WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, February 28, 2013

neno la leo;elimu

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu: Elimu
Ndugu zangu,
Napenda usiku huu nitaje matatu tu miongoni mwa ninayoamini kuwa ni malengo ya nchi kwenye elimu ;
- Kuimarisha Umoja wa Kitaifa na kupunguza pengo la walio na wasio nacho.
-Kuwaendeleza walioelimika kuwa raia wema.
-Kuendeleza uchumi wa nchi.
Na elimu ni nini hasa? 
Jibu; ni shughuli yenye maana na tija kwa anayeifanya. Ni sharti iwe na dhumuni na malengo. 
Ndio, ni shughuli muhimu sana kwa mwananamu na nchi. Na kwa nchi,   ni shughuli yenye gharama.
Na hakuna nchi yeyote duniani iliyopiga hatua za maana kwenye kinachoitwa maendeleo bila kuwekeza kwa wingi kwenye elimu. Hivyo, elimu ndicho kitu cha kwanza.
Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
<a href=
Ndugu zangu,
Napenda usiku huu nitaje matatu tu miongoni mwa ninayoamini kuwa ni malengo ya nchi kwenye elimu ;
- Kuimarisha Umoja wa Kitaifa na kupunguza pengo la walio na wasio nacho.
-Kuwaendeleza walioelimika kuwa raia wema.
-Kuendeleza uchumi wa nchi.

Na elimu ni nini hasa?
Jibu; ni shughuli yenye maana na tija kwa anayeifanya. Ni sharti iwe na dhumuni na malengo.

Ndio, ni shughuli muhimu sana kwa mwananamu na nchi. Na kwa nchi, ni shughuli yenye gharama.

Na hakuna nchi yeyote duniani iliyopiga hatua za maana kwenye kinachoitwa maendeleo bila kuwekeza kwa wingi kwenye elimu. Hivyo, elimu ndicho kitu cha kwanza.

Na hilo ni Neno la Leo
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz/

Yanga mwendo mdundo

Mganyizi Martin (kulia) wa Kagera Sugar, akimtoka mlinzi wa Yanga , Nadir Haroub 'Cannavaro' wakati wa mechi yao ya ligi kuu ya Tanzania Bara kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Haruna Niyonzima 'Fabregas' aliibeba Yanga kwa mara nyingine baada ya kufunga goli 'kali' lililowapa ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
 
Matokeo hayo yaliwaweka 'Wanajangwani' katika nafasi nzuri ya kuelekea ubingwa baada ya kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi sita dhidi ya Azam wanaowafuatia katika nafasi ya pili.
 
Yanga wamefikisha pointi 42 baada ya kuteremka dimbani mara 18, wakifuatiwa na Azam waliocheza idadi hiyo pia ya mechi. Mabingwa watetezi, Simba, ambao walipata kipigo kisichotarajiwa cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Jumapili, wanaendelea kusuasua katika nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 34. 
 
Niyonzima ambaye ndiye aliyefunga goli pekee pia lililowapa Yanga ushindi wa 1-0 wakati walipocheza dhidi ya Azam Jumamosi, alifanya juhudi binafsi kwa kuwatoka mabeki kadhaa wa Kagera na kutishia kutoa pasi kabla ya kugeuka na kupiga shuti lililomshinda kipa  Hannington na kujaa wavuni katika dakika ya 66.   
 
Goli hilo liliibua shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao tayari walishaanza kuingiwa na hofu kutokana na kiwango cha cha juu cha wapinzani wao kilichowapa 'jeuri' kutawala mechi hiyo katika kipindi cha pili.
 
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Burundi, Didier Kavumbagu aliikosesha Yanga kupata goli la utangulizi kwa njia ya penati katika dakika ya 45 baada ya shuti lake kupaa juu ya lango. 
 
Refa Simon Mberwa aliamuru ipigwe penati hiyo baada ya kipa wa Kagera, Hannington kudaka mguu wa Kavumbagu wakati akijaribu kuokoa na kipa huyo alionyeshwa kadi ya njano kwa kosa la kujaribu kupinga adhabu hiyo na kutishia kutoka uwanjani kabla ya kurejeshwa na kocha wake Abdallah Kibaden.
 
Katika dakika ya 49, Frank Domayo alipiga shuti kali lililompita kipa wa Kagera na kugonga mwamba kabla ya mpira kurejea uwanjani. 
 
Kagera walionyesha soka safi na kulishambulia zaidi lango la Yanga katika kipindi cha pili lakini wenyeji walisimama imara na kuokoa hatari kadhaa.  
 
Said Bahanunzi alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumvuta jezi George Kavilla wa Kagera katika eneo la kati ya uwanja na Nadir  
 
Haroub 'Cannavaro' alionyeshwa pia kadi ya njano katika dakika ya 82 baada ya kumkwatua Paul Ngwai aliyekuwa anaelekea kufunga. 
 
Wachezaji Nizar Khalfan na David Luhende wa Yanga walifanya jumla ya kadi zote za njano kwa klabu yao jana kufikia tano wakati walipoadhibiwa wakiwa nje ya uwanja kwa kosa lililoonekana kuwa ni kugomea maelekezo waliyopewa na refa wa mezani. Kadi hizo zilimaanisha kuwa 'Wanajngwani' wajiandae kutozwa faini ya Sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ya Bara kuhusiana na adhabu kwa timu inayopata kadi za idadi hiyo katika mechi moja. 
 
Baada ya mechi kumalizika, mashabiki wa Yanga waliojawa na furaha waliliendea basi liliolowabeba wachezaji wao na kuimba huku wakiwapongeza kwa kuwataja majina na kushangilia kwa kupuliza 'vuvuzela'. 
 
Akizungumza jana, kocha wa Yanga, Mholanzi Ernst Brandts alisema amefurahi timu yake kushinda kwani walicheza dhidi ya timu ngumu iliyowafunga 1-0 katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa wachezaji wake walikuwa wamechoka baada ya kucheza mechi nyingine ngumu pia dhidi ya klabu ya Azam Jumamosi.
 
"Kiasi hatukucheza katika kiwango chetu kwa sababu wachezaji walichoshwa na mechi iliyopita (dhidi ya Azam) iliyokuwa ngumu na ushindani mkali," alisema Brandts.
 
Kocha wa Kagera, Abdallah Kibaden, aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri licha ya kuchoshwa na urefu wa safari ya kutoka kwao Bukoba.
 
Katika mechi nyingine za ligi hiyo jana, Ruvu Shooting waliwashikilia wenyeji Coastal Union kwa sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku bao pekee lililofungwa na Nahoda Bakari katika dakika ya 51 likiwapa Polisi Morogoro ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Jamhuri na Mtibwa walishindwa kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.
 
Vikosi: 
Yanga:- Mustafa Barthez,Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Athumani Iddi 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu/Hamis Kiiza (dk.60), Said Bahanunzi/Jerry Tegete (dk.68), Haruna Niyonzima.
 
Kagera:-Hannington Kalyesubula, Benjamin Asukile, Muganyizi Martin, Malgesi Mwangwa, Amandus Nesta, George Kavilla, Julius Mrope/Paul Ngwai (dk.62), Juma Nade, Darlington Enyinna, Shija Mkina, Daud Jumanne. 
CHANZO: NIPASHE

Papa: Ilikuwa dhoruba

 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Benedict XVI
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Benedict XVI, alijitokeza jana kwa mara ya mwisho mbele ya maelfu ya waumini wake katika viwanja vya Mtakatifu Petro na kuzungumzia uongozi wake huku akieleza kwamba ulikuwa na nyakati za dhoruba na furaha.
Papa Benedict XVI aliwahutubia maelfu ya Wakatoliki katika mkesha wa kihistoria wa kujiuzulu kwake kama kiongozi wa Wakatoliki bilioni 1.2 kote ulimwenguni.

Mbele ya umati wa watu Papa Benedict XVI alizungumzia nyakati za mapambano na pia za furaha wakati wa hotuba yake ya mwisho kwa umma katika viwanja vya Mtakatifu Petro.
Katika ujumbe wake binafsi usiyo wa kawaida, alisema kuwa kumekuwa na “siku nyingi za nuru” lakini pia “nyakati za dhoruba kali”.

“Hata kama kanisa likipita kwenye bahari yenye dhoruba kali kiasi gani, Mungu hawezi kuliacha lizame,” alisema Papa ambaye anajiuzulu rasmi leo na kutoa nafasi kwa makardinali wa kanisa hilo kuanza mchakato wa kumpata mrithi wake.

Maneno hayo yametafsiriwa na wengi kama maoni yake juu ya kashfa ya unajisi wa watoto na madai ya rushwa ambayo yaliibuka wakati wa uongozi wake.

“Ilikuwa ni sehemu ya safari ya kanisa kwamba limekuwa na nyakati za furaha na nuru, lakini pia wakati ambao haukuwa rahisi,” alisema.

Papa aliwashukuru makardinali, makasisi katika Roma, maofisa wa Vatican na mapadre duniani kote kwa kazi zao, pamoja na sharika zao na kueleza kuwa alichukua uamuzi wa kustaafu ‘kwa amani ya ndani ya akili yake’.

“Kupenda kanisa pia ina maana ya kuwa na ujasiri wa kufanya uamuzi mgumu,” alisema na kuomba waumini hao wasali kwa ajili yake na Papa mpya.

Alisema maisha yake baada ya kustaafu yatarudi mahali binafsi na kusema: “Siyo maisha ya kusafiri, kuhudhuria mikutano na makongamano wala kufuta cheo cha Papa.”
Mahujaji walianza kukusanyika katika viwanja hivyo mjini Vatican mapema jana, ili kumuaga Papa mwenye umri wa miaka 85 ambaye alitangaza nia ya kujiuzulu Februari 12, mwaka huu kwa kusema kuwa alikuwa mdhaifu sana kuendelea na uongozi wake katika ulimwengu wa sasa.

Makao makuu ya kanisa Katoliki yamesema takribani watu 50,000 wamenunua tiketi za kuhudhuria hafla hiyo, lakini wengine wengi huenda wakajitokeza na hivyo maofisa wamejiandaa kuwakaribisha watu 200,000.

Vifaa vya ukaguzi vimewekwa katika eneo hilo, pamoja na walenga shabaha na kuweka maeneo ya kliniki.

Hafla hiyo ilianza kwa Papa kuzuru mji wa Vatican akiwa ndani ya gari maalum nyeupe, na kutoa hotuba yake ya mwisho kwa waumini wake wa jimbo la Roma na ulimwengu mzima.
Makardinali kutoka kote ulimwenguni wataanzisha mikutano kujadili kuhusu masuala muhimu ya kanisa Katoliki, kuweka tarehe ya mkutano wa kumchagua Papa mpya na kutathmini orodha ya wagombea wanaoweza kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI.

Mapema mwezi huu Papa alipotangaza kustaafu, alisema atajishughulisha zaidi na sala.
Misa yake ya mwisho ya jana ilihudhuriwa na zaidi ya waumini 150,000 kutoka kila pembe ya dunia.

Wakazi wa jimbo la Kusini mwa Ujerumani Bavaria anakotokea kiongozi huyo wa kanisa Katoliki ulimwenguni walihudhuria kwa wingi kumuaga jamaa yao. Katika misa yake hiyo ya mwisho ya hadhara kama kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni, Papa Benedict XVI akiwa ndani ya gari maalum la Vatican aliusalimia umati wa waumini uliojitokeza katika viwanja vya Mtakatifu Petro muda mrefu zaidi kuliko kawaida yake kabla ya kuwakaribisha kwa mazungumzo baadhi ya viongozi ikiwa ni pamoja na Rais Ivan Gasparovic wa Jamhuri ya Slovakia.

Miongoni mwa waumini hao kuna wale wanaotokea katika jimbo la Kusini la Bavaria, wakibeba bendera za jimbo hilo na kupiga muziki wa Bavaria ambao mwenyewe Joseph Ratzinger (Papa) anapenda kuusikia ukichezwa.

Siku kadhaa zilizopita, umati wa waumini kutoka Ujerumani wamekuwa wakimiminika mjini Roma. Wenyewe wanasema hata akiacha wadhifa huo ataendelea kuwa muhimu kwao.
Tobias Eichinger, aliyekwenda Roma pamoja na mchumba wake Cornelia alisema:
“Tunataka kumuombea Papa mtakatifu ambaye ni wa kutoka Bavaria na pia ni mwenzetu, kila la kheri.”

Mshika bendera wa kundi la waumini wa Bavaria, Helmut Jawurek, anahisi uamuzi wa Papa Benedict XVI kimsingi ni sawa. Anasema ataendelea kuwa mtiifu kwa kiongozi mwingine wa kanisa Katoliki ulimwenguni atakayechaguliwa na makardinali mwezi ujao.
“Kanisa Katoliki ni kanisa la dunia na uraia si muhimu, la muhimu zaidi ni imani,” alisema.

Baada ya uamuzi wa Papa Benedict XVI kutangaza nia ya  kujiuzulu, Kanisa Katoliki limejikuta katika hali ambayo halijawahi kuwamo kwa kipindi cha takribani miaka 700.
Ni washauri wachache tu walio karibu na Papa, ambao walijua mpango wake wa kujiuzulu kabla ya kutangazwa hadharani. Hata vigogo katika uongozi wa Vatican walishtushwa na uamuzi huo.

Kitendo cha kuamua kujiuzulu kwa Papa kumeibua maoni mbalimbali kwa Wakatoliki huku wengine wakieleza kwamba uamuzi wake ni wa kishujaa na utaleta nguvu mpya katika kanisa hilo na pengine kumaliza mtindo wa kuwachagua wakongwe kuliongoza kanisa hilo.

NI VIGUMU KUTABIRI MRITHI
Baada ya ibada ya jana ya Papa kuwaaga waumini wa kanisa hilo, mchakato wa kumtafuta mrithi wake utaanza kupitia utaratibu ule ule unaotumika pindi Papa anapofariki. Kwa sasa nafasi ijulikanayo kama kiti cha Petro itakuwa wazi na kanisa litakuwa na siku kati ya 15 na 20 kumchagua Papa mwingine.

Uvumi kuhusu nani anaweza kuchaguliwa kuwa Papa mpya ulianza mara tu baada ya Papa anayeondoka kutangaza uamuzi wake. Lakini, hata wale wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya Vatican wametoa tahadhari kwamba si rahisi kutabiri nani atachaguliwa.

Vatican imesema inatarajia kuwa Papa mpya atajulikana kabla ya siku kuu ya Pasaka, ambayo ni Machi 31, ingawa kila kitu kitategemea mkutano wa faragha wa makardinali.

Inakadiriwa kwamba takribani makardinali 115 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni watapigakura ya kumchagua mrithi wa Papa Benedict XVI.

Aidha, uongozi huo umesema kwamba atabakia na cheo chake cha Papa Benedict XVI na kwamba hatarejea kwenye jina lake la ubatizo la Joseph Ratzinger. Pete yake ambayo ni nembo ya wadhifa huo itaharibiwa mara tu atakapokabidhi ofisi.

Uongozi wake wa miaka minane aliyoushikilia wadhifa wa Papa ni moja ya vipindi vifupi katika historia ya wadhifa huo.  Hata hivyo, kipindi hicho kilitosha kumpatia Papa Benedict XVI maadui wengi, wakiwamo mashoga na wanaharakati wa kupambana na ugonjwa wa Ukimwi. Katika kipindi hicho pia kashfa nyingi za visa vya mapadre kuwanajisi watoto zilifichuliwa.
 
CHANZO: NIPASHE

Neno La Leo: " Inuka Twende Ni Kwa Walioagana!"

Photo: Neno La Leo: " Inuka Twende Ni Kwa Walioagana!"
Ndugu zangu,
Hakuna wawili watembeao pamoja pasi na maelewano. 
Ukiwaona wanadamu wawili wanatembea pamoja, basi, wana makubaliano. Ni watu waliopatana.
Kwenye kundi la watu wa mataifa tofauti ukimsikia Mtanzania anamtamkia Mtanzania mwenzake, tena kwa Kiswahili; " E bwana inuka twende zetu!", na Mtanzania huyo mwingine akabaki amekaa bila kushtuka, basi, utilie mashaka UTanzania wake.
Ndio, " Inuka twende ni kwa waliogana". Ni watu wenye kufahamiana. Ni ndugu.
Nimeanza kuingiwa na hofu kuwa Watanzania tumeanza kupoteana kama ndugu. " Inuka twende' yetu imeanza kuangaliwa kwa sura ya udini, ukabila na itikadi. 
Hatujafika pabaya sana, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tumeshaziona ishara. Miongoni mwetu Watanzania tumeanza kuzisikia kaauli za ; " Umewasikia jamaa zetu Wakrito? Umewasikia jamaa zetu Waislamu? Umewasikia jamaa zetu WaZanzibar? Umewasikia jamaa zetu wa Bara?......"
Hizi ni ishara za undugu unaosambaratika. Zamani sisi sote tulikuwa ni ndugu. Tulitembea pamoja, ishara ya watu tuliopatana.
Leo kuna Watanzania wanaoambiwa; " E bwana wee, siku hizi nakuona unatembea na kuongea na wale jamaa zetu wa upande mwingine!"
Ndio, Watanzania tumeacha kuwa ndugu. Tunagawanyika kwenye mapande. Ni kwa kuzitazama tofauti za dini, kabila na itikadi. 
Hatujafikia pabaya, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tukumbuke; " Inuka twende ni kwa waliogana".  Watanzania tulishaagana. Tulishakubaliana. Tulijua tunakokwenda kama Taifa. Kama ndugu. Tumeanza sasa kusambaratika. 
Tuinuke sasa twende kupambana na yote yenye kutugawa kama ndugu wa taifa moja. Tuna kila sababu, nia na uwezo wa kushinda mapambano haya dhidi ya ubaguzi wa aina zote.
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
<a href=
Ndugu zangu,

Hakuna wawili watembeao pamoja pasi na maelewano.
Ukiwaona wanadamu wawili wanatembea pamoja, basi, wana makubaliano. Ni watu waliopatana.

Kwenye kundi la watu wa mataifa tofauti ukimsikia Mtanzania anamtamkia Mtanzania mwenzake, tena kwa Kiswahili; " E bwana inuka twende zetu!", na Mtanzania huyo mwingine akabaki amekaa bila kushtuka, basi, utilie mashaka UTanzania wake.


Ndio, " Inuka twende ni kwa waliogana". Ni watu wenye kufahamiana. Ni ndugu.

Nimeanza kuingiwa na hofu kuwa Watanzania tumeanza kupoteana kama ndugu. " Inuka twende' yetu imeanza kuangaliwa kwa sura ya udini, ukabila na itikadi.

Hatujafika pabaya sana, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tumeshaziona ishara. Miongoni mwetu Watanzania tumeanza kuzisikia kaauli za ; " Umewasikia jamaa zetu Wakrito? Umewasikia jamaa zetu Waislamu? Umewasikia jamaa zetu WaZanzibar? Umewasikia jamaa zetu wa Bara?......"

Hizi ni ishara za undugu unaosambaratika. Zamani sisi sote tulikuwa ni ndugu. Tulitembea pamoja, ishara ya watu tuliopatana.

Leo kuna Watanzania wanaoambiwa; " E bwana wee, siku hizi nakuona unatembea na kuongea na wale jamaa zetu wa upande mwingine!"

Ndio, Watanzania tumeacha kuwa ndugu. Tunagawanyika kwenye mapande. Ni kwa kuzitazama tofauti za dini, kabila na itikadi.

Hatujafikia pabaya, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tukumbuke; " Inuka twende ni kwa waliogana". Watanzania tulishaagana. Tulishakubaliana. Tulijua tunakokwenda kama Taifa. Kama ndugu. Tumeanza sasa kusambaratika.

Tuinuke sasa twende kupambana na yote yenye kutugawa kama ndugu wa taifa moja. Tuna kila sababu, nia na uwezo wa kushinda mapambano haya dhidi ya ubaguzi wa aina zote.


Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz/

Tuesday, February 26, 2013

Rage: Sijiuzulu Simba ng'o!

 
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage amesema hawezi kujiuzulu nafasi yake kutokana na matokeo yao yasiyoridhisha katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na pia kufungwa katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwavile yeye si miongoni mwa maafisa wa benchi la ufundi.
Baadhi ya vyombo vya habari vilidai jana kuwa Rage amejiuzulu cheo chake kutokana na matokeo mabaya ya timu yake.

Hata hivyo, akizungumza katika mahojiano na kituo cha redio jijini Dar es Salaam jana, Rage alisema kuwa hawezi kuachia ngazi kwani hahusiki kwa lolote na mwenendo wao wa kusuasua.

Alifafanua zaidi kuwa walau wachezaji na watu wa benchi la ufundi ndiwo wanaopaswa kuulizwa juu ya kufanya kwao vibaya na kwamba, kamati yake ya utendaji imepanga kukutana na benchi la ufundi ili kujua tatizo liko wapi. 

“Siwezi kujiuzulu kwa sababu mimi sichezi uwanjani na wala sifundishi timu. Mbona klabu nyingi na hata zile za Ulaya zinafungwa lakini viongozi hawajiuzulu,” alisema Rage.
“Kama ni suala la kuwajibika, wawajibike makocha na wachezaji...sisi kama viongozi hatuhusiki na matokeo ambayo Simba imekuwa ikiyapata,” aliongeza.

Kumekuwa kukiibuka makundi ya mashabiki wa Simba wanaotaka mwenyekiti huyo aachie ngazi, wakimtuhumu kuwa sehemu ya vikwazo vinavyoikabili klabu yao msimu huu.

Simba ilianza kwa kusuasua katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Bara kwa kushikiliwa sare mbili na kufungwa moja juzi dhidi ya Mtibwa huku pia ikichapwa kwa idadi hiyo ya mabao katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo.

Katika mechi ya juzi waliyolala nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mashabiki walionekana kukerwa kiasi cha kulifanya jeshi la polisi kuwatawanya kwa maji ya kuwasha.

Mabingwa hao wana kibarua kizito cha kutetea ubingwa wao msimu huu kwani hadi sasa ingali ikihaha katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 31, nane nyuma ya vinara wa ligi hiyo, mahasimu wao wa jadi Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi. Simba pia imeachwa kwa pointi tano na Azam wanaokamata nafasi ya pili.
 
CHANZO: NIPASHE

Sheikh Khalifa aitaka Serikali kudhibiti chuki


MWENYEKITI wa Taasisi ya Kiislamu ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis ameishauri  Serikali kuchukua hatua za haraka kulinusuru taifa ili lisiingie katika dimbwi la umwagaji damu kwa misingi ya chuki za kidini.

Hivi karibuni kulitokea matukio ya kuuawa kwa viongozi wa kidini mkoani Geita na visiwani Zanzibar ambapo Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki aliuawa baada ya kupigwa risasi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Sheikh Khamis alisema vitendo vya mauaji ya viongozi wa kidini, uchomaji wa nyumba za ibada na vurugu za maandamano ya kila siku ya Ijumaa vinaashiria kuwepo kwa kikundi cha watu wachache ambao wamechoka kuishi kwa amani.

“Hatuamini kama mauaji hayo yametekelezwa na waislamu kwa sababu Uislamu unahimiza amani na unapinga waziwazi vitendo vya kinyama kama hivyo,” alisema Sheikh Khamis.

Sheikh huyo alisema kuna baadhi ya vikundi ambavyo vimekuwa vikiwatumia vijana wasiojua kitu kwa masilahi yao binafsi na kwamba vikundi hivyo vinaitia fedheha na aibu jamii ya Kiislamu kwa kulitumia vibaya jina la Uislamu.

Alisema vikundi hivyo vimekuwa vikivamia baadhi ya misikiti na kuiteka huku wakiigeuza mingine kuwa vituo vya kujifunzia kareti na kufanyia mikutano na hotuba za kuwahamasisha waislamu kufanya vurugu.
Alisema hakuna mahala ambapo Uislamu unafundisha kujichukulia sheria mikononi, kupuuza au kutokuheshimu mamlaka ya dola na vyombo vya sheria.

Alisema kitendo cha baadhi ya waumini wa dini hiyo kujitumbukiza katika maandamano ya kuishinikiza Serikali, mahakama na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) ili kumwachia kwa dhamana Sheikh Ponda na wenzake ni kinyume na taratibu za kisheria zilizowekwa katika kumpatia mtuhumiwa dhamana.

Mwenyekiti huyo aliwaasa waislamu wote Tanzania kuendelea kuilinda amani na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kufanikiwa kuwakamata wauaji na  wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
 

Pia aliishauri Serikali iache kufumbia macho matendo maovu na ya kuvunja sheria badala yake itumie uwezo na dhamira yake ili kudumisha amani iliyoko nchini.

source Mwananchi

Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015



WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.


Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.

Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti uliotangulia.
 
Wengine wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7) na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (5).

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).
Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.
Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.

Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.
CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.

Uwezekano mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka jana kilikuwa na uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na kuibua vuguvugu kubwa masikioni mwa wananchi.

Chadema hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya Movement For Change (M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama uchaguzi wa CCM.
Chama kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka 2011 hadi nne mwaka 2012.

Hata hivyo, asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama chochote imepanda kutoka asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.
Rushwa
 
Katika suala la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu 10 waliohojiwa, wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia asilimia 41, asilimia 30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema imepungua na asilimia tano hawajui.
 
Gazeti Mwananchi

LOWASSA: CCM ITASHINDA 2015

  
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Moh Edward Lowassa amesema kuwa iwaposerikali zote mbili ile Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na ya visiwani, zitatekeleza  kwa usahihi maelekezo ya mkutano mkuu wa CCM juu ya suala la ajira basi chama hicho kitashinda kiurahisi katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Akizungumza katika mahojiano na Radio Uhuru jijini Dar es Salaam, jana juu ya uchaguzi wa Kenya Mh Lowassa  amesema amefurahishwa kuwa suala la tatizo la ajira kwa vijana limekuwa ni moja ya ajenda muhimu katika uchaguzi huo wa wiki ijayo.

`Nimefurahi kuwa wenzetu wameliona hili kuwa ni tatizo kubwa nan i ajenda muhimu katika uchaguzi wao.Nimefurahi Waziri Mkuu Odinga alielezea jinsi serikali yao ilivyojaribu kulishughulikia suala hili’’ alisema Lowassa na kuongeza kuwa  ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashahriki kutambua rasmi juu ya tatizo hilo.

 Amesema kuwa chama chake cha CCM kimepiga hatua kubwa ya kukiri kuwepo kwa tatizo hilo la ajira kwa vijana, na kimetoa maelekezo kwa serikali zote mbili kulishughulikia.

``Moja ya maazimio ya mkutano mkuu wa CCM ni juu ya suala la ajira na katika kika cha halmashauri kuu hivi karibuni, tulilijadili kwa kina tatizo hili, na kwakweli kama serikali zetu hizi zitatekeleza maelekezo yake, sina shaka yoyote CCM tutashinda kiurahisi 2015’’ alisema .

 Mh Lowassa ambaye amekuwa msemaji mkuu wa suala la ajira kwa vijana akiliita ni bomu linalosubiri kulipuka, aliongeza kuwa , maamuzi ya vikao hivyo yakitekelezwa vizuri vitaifanya CCM iingie kwenye uchaguzi mkuu ikiwanamajibu sahihi yaliyokwishajibiwa juu ya tatizo la ajira kwa vijana.

 `CCM imeanza kulishughulikia ili tusiulizwe na vijana 2015, tuangalie uchaguzi wa Kenya hii ni moja ya ajenda muhimu katika kujinadi’’alitanabaisha.

Amesema kuwa kilimo ni moja ya eneo ambalo linaweza kwa kiasi kikubwa kutatua tatizo hilo.’’pamoja na kwamba  bado naamini kuwa elimu kabla kilimo kwanza, lakini sekta hii nakubaliana kabisa kuwa inaweza kusaidia kukabiliana na tatizo hili’’ alisema .

 Aidha amesema kuwa  viwanda vikubwa vya nguo ni eneo jingine ambalo linaweza kwa kiasi kikubwa kusaidia upatikanaji wa jira kwa vijana.`` Mkutano mkuu ulizielekeza serikali zetu kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vya nguo,hapa tunaweza kukopa kutokana na rasilimali ya gesi tuliyonayo ili kujenga viwanda vya nguo katika maeneo yanayolimwa  pamba’’alishauri na kutolea mfano wan chi ya Ghana ambayo baada ya kubaini kuwa na nishati ya mafuta iliamua kukopa kabla ya kuanza kuyachimba na fedha hizo zikasaidia katika sekta nyingine za kimaendeleo.

`Hii inawezekana kabisa,  viwanda vya nguo ndiyo vyenye kutoa ajira kubwa,tusingoje mpaka vijana waje kutuuliza 2015’’ alionya Lowassa ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa watu wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujayo.

 Kauli hiyo ya Lowassa imekuja siku moja tu baada ya  Shirika la utafiti la Synovate kutoa matokeo ya uchaguzi wake yanaoonesha kuwa chama  tawala CCM kimeongezeka umaarufu ambapo asilimia 52 ya wananchi waliyohojiwa wamesema kuwa wangependa kujiunga nacho.Ama kwa upande wake Mh Lowassa kwa mujibu wa utafiti huo umaarufu wake kuelekea 2015 umepanda kwa asilimia sita  na kufikia asilimia 7 akiwa miongoni mwa vigogo watano wa juu wanaopewa nafasi ya kushinda urais iwapo uchaguzi ungefanyika leo.
 
Lowassa kwa mujibu wa utaifi huo anataguliwa na Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli mwenye asilimia 8, Zitto Kabwe wa Chadema na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wenye asilimia 9 na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slah mwenye asilimia 17 akiporomoka kutoka asilimia 42 aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita
 
source: Mjengwa Blog