Wachezaji wa Timu
ya Taifa ya Nigeria,wakishangilia baada ya kutwaa Taji ya Mataifa ya Afrika
kufuatia kuifunga Burkina Faso bao 1-0.
NIGERIA ilitawala mchezo wa fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika na kuifunga Burkina Faso bao 1-0 na kutwaa taji mjini, Johannesburg,
Afrika Kusini.
Sunday Mba alikuwa shujaa wa ushindi wa Nigeria (Super Eagles)
baada ya kufunga bao pekee dakika tano kabla ya filimbi ya kutenganisha nusu ya
mchezo huo mkali ulioshuhudiwa na watazamaji 85,000.
Wilfried Sanou angeweza
kusawazisha bao hilo kwa Burkina Faso (Stallions) katikati ya kipindi cha pili,
shukrani kwa kipa wa Nigeria Vincent Enyeama aliyecheza vizuri kuokoa hatari
hiyo.
Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Nigeria hatua ya fainali tangu mwaka 2000, na walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji mbele ya Burkina Faso, taifa dogo Afrika Magharibi.
Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Nigeria hatua ya fainali tangu mwaka 2000, na walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji mbele ya Burkina Faso, taifa dogo Afrika Magharibi.
Burkina Faso haijawahi kuifunga Nigeria katika mechi 12
walizokutana katika mashindano mbalimbali, na hiyo ilitosha kuipa Nigeria
nafasi ya kushinda mchezo. Efe Ambrose alikuwa na nafasi tano za kufunga
kipindi cha kwanza, lakini ya kukumbukwa zaidi ni pale alipopiga juu mpira
akimalizia kiki ya adhabu ndogo kutoka kwa Victor Moses ndani ya dakika saba
tangu kuanza mchezo.
Nigeria waliotawala mchezo kwa kiasi kikubwa, walikaribia
kufungwa kama siyo, Aristide Bance kupoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya
shuti lake la mita 25 kukosea shabaha na kwenda nje ya lango huku.
Nigeria wangeweza kufunga bao la pili kama Ideye angetumia
vizuri pasi aliyopewa kuusindikiza kirahisi mpira wavuni, lakini akaishia
kupiga nje.
Huo ni ubingwa wa tatu kwa Nigeria, lakini wa kwanza kwa tangu
mwaka 1994 walipotwaa mara ya mwisho baada ya kuifunga Zambia mabao 2-1 katika
mchezo wa fainali.
REKODI
Nigeria:
Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi anakuwa kocha wa pili kama mchezaji kutwaa taji na pia kama kocha katika historia ya michuano hiyo, akiungana na Mahmoud Al Gohari wa Misri.
Nigeria:
Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi anakuwa kocha wa pili kama mchezaji kutwaa taji na pia kama kocha katika historia ya michuano hiyo, akiungana na Mahmoud Al Gohari wa Misri.
Nigeria ina rekodi ya pekee ya kiwango cha ubora wa soka duniani
(Fifa), kwani ndiyo timu pekee Afrika iliyowahi kushika nafasi ya tano duniani
mwaka 1994. Kwa sasa inashika nafasi ya 52.Kwa mara ya kwanza Nigeria ilicheza
fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994, ikiwa kundi moja na Bulgaria, Ugiriki na
Argentina na kufanikiwa kuongoza kundi lake.
Iliifunga Bulgaria 3ñ0, ikapoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na
Argentina na kufanikiwa kusonga mbele raundi ya pili baada ya kuifunga Ugiriki
mabao 2ñ0.
Katika raundi ya pili, Nigeria ilicheza na Italia, ambapo mpaka
dakika 25 za kwanza tayari walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na
Emmanuel Amunike.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment