Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu
Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie
wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme
mjni Moshi jana
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la
Askofu Mstaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus
Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu
Mfalme, mjini Moshi jana
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu
Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie
wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme
mjini Moshi Jana
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
Bungeni (KUB) akitoa heshima zake za mwisho kwa Askofu Mstaafu wa Kanisa
Katoliki nchini, hayati Amedeus Peter Msarikie, katika misa ya kumuaga
iliyofanyika jana katika Kanisa la Kristo Mfalme, Mjini Moshi.Picha na Freddy Maro-IKULU
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Alhamisi, Februari 14,
2013 ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo
la Moshi na kutoka sehemu nyingine nchini, kumzika Askofu Mstahivu
(Bishop Emeritus) Amedeus Peter Msarikie.
Rais Kikwete aliwasili kwenye
Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi kiasi cha saa sita na dakika
tano mchana kuungana na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin
Mkapa na mamia kwa mamia wananchi kwa ajili ya mazishi ya Askofu
Msarikie ambaye alifariki dunia Alhamisi iliyopita, Februari 7, 2013 kwa
ugonjwa wa saratani katika hospitali moja mjini Nairobi, Kenya.
Mara baada ya kuwasili, Rais
Kikwete alitia saini kwenye kitabu cha maombolezo na ikaanza ibada ya
mazishi ilivyohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi wakiwamo maaskofu
zaidi ya 20 kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini.
Mwili wa Marehemu Msarikie
uliteremshwa kaburini kiasi cha saa saba na dakika 35 ndani ya Kanisa
hilo na Rais Kikwete akaweka udogo kwenye kaburi na baadaye shada la
maua.
Akizungumza kwenye mazishi hayo,
Rais Kikwete amemwelezea Askofu Msarikie ambaye alikuwa Askofu wa Jimbo
la Moshi kwa miaka 26 kama “kiongozi shupavu wa kiroho ambaye aliwalea
vyema kondoo wa bwana. Lakini pia alikuwa kiongozi hodari kwa maendeleo
ya jamii yaliyowanufaisha waumini wake na hata wale wa madhehebu na
dini nyingine.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Kwa
kweli sote tumepoteza mtu muhimu. Tunamfahamu marehemu Baba Askofu
Msarikie kwa mema mengi aliyowatendea watu wa jimbo lake, ya kiroho na
ya maendeleo. Mimi binafsi, wana-moshi na Watanzania kwa ujumla
tutamkumbuka na kumuenzi Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi
aliyowafanya wanadamu wenzake na nchi yetu.”
source: Haki Ngowi
No comments:
Post a Comment