WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, February 17, 2013

PADRE EVARIST MUSHI WA KANISA LA MTONI ZANZIBAR AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


mushi 
Hali si shwari nchini baada ya Padri Mushi ambaye alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Minara Miwili – Zanzibar kuuwawa kinyama kwa kupigwa risasi .

Padri huyo ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mida ya saa moja asubuhi akielekea kanisani

Taarifa zilizopatikana sasa hivi ni kuwa Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi saa 1.00 asubuhi na kufariki kabla hajafika hospitali ya Mnazi Mmoja. Paroko huyu amepigwa risasi akishuka katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00 leo.

Padri Evarist Mushi amepigwa risasi kichwani na kufa papohapo na watu wasiojulikana akiwa njiani anaenda kuendesha misa katika Kanisa la Mt.Theresia eneo la Mtoni Zanzibar.

Msemaji wa Polisi Zanzibar, Inspekta Mohamed Mhina amethibitisha tokeo hilo.

wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki  mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.
Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu.

source: Francis Godwin and   lakwangule blog                                              

2 comments:

  1. Zanzibar hii, kwa wakristo ni ngumu kupata mtetezi, maana yamkini hata hao viongozi wa juu pia wanafurahia kifo cha padre Mushi, msidanganywe wanaposema eti jeshi la polisi linafanya uchunguzi, uchunguzi gani? kesi ya mbwa ukampelekee mbweha? mliona wapi? lakini iko siku moja tu HUKUMU ya kweli itapita. Nyie tunyanyaseni tuchinjeni sote lakini siku yako nawe yaja, utalia na kusaga meno. Inauma unapokutana mtoto mdogo njiani akisema " nimefurahi sana bora alivyokufa haswa" kama sio kasumba ya udini ni nini? wanafundishwa nini na wazee wao? WANAFUNDISHWA KUWA NA CHUKI DHIDI YA WAKRISTO. LAKINI WATAMBUE YA KUWA SIO KAMA WAKRISTO HATUWEZI KUFANYA FUJO AU KUFANYA KAMA WANAVYOFANYA WAO, ILA SISI TUNA AMANI NDANI YA MIOYO YETU, ILE AMANI AMBAYO KRISTO ALITUACHIA, NA TUNA ROHO ZA KI-UTU. HATUNA KISASI MAANA TWAJUA KISASI NI CHA BWANA MUNGU MWENYEWE. ILA ANGALIENI BADO KITAMBO TU MTAIPATA FRESH.

    ReplyDelete
  2. Kama mnapata hayo mafundisho machafu kuwa kuuwa ndo mtakwenda peponi, basi mnajidanganya
    bali mjue kuwa laana iko nyuma yenu.mtalaaniwa hata vizazi vyenu vyote, mna roho za kishetani bora
    ndugu zetu waishi na wanyama kuliko binadamu wa aina hiyo. poleni wote na RIP Fr Mushi.







    ReplyDelete