Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Moh Edward Lowassa amesema kuwa
iwaposerikali zote mbili ile Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na ya
visiwani, zitatekeleza kwa usahihi maelekezo ya mkutano mkuu wa CCM juu
ya suala la ajira basi chama hicho kitashinda kiurahisi katika uchaguzi
mkuu wa 2015.
Akizungumza
katika mahojiano na Radio Uhuru jijini Dar es Salaam, jana juu ya
uchaguzi wa Kenya Mh Lowassa amesema amefurahishwa kuwa suala la tatizo
la ajira kwa vijana limekuwa ni moja ya ajenda muhimu katika uchaguzi
huo wa wiki ijayo.
`Nimefurahi
kuwa wenzetu wameliona hili kuwa ni tatizo kubwa nan i ajenda muhimu
katika uchaguzi wao.Nimefurahi Waziri Mkuu Odinga alielezea jinsi
serikali yao ilivyojaribu kulishughulikia suala hili’’ alisema Lowassa
na kuongeza kuwa ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashahriki kutambua rasmi
juu ya tatizo hilo.
Amesema
kuwa chama chake cha CCM kimepiga hatua kubwa ya kukiri kuwepo kwa
tatizo hilo la ajira kwa vijana, na kimetoa maelekezo kwa serikali zote
mbili kulishughulikia.
``Moja ya
maazimio ya mkutano mkuu wa CCM ni juu ya suala la ajira na katika kika
cha halmashauri kuu hivi karibuni, tulilijadili kwa kina tatizo hili, na
kwakweli kama serikali zetu hizi zitatekeleza maelekezo yake, sina
shaka yoyote CCM tutashinda kiurahisi 2015’’ alisema .
Mh
Lowassa ambaye amekuwa msemaji mkuu wa suala la ajira kwa vijana
akiliita ni bomu linalosubiri kulipuka, aliongeza kuwa , maamuzi ya
vikao hivyo yakitekelezwa vizuri vitaifanya CCM iingie kwenye uchaguzi
mkuu ikiwanamajibu sahihi yaliyokwishajibiwa juu ya tatizo la ajira kwa
vijana.
`CCM
imeanza kulishughulikia ili tusiulizwe na vijana 2015, tuangalie
uchaguzi wa Kenya hii ni moja ya ajenda muhimu katika
kujinadi’’alitanabaisha.
Amesema
kuwa kilimo ni moja ya eneo ambalo linaweza kwa kiasi kikubwa kutatua
tatizo hilo.’’pamoja na kwamba bado naamini kuwa elimu kabla kilimo
kwanza, lakini sekta hii nakubaliana kabisa kuwa inaweza kusaidia
kukabiliana na tatizo hili’’ alisema .
Aidha
amesema kuwa viwanda vikubwa vya nguo ni eneo jingine ambalo linaweza
kwa kiasi kikubwa kusaidia upatikanaji wa jira kwa vijana.`` Mkutano
mkuu ulizielekeza serikali zetu kujikita katika uanzishwaji wa viwanda
vya nguo,hapa tunaweza kukopa kutokana na rasilimali ya gesi tuliyonayo
ili kujenga viwanda vya nguo katika maeneo yanayolimwa pamba’’alishauri
na kutolea mfano wan chi ya Ghana ambayo baada ya kubaini kuwa na
nishati ya mafuta iliamua kukopa kabla ya kuanza kuyachimba na fedha
hizo zikasaidia katika sekta nyingine za kimaendeleo.
`Hii
inawezekana kabisa, viwanda vya nguo ndiyo vyenye kutoa ajira
kubwa,tusingoje mpaka vijana waje kutuuliza 2015’’ alionya Lowassa
ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa watu wanaotaka kuwania urais katika
uchaguzi mkuu ujayo.
Kauli
hiyo ya Lowassa imekuja siku moja tu baada ya Shirika la utafiti la
Synovate kutoa matokeo ya uchaguzi wake yanaoonesha kuwa chama tawala
CCM kimeongezeka umaarufu ambapo asilimia 52 ya wananchi waliyohojiwa
wamesema kuwa wangependa kujiunga nacho.Ama kwa upande wake Mh Lowassa
kwa mujibu wa utafiti huo umaarufu wake kuelekea 2015 umepanda kwa
asilimia sita na kufikia asilimia 7 akiwa miongoni mwa vigogo watano wa
juu wanaopewa nafasi ya kushinda urais iwapo uchaguzi ungefanyika leo.
Lowassa
kwa mujibu wa utaifi huo anataguliwa na Waziri wa Ujenzi John Pombe
Magufuli mwenye asilimia 8, Zitto Kabwe wa Chadema na Waziri Mkuu
Mizengo Pinda wenye asilimia 9 na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad
Slah mwenye asilimia 17 akiporomoka kutoka asilimia 42 aliyokuwa nayo
miaka miwili iliyopita
source: Mjengwa Blog
No comments:
Post a Comment