Fidelis Butahe
KITENDO cha kuzitupa hoja zilizowasilishwa bungeni na wabunge John Mnyika wa Chadema na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, kimesababisha chama kikuu cha upinzani Chadema, kuamua kufanya maandamano nchi nzima ili kuwashtaki kwa wananchi Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai.

Maandamano
hayo yatatanguliwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika kesho Viwanja vya Temeke
Mwisho, Dar es Salaam, sanjari na kuwapokea wabunge wake wanaorejea kutoka
kwenye mkutano wa Bunge uliomalizika jana Dododma.
Chadema
kimedai kuwa kanuni za bunge zina upungufu na kwamba kitendo cha spika na naibu
wake kuzima hoja za wabunge hao kinadhihirisha kuwa viongozi hao wa mhimili huo
wa taifa wameshindwa kulinda hoja zenye maslahi kwa wananchi na wameligeuza
bunge kuwa ‘kijiwe cha CCM’.
Hoja zilivyozimwa
Wiki hii, katika kikao hicho cha Bunge, Mnyika aliwasilisha hoja binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, hoja hiyo ilizimwa na Ndugai, ambaye baadaye aliruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, hatua ambayo iliwafanya wabunge wote wa upinzani kusimama kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua hiyo ya Ndugai wakidai kwamba Naibu Spika huyo amevunja kanuni alizopaswa kuzisimamia.
Kitendo
hicho pia kilisababisha kikao kuahirishwa kabla ya muda uliopangwa, huku hoja
ya Profesa Maghembe ya kupendekeza kuondolewa bungeni kwa hoja ya Mnyika
ikiungwa mkono na wabunge wa CCM.
Sambamba na tukio hilo Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliwasilisha hoja binafsi akidai Serikali haina mitalaa ya elimu na kutaka Bunge kuunda kamati teule kuchunguza udhaifu huo.
Hata
hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali, badala yake Ndugai aliunda kamati kuichunguza
mitalaa hiyo kuangalia uhalali wake, kabla ya kuthibitishwa na Bunge.
Licha ya kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk
Shukuru Kawambwa kuwasilisha bungeni mitalaa hiyo juzi, ambapo Mbatia alisema
hakubaliani na mitalaa hiyo kwa maelezo kuwa kilichowasilishwa siyo
kilichoahidiwa awali na Dk Kawambwa.
Tamko la Chadema
Katika tamko la jana la Chadema mbele ya waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaira alisema :“Kwanza tutawapokea wabunge wote wa upinzani pale Ubungo na baadaye yataanza maandamano kuanzia eneo la Tazara, hadi katika Viwanja vya Temeke Mwisho, ambako utafanyika mkutano mkubwa wa hadhara.”

Akizungumzia
kibali cha Jeshi la Polisi, Kigaira alisema tayari wameshatoa taarifa, uwanja
wanaotarajia kufanya mkutano huo siku ya Jumapili hautakuwa na shughuli
nyingine, hivyo hakuna kisingizio chochote wala sababu za kuzuiliwa kwa mkutano
na maandamano hayo.
Alisema
kilichofanywa na viongozi hao wakuu wa Bunge, huku Serikali ikiwataka
wananchi kuamini kuwa wabunge wa Chadema ni wakorofi ni sawa na ‘’kubaka
demokrasia na ubabe wa kiti cha Spika.’’
“Kazi
ya Bunge ni kuibana, kuihoji Serikali na kuwapigania wananchi, tutafanya
mkutano kuwaeleza ukweli wananchi na kamwe hatuwezi kukubali kuona spika na
naibu wake wakiligeuza Bunge kuwa kijiwe cha CCM,” alisema Kigaira.
Alisema kwa mujibu wa kanuni ya 57 na 58 ya Bunge, waziri au mbunge, hawezi kuizima hoja ya mbunge mwenzake na kwamba kitendo cha spika kuruhusu hoja ya Mnyika kutupwa ni kinyume na kanuni hizo.
“Tumeamua
kuwapokea wabunge wote wa upinzani kwa kuwa wote walishirikiana bungeni, lakini
pia tumevialika vyama vyote vya siasa katika kambi ya upinzani kuhudhuria
maandamano na mkutano wetu,” alisema Kigaira na kuongeza:
“Watanzania
ndiyo wenye uamuzi, sisi tutakachokifanya ni kuwaeleza ukweli tu jinsi hali
ilivyo kwa sasa huko bungeni, wao ndiyo watapima kama spika anafaa au hafai na
hatimaye kuondoa umungu mtu wao.”
Kigaira alisema kuwa baada ya mkutano huo wataendelea na mikutano katika kanda 10 nchini, zinazojumuisha mikoa 30 na kwamba hadi mwishoni mwa mwezi huu watakuwa wamemaliza mikutano yote.
“Tunataka
Watanzania wachukue hatua,maana Bunge lipo kwa ajili ya Watanzania ambao ndiyo
wenye uamuzi wa kila kitu” alisema Kigaira na kuongeza:
“Mbona
wakati Spika wa Bunge ni Samwel Sitta, kulikuwa hakuna vurugu za namna hii?
Mhimili pekee unaowakilisha kilio cha wananchi ni Bunge, lakini hivi sasa
imekuwa kinyume chake.”
source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment