WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere

Thursday, February 28, 2013

Neno La Leo: " Inuka Twende Ni Kwa Walioagana!"

Photo: Neno La Leo: " Inuka Twende Ni Kwa Walioagana!"
Ndugu zangu,
Hakuna wawili watembeao pamoja pasi na maelewano. 
Ukiwaona wanadamu wawili wanatembea pamoja, basi, wana makubaliano. Ni watu waliopatana.
Kwenye kundi la watu wa mataifa tofauti ukimsikia Mtanzania anamtamkia Mtanzania mwenzake, tena kwa Kiswahili; " E bwana inuka twende zetu!", na Mtanzania huyo mwingine akabaki amekaa bila kushtuka, basi, utilie mashaka UTanzania wake.
Ndio, " Inuka twende ni kwa waliogana". Ni watu wenye kufahamiana. Ni ndugu.
Nimeanza kuingiwa na hofu kuwa Watanzania tumeanza kupoteana kama ndugu. " Inuka twende' yetu imeanza kuangaliwa kwa sura ya udini, ukabila na itikadi. 
Hatujafika pabaya sana, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tumeshaziona ishara. Miongoni mwetu Watanzania tumeanza kuzisikia kaauli za ; " Umewasikia jamaa zetu Wakrito? Umewasikia jamaa zetu Waislamu? Umewasikia jamaa zetu WaZanzibar? Umewasikia jamaa zetu wa Bara?......"
Hizi ni ishara za undugu unaosambaratika. Zamani sisi sote tulikuwa ni ndugu. Tulitembea pamoja, ishara ya watu tuliopatana.
Leo kuna Watanzania wanaoambiwa; " E bwana wee, siku hizi nakuona unatembea na kuongea na wale jamaa zetu wa upande mwingine!"
Ndio, Watanzania tumeacha kuwa ndugu. Tunagawanyika kwenye mapande. Ni kwa kuzitazama tofauti za dini, kabila na itikadi. 
Hatujafikia pabaya, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tukumbuke; " Inuka twende ni kwa waliogana".  Watanzania tulishaagana. Tulishakubaliana. Tulijua tunakokwenda kama Taifa. Kama ndugu. Tumeanza sasa kusambaratika. 
Tuinuke sasa twende kupambana na yote yenye kutugawa kama ndugu wa taifa moja. Tuna kila sababu, nia na uwezo wa kushinda mapambano haya dhidi ya ubaguzi wa aina zote.
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
<a href=

http://mjengwablog.co.tz/

No comments:

Post a Comment