijana wetu wengi sana kupata elimu ya
awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.
Na kwa kutambua mafanikio haya yote serikali
bado inaendelea kutoa kipaumbele cha kwanza kwa bajeti ya elimu ili
iweze kuajiri walimu wengi zaidi, kuongeza vitabu na vifaa vya kujifunzia na
kufundishia.
kuongeza matumizi ya teknohama katika
utoaji wa mafunzo pamoja na kujenga uwezo wa wanafunzi na waalimu
kiteknolojia ili kwenda sambamba na karne hii ya utandawazi.
Aidha, inaendelea na mpango wake wa kujenga maabara za
sayansi katika sekondari zetu zote.
Serikali imesisitiza adhima ya kuchuakua hatua thabiti
za kuboresha maslahi na mazingira ya kufanyia kazi ya walimu na
watumishi wa sekta ya elimu.
Serikali imekusudia kutenga pesa za kutosha katika
kufikia malengo haya.
Tatizo liko wapi?
- Msongamano wa wanafunzi katika shule zetu ambao hauendani na bajeti inayotolewa, vifaa vya kufundishia; vyumba vya kusomea ambavyo vitaweza kuwagawanya wanafunzi katika idadi ambayo ni rahisi kufundishika na kuelewa na kusaidiwa; Hivyo hushusha kiwango bora cha elimu;
- Ubovu wa huduma za jamii kama barabara, hospitali, maji safi na salama; ukosefu wa mishahara mizuri ya kuwamotivate walimu zaidi kuingia katika taaluma hii; ni kweli kuwa elimu ni silaha pekee ambayo inaweza kutusaidia kubadilisha dunia na maisha yetu, kwa msingi huu wale ambao wana elimu sio tu elimu bali elimu bora wananafasi kubwa ya kufanikiwa;
Je sisi tunataka nini?
Taifa linahitaji
utekelezwaji wa haki hii ya msingi kwa vijama wetu yaani:
Elimu bora ambayo
inatokana na walimu bora ambao wameshiba na wameridhika ma maisha yao kwa
kupata haki zote wanazostahili kupata na wanawajibika kwa moyo bila mashaka
Mitaara ya elimu
itayarishwe iendane na masomo yanayolingana na hali halisi ya maendeleo ya
dunia ya sasa pamoja na masomo ambayo yanawavutia wanafunzi kujitafutia zaidi
jitihada za kusoma?
Sababu nyingine
zinazowafanya watoto wetu wasifanye vizuri shuleni ni pamoja na wanafunzi
kuchukia shule kutokana na sababu za kitaaluma na kimazingira, shule zetu
nyingi zina kosa vifaa muhimu ya kufundishia na kujifunza shule kama inakosa
vitabu vya kiaada vifaa vya mahabara je unategeme kuwa kutakuwa na ubora wa
elimu hapo? Mimi nasema hapana na tusitegemee miujiza kutoka katika shule zetu
za serikali ambazo watoto wetu wengi ndiko wanakosoma.
Pale tutakapo amua kuacha
maneno na kuanza kutekeleza maneno yetu kwa vitendo ndipo tutegemee kuona:
watoto wetu wakifikia malengo yao ya elimu kupitia elimu bora na kufanikiwa
kuondoa umasikini kwa kiwango kikubwa sana.
Pengine kwa akili tu ya
kawaida tunaweza kusema kuwa serikali yetu inahusika katika kuharibu mfumo
mzima wa elimu, kwa nini nasema hivi kwa msingi huu mmoja mkubwa elimu inapasa
iwaguse na kuwahusu moja kwa moja watoto wetu; mahitaji yao yanatakiwa yatiliwe
mkazo kwanza kabla ya mambo mengi ya serikali,
Inatakiwa mtoto wa
kitanzania kwenda katika shule nzuri inatakiwa iwe ni haki yake ya kikatiba,
watoto wafundishwe na walimu ambao ni wazuri ambao wanapokea mishahara mizuri
na wanavifaa vizuri vya kufundishia
KWA NINI SHULE BINAFSI ZINAFANYA VIZURI?
Nini kinatokea katika shule za binafsi wana walimu
wazuri ambao wanalipwa vizuri na wanavifaa vya kutosha sasa nini tutegemeenini kutoka katika shule kama hizi ni wazi kuwa matokeo yao ya mitihani itakuwa ni daraja la kwanza na watoto wakifeli ni daraja la
pili;
katika mafanikio ya ufaulu wao wazazi nao wanamchanga mzuri sana katika
maendeleo ya watoto wao, wazazi wanahusishwa katika maswala ya kitaaluma na ya kijamii sambamba na watoto
wao; mzazi anajua ratiba ya kitaaluma na maendeleo ya mtoto/mwanafunzi utaratibu wa shule unampa nafasi ya pekee kama mwalimu jamii ambaye anaendeleza nidhamu na tabia ya usomaji wa mtoto/mwanafunzi nje ya mazingira ya shule na katika maisha
ya kawaida ya mtot ndani ya familia;
Kama Taifa tukifanikiwa kufikia hatua kama hii kama shule hizi na jamii nyingine zilizoendela zinavyofanya tutakuwa tumesonga mbele katika mafanikio ya elimu ya watoto wetu; ni kitu kizuri kuona wazazi wakishiriki moja kwa moja katika maisha ya kawaida ya watoto wao na mtoto/mwanafuzni asipomwona mzazi wake katika maswala mbalimbali ya shule anasikitika na ndani ya demokrasia ya mtoto mwenye nidhamu anamuuliza mzazi wake Baba/Mama leo hujeangalia kazi zangu au leo hukuja katika michezo yetu na hukufanikiwa kuniona jinsi nilivyocheza vizuri, hali hii hatimaye inamwumiza mzazi na inajenga uwajibikaji wa wazazi kwa watoto wao na kuleta ufanisi mzuri wa kitaaluma shuleni.

Shule zetu zisijikite sana
katika maandalizi ya mitihani tu zijikite vile vile katika kuwasaidia watoto
wetu katika kujiandaa na maisha yao.
JE WANAFUNZI WANAOSOMA
SHULE ZA KATA WANA HAKI SAWA NA WALE WA MIJINI? JE TUNAJADILI PIA MATOKEO YA
SHULE ZA KATA/VIJIJINI?
Je shule zetu za vijijini zinafikiwa
vipi katika maendeleo ya elimu?
Tunafahamu kuwa wazazi
wetu wengi ambao wako vijijini hawawezi kuwasaidia watoto wao kwa vile hata
wenyewe wahajeelimika vyakutosha na hata wakati mwingine wanaona aibu kujadili
mambo ya shule kwa vile hawajui;
Matokeo yake wanafunzi
wengi wanajikuta wakishiriki zaidi katika shughuli za kilimo ( Elimu ya
Kujitegemea na kuwafanyia walimu wao kazi majumbani);
NINI KINAWAFUKUZA WALIMU
WAZURI KAMA WAKO KATIKA SHULE ZA KATA/VIJIJI?
Kutokana ubovu na huduma
duni za jamii si rahisi kuwapata walimu bora kwenda kufundisha vijijini wengi
watapendelea kubaki mijini;
Hata serikali inajikuta
katika wakati mgumu wa kupeleka huduma kama vitabu, nafasi nyingi ambazo
zimezcha wazi kutojaza mara moja, hata pale zinapojazwa zinakuwa na walimu
ambao sio wazoefu na wazuri kitaaluma.
Ni mara nyingi sana walimu
ambao wanfundisha katika shule za vijijini wanaweza wakawa wanafundisha muda
mfupi ukilinganisha na wenzao wa mijini kutoka na sababu kama vile wanatakiwa
kutembea umbali mkubwa kwa ajili ya kwenda kutibiwa, kuchukua mishahara, kwa
ajili pengine ya kwenda kwa ajili ya mafunzo ya au kutembelea familia
zao;
Wlimu wengi wanakuwa
hawana nyumba za karibu na shule pengine na wakati mwingine inawapasa kutembea
kwa miguu umbali mkubwa kwenda kufundisha asubuhi hali hii inaweza kusababisha
kuanza vipindi kwa kuchelewa;
Swala la ukaguzi na
utendaji wa walimu ni tatizo pia kutoka na tatizo sugu la usafiri hata wakaguzi
hawatembelei shule hizo kuona maendeleo yake mara kwa mara;
HITIMISHO
Lazima tukubali kuwa kuwa
na walimu bora ambao wanavifaa vinavyotakiwa kwa ajili ya elimu bora huleta
tofauti kubwa sana kwa wanafunzi wetu na sifa kubwa kwa taifa letu; taifa
lisipokuwa tayari kubadilika tutaendelea kunyosheana vidole kuhusu matokeo ya
wanafunzi wetu kila mwaka kama jedwali la hapo chini linavyoonyesha, kwa ujumla
ni aibu kubwa kuona watoto wetu wanafeli kwa kiasi kikubwa namna hii, na
kubaliana na wengi ambao wamediriki kusema kuwa hili ni janga la kitaifa ni
vyema kama tulitafutia ufumbuzi wa haraka; washauri wa serika li yetu mnashauri
nini?
Na lazima tukubali kuwa
elimu bora kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu ni haki ya kila mwanafunzi katika
jamii hii ya kitanzania; viongozi wetu wanapaswa kulijua hilo na kulielewa hilo
na kulitekeleza kwa moyo woto na kwa faida ya wote;
Swali la kujiuliza ni hili
pamoja na faidia zote zitokanzao na elimu, kwa nini serikali yetu bado haioni
faida ya kuwekeza zaidi katika elimu? “Imesahau kuwa Elimu ni mtaji wa msingi
kwa jamii?” Je serikali inaogopa kuwekeza kwenye elimu kwa sababu ya ushindani
kutoka kwa wananchi katika kuwaongoza? Ni ukweli kuwa jamii ikiwezesha kwa
elimu bora matokeo yake ni kuwa hawatakuwa tayari kukubali kuburuzwa na
kudanganywa danganya pengine na sera ambazo hazieleweki;
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WAPE HEKIMA ZAIDI VIONGOZI WETU KWA KUSHIRIKIANA NA WAZAZI WAWEZE KUTUTOA HAPA TULIPOKWAMA KIELIMU KWA FAIDA YA TAIFA HILI;
No comments:
Post a Comment