WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, February 26, 2013

Rage: Sijiuzulu Simba ng'o!

 
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage amesema hawezi kujiuzulu nafasi yake kutokana na matokeo yao yasiyoridhisha katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na pia kufungwa katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwavile yeye si miongoni mwa maafisa wa benchi la ufundi.
Baadhi ya vyombo vya habari vilidai jana kuwa Rage amejiuzulu cheo chake kutokana na matokeo mabaya ya timu yake.

Hata hivyo, akizungumza katika mahojiano na kituo cha redio jijini Dar es Salaam jana, Rage alisema kuwa hawezi kuachia ngazi kwani hahusiki kwa lolote na mwenendo wao wa kusuasua.

Alifafanua zaidi kuwa walau wachezaji na watu wa benchi la ufundi ndiwo wanaopaswa kuulizwa juu ya kufanya kwao vibaya na kwamba, kamati yake ya utendaji imepanga kukutana na benchi la ufundi ili kujua tatizo liko wapi. 

“Siwezi kujiuzulu kwa sababu mimi sichezi uwanjani na wala sifundishi timu. Mbona klabu nyingi na hata zile za Ulaya zinafungwa lakini viongozi hawajiuzulu,” alisema Rage.
“Kama ni suala la kuwajibika, wawajibike makocha na wachezaji...sisi kama viongozi hatuhusiki na matokeo ambayo Simba imekuwa ikiyapata,” aliongeza.

Kumekuwa kukiibuka makundi ya mashabiki wa Simba wanaotaka mwenyekiti huyo aachie ngazi, wakimtuhumu kuwa sehemu ya vikwazo vinavyoikabili klabu yao msimu huu.

Simba ilianza kwa kusuasua katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Bara kwa kushikiliwa sare mbili na kufungwa moja juzi dhidi ya Mtibwa huku pia ikichapwa kwa idadi hiyo ya mabao katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo.

Katika mechi ya juzi waliyolala nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mashabiki walionekana kukerwa kiasi cha kulifanya jeshi la polisi kuwatawanya kwa maji ya kuwasha.

Mabingwa hao wana kibarua kizito cha kutetea ubingwa wao msimu huu kwani hadi sasa ingali ikihaha katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 31, nane nyuma ya vinara wa ligi hiyo, mahasimu wao wa jadi Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi. Simba pia imeachwa kwa pointi tano na Azam wanaokamata nafasi ya pili.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment