MAUAJI YA MAPADRI ZANZIBAR
Uchambuzi yakinifu kwa kuzingatia utaalamu wa makosa ya jinai
1: UTANGULIZI
Watu wasiojulikana walimpiga risasi kichwani Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar siku ya Jumatano (boxing day) tarehe 26 Desemba 2012.Tukio hilo lilitokea baada ya Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan Zanzibar kudai kuwa kumekuwepo vipeperushi vilivyosambazwa vikiwatisha watu wenye imani ya Kikristo na kuiomba serikali iongeze ulinzi na kuimarisha usalama. Kwa bahati, Padri Mkenda hakufa na anaendelea na matibabu.
Jumapili 17 Februari 2013, Padre mwingine wa Kanisa la Katoliki Zanzibar, parokia ya Minara Miwili lililopo mji mkongwe,Padri Evarist Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa Risasi utosini na watu wasiojulikana. Padri huyo alikuwa akielekea kuendesha misa ya saa 3 asubuhi kwenye kanisa la Mt. Theresia na akiwa eneo la Mtoni alisimamishwa na watu wawili ambapo mmoja wao alimpiga risasi utosini na kufariki papo hapo.
Hili ni tukio la pili kwa Mapadri kushambuliwa huko Zanzibar ndani ya kipindi cha miezi miwili. Cha ajabu ,mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa hukusika na matukio hayo.
2: Uchambuzi wa Kijinai
Matukio haya ni ya kupangwa na yanafanywa na serial killersna wahusika ni walewale kwa sababu zifuatazo:-
1) Waliompiga risasi kichwani Padri Mkenda tarehe 26 Desemba 2012 na waliompiga irsasi klichwani Padri Mushi ni walewale kwa sababu matukioyote mawaili pikipiki aina ya vespa imetumika.
2) Mauaji yote yametokea katika eneo moja au maeneo ya jirani. Ni Zanzibar ileile…..na wauaji hawaishi mbali na maeneo ambayo wamefanya matukio.
3) Mauaji hufanyika wakati wa asubui.
4) Bila kubisha ni mauaji ya kidini.
5) Makanda ya risasi katika tukio la Padri Mkenda na Padri Mushi yanaweza kuwa maganda ya bastola ya aina moja.
6) Aina ya uuaji …kwa kupiga risasi kichwani umefanyika katika matukio yote.
7) Kitendo cha kumpiga mtu asiye na kosa (ambaye hawezi kujitetea) risasi kichwani ni ushahidi kuwa wauaji walidhamiria kuuwa.
8) Mauaji yote haya inaonesha kijinai yamepangwa kwa ustadi mkubwa kabisa. Wauaji ni wawili ila wana watu wanaowaelekeza kuuwa nyuma yao.
9) Mauaji yote hufanyika jumapili au siku ya ibada wakati mapadri huwa wanaenda kanisani kwa sababu ni siku ambazo hakuna watu wengi katika maeneo husika.
10) Kwa vile wanaolengwa ni mapadri ni vigumu kusema mauaji haya si ya kidini hasa ikizingatiwa hali ya vujo za kidini ilivyo Zanzibar na nchini kwa ujumla.
11) Wauaji hawa huitwa serial killers kwa vile huuua mtu mmoja na kisha kuendelea kuuwa watu wengi na iwapo hawatakamatwa huendelea kuuwa zaidi. Mfano wa watu hawa ni Ndugu Carl Eugene Watts wa huko Texas, Marekani ambaye kati ya mwaka 1970 hadi 1982 alikuwa ameua watu zaidi ya 100 wote wakiwa wasichana/wanawake wadogo, alipenda kuwaua nyakati za asubui kwa kuwanyonga na wengi wakiuliwa siku ya jumapili. Muuaji huyu alipewa jina la utani ‘The Sunday Morning Slasher’…yaani muuaji wa jumapili asubui.
12) Kwa vile wauaji ni wawili kwa mujibu wa mashuhuda waliowaona basi mauaji haya hupangwa na pia hugawana majukumu.
13) Pia kuna uwezekana kuwa wauaji hushirikisha watu wengine ambao huja eneo la tukio kuangalia hali ya usalama na vilevile wauaji hawa huwasiliana kwa simu kujua muda ambao wanayetaka kumuua huwa yupo nje ya nyumba yake au barabara.
14) Wauaji hushirikiana na wahalifu wengine wanaokuwa jirani na eneo la tukio ili kujikinga.
15) Kabla ya mauaji kutendeka wauaji hawa hufanya mikutano uso kwa uso, huwasiliana kwa njia ya simu, pia hutumia lugha maalum ambayo ni ya kwao tu, hukusanya taarifa za watu wa kuwaua, wana viongozi wao wanaowaelekeza na wana watu wanaowasaidia.
16) Lengo la wauaji hawa ni kuuwa. Padri Mkenda alisalimika kwa bahati tu. Lakini akijaribu kurudi Zanzibar lazima atamaliziwa kwani wauaji hufurahi wanapoua na kuumua mtu ambaye walishindwa kumuua ni furaha kwao.
17) Baada ya kushindwa kumuuwa Padri Mkenda ; wauaji walipanga wasikosee katika kumuua Padri Mushi ndio maana risasi iliengwa vizuri utosini kuhakikisha anakufa papohapo.
3: Tabia za wauaji wa mapadri wa Zanzibar
Ukiangalia jinsi mapadri hawa wa Zanzibar walivyopigwa risasi utagundua kuwa wasifu na saikolijia ya jinai ya wauaji hawa ni zifuatazo:-
1) Wauaji umri wao ni kati ya miaka 19 na 46, wanaume, ngumu kwao kupata kazi za maana, wana matatizo ya kisaikolojia na wana imani kali ya dini yao. Wauaji hawa hata kama wana ajira ni vigumu kukaa na ajira moja kwa muda mrefu.
2) Wauaji wote ni waumini wa dini moja ndio maana hulengavictims wao kutoka dini nyingine.
3) Wauaji ni watu ambao hawana kazi za kudumu.
4) Wauaji ni watu ambao maisha yao ya utotoni hayakuwa mazuri sana.
5) Wauaji ni watu ambao hawakufanya vizuri shuleni na darasani.
6) Wauaji ni watu ambao misingi yao ya maisha inayumba.
7) Wauaji ni wabinafsi, wabaguzi wa kidini, hawana huruma, wana penda kusifiwa na wanapenda kujipendelea.
8) Mpango wa siri wa wauaji hawa ni kuuwa mapadri au waumini wa dhehebu fulani lakini hasa mapadri.
9) Wauaji hawa wasipokamatwa wataendelea kuuwa mapadri.
10) Hakuna mtu atakaye weza wazuia kuuwa mapadri labda tu wakikamatwa na dola.
11) Kwa hali fulani inaonesha wauaji wana elimu ndogo sana ya masuala ya kidunia.
12) Wauaji ni wapenzi wa vyombo vya habari na hupenda kusoma na kutunza magazeti hasa yanayohusu matukio ya mauaji/uhalifu wanayoyafanya.
13) Wauaji hawaui kwa ajili ya kutafuta pesa au mali bali wanaua ili wapate umaarufu kwa wanaowatuma (attention seekers).
14) Wauaji ni watu wenye kipato cha kawaida, kati au chini kabisa.
15) Wauaji wanaamini wanaua kwa sababu ya dini na hivyo hawana kosa wala hatia.Jambo ambalo si sahihi. Huko Uingereza mwaka 1993, msichana mwenye miaka 17,Shafilea Iftikhar Ahmed aliuwawa na wazazi wake kwa vile alionekana hafuati masharti ya dini za wazazi wake. Wazazi wake waliamini kuwa kuuwa ili kulinda imani ya dini ni jambo sahihi.
16) Wauaji ni wafuasi ambao wamefundishwa kuwa dini nyingine ni adui jambo ambalo si sahihi.Wanasahau kuwa vitu vingi vinanyowazinguka na wanavyovitumia pia huwa vimetengenezwa na watu wa dini nyingine. Mfano wauaji wanatumia pikipiki za vespa scooter ambazo hutengenezwa na nchi ambayo si ya kidini. Vespa ni neno la kiitaliano lenye maana ya wasp yaani mdudu arukaye jamii ya nyuki.
4: Mifano ya mauaji kama hayo hapa duniani
Dr. Harold Fredrick Shipman wa Uingereza ni moja wapo wa serial killer dunia iliwai kumpata. Kati ya mwaka 1974 hadi 1998 aliuwa watu aidi ya 250 huko Uingereza. Wengi wa aliwaua walikuwa wagonjwa wake wazee na watu wenye umri mkubwa. Wengi wa aliowaua walikuwa wanawake. Mtu mwenye umri mdogo aliyemuua alikuwa na miaka 41. Dr. Shipman, tofauti na wauaji wa Zanzibar wanaotumia risasi, Dr. Shipman alikuwa akiuwa wagonjwa wake kwa kutumiadiamorphine na pethidine. Pia yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa anaandika katika vyeti vyao vya vifo sababu za vifo vyao.
Dunia iliishapata serial killers ambao huwa wanauwa watoto tu, wanawake peke yao, washoga peke yao, wanaume peke yao, rangi fulani peke yao, makahaba peke yao n.k. Mauaji haya nia anina mpya nyingine ya mauaji.
5: Ushauri kwa polisi
Polisi na wapelelezi wanapaswa wajue aina ya vespailiyotumika, rangi yake, aina ya matairi, alama za matairi, rangi ya nguo za wauaji, wajihi na sura za wauaji kwa kusikiliza maelezo ya mashahidi walioshuhudia mauaji, namba za usajiri za vespa hiyo hata kama walioshudia walikariri namba moja tu. Si lazima wakariri namba zote.
Ni vema polisi waandae mtego mwingine wa kuwakamata wauaji kwani watarudia tena kuuwa ndani ya siku 30 hadi 120 kutoka tukio la hivi karibuni. Si sahihi kwa polisi kupeleleza bila kuandaa mtego makini.
Polisi hawawezi kushughulikia suala hili kwa umakini kwani hata katika nchi zilizoendelea kama Uingereza na Marekani; polisi hawakufaulu hadi wataalamu wa makosa ya jinai waliposhirikishwa. Anaweza kujitolea kuwasaidia polisi katika upelelezi kama wataitaji msaada wangu. Hatua za haraka zisipochukuliwa mapema hali itakuwa mbaya zaidi.
NB mwandishi wa uchambuzi huu ni mwanasheria jijini Dar es salaam
source: lukwangule blog
No comments:
Post a Comment