- Kwa nini kadi hizo zisirudishwe kwa vyama husika katika matawi yao ili waweze kuhakiki wananchama wao?
- Vyama vya siasa vinahakiki vipi wanachama wake?
- Kwa nini mikutano mingi ya hadhara ya vyama vya siasa agenda kubwa ni kuwapokea wanachama wapya?
Nashindwa kuelewa pamoja na vyama vyetu vya siasa kumiliki wataalamu wa
uchambuzi wa mambo ya siasa na uchumi, bado wameshindwa kutumia taaluma yao hii
nyeti kuwashauri wenyeviti wa vyama vyao kuwa kuweka agenda ya kuwapokea na
wanachama wapya katika mikutano yao ya siasa ni matumizi mabaya ya muda na
ruzuku itokanayo na rasilimali ya Taifa letu. Muda huo ungeweza kutumika katika
kufafanua agenda mbalimbali zahusizo maendeleo ya wananchama wao au hata kuwapa elimu mbadala juu ya haki zao
ili waweze kujikwamua kutoka katika wimbi kubwa la umasikini.
Kama nilivyouliza hapo juu: Nafikiri ingekuwa ni busara kama kadi hizo
zingerudishwa na kutolewa katika matawi ya vyama vyao;lakini nafikiri huu ni
ufinyu wa uelewa wa demokrasia na kushindwa kuthubutu kwa viongozi wetu wa
vyama; na kubwa zaidi ni kutafuta umarufu wa kichama; je tunauhakika gani kama
wanachama hao sio wa chama hicho hicho? Je hao wanaorudisha hizo kadi sio
mamluki wa kisiasa; ambao kwa upeo na uelewa wa ukuaji wa demokrasis ndani ya
vyama vyetu viongozi wetu wanafikiri kuwa matukio kama haya yanawaongeza
wananchama kumbe nafikiri wanongeza kero ndani ya vyama vyao kwa kuwapata
wananchama wa msimu ambao wengi wao huishia kuwa mamluki wa kisiasa wanaohama
tuko chama kimoja kwenda kingine.
Na kubaliana na mwana zuoni ambaye aliwahi sema
kuwa “Inaelekea
nyie hamuwajui waTanzania walivyo hawana chama permanent, kesho wakisikia CUF
wako Jangwani watarudisha hizo kadi na kuingia CUF, keshokutwa ikirudi CDM
watarudisha za CUF na CCM na kuingia CDM, na CCM wakirudi tena kufanya mkutano
watarudisha hizo kadi na kuchukua za CCM Kwa kifupi siasa za Bongo ni sawa na
makampuni ya simu watu hununua simcard za makampuni mbali mbali kulingana na
msimu”
Vyama vya siasa Tanzania
hata chama kikongwe CCM wana tatizo la kutojua wana wanachama wangapi ambao ni
hai na ambao wanaweza kukisaidia chama katika kukiletea maendeleo na kukipigia
kura wakati wa uchaguzi, vyama vingi vinapumbazwa na halaiki ya watu wakati wa
mikutano yao ya wazi; hebu mkumbuke Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema mwaka
1995 alivyoweza kukusanya wafuasi wengi bali hawakuwa wananchama; na
alijihakikishia kuwa anashinda kutokana na umati wa watu kila alipokuwa
akihutubia mikutano; matokeo ya uchaguzi kwa njia ya kura yalipohitimishwa
hakuamini kabisa macho na kile alichokiona;
Vyama vijitahidi kuondoa
hii kasumba ili iwasaaidie wakati wa wa
uchaguzi ili waweze kuwa na uhakika walao wa aslimia 75% ya wanachama wao ambao
ni hai na watakupigia kura chama chao katika mazingira yeyote yale.
- Je kazi ya idara ya uenezi ya chama ni nini?
- Je idara hii kichama kwa jinsi vyama vyetu vinavyofanya kazi hivi sasa ina mapungufu gani?
Kwa tafsiri yangu, nafikiri
moja ya upungufu wa kada ya uenezi ya
chama husika ni kujikita zaidi katika kukizungumzia chama kwenye vyombo vya
habari na kusahau kazi yake ya msingi ya
kujenga uadilifu na maadili ya viongozi wake na wanachama wake; vyama vyetu
vinamwelekeo wa kukosa sifa ya siasa
safi na uongozi bora ndani ya chama husika. Siasa ni zaidi ya ushabiki wa
mpira; siasa safi zenye tija litawezesha taifa lolote lile kusonga mbele;
Kwa msingi huu vyama
vinatakiwa vianze kujiandaa katika kujiletea mapinduzi ya kifikra dhidi ya kujenga
fikra kwa wanachama wao na sio dhana ya kuhamasisha wanachama wao kuhama hama
kwa lengo la kutafuta umaarufu; Leo hii Taifa tumetawaliwa zaidi na ushabiki wa
kisiasa ambao kwa ujumla hamsaidii kabisa mwananchi wa taifa hili katika
kumwondoa katika umasikini unaomzunguka; viongozi wetu wajue kuwa sera za
kuwashawisha wananchama kuhama hama haisaidii kabisa kukifanya chama kuwa
imara. kuhamia chama kingine bila kuwa na dhamira hii ni upotoshaji na pengine
kusiwe ni kujijengea umaarufu kusikuwa na tija.
- Je viongozi ambao walikuwa na dhamana wanapohamia
- vyama vingine tunajifunza nini?
- Wanakuwa wamekosa nini?
- Je kuhamia chama kingine ni suluhisho?
Kwa jibu la haraka kwa
wahamiaji katika vyama vingine wenye dhama wanatukumbusha kuwa hakuna wanasiasa ni watu wanataka nafasi na kujineemesha
wenyewe. Kama ameshindwa kubadilisha maisha ya watu katika dhamana ambayo
alikuwa nayo kwenye chama chake cha zamani atawezaje kutumia nafasi hii katika
chama kipya? Kwa uchungu kabisa nasema kuwa Wanasiasa wanaendelea kutudanganya
na kwa ufinyu wa uelewa wetu wanatumia nafasi hii kufanikisha malengo yao.
Ushauri wangu viongozi
wetu wa vyama wangeweza kutumia muda huu wa kugawa kadi za kujiunga na chama
kwa kuwashauri wananchi na wanachama wao kuwapa elimu ya kuondoa umasikini; Kama
mwandishi mmoja alivyowahi sema kuwa “Watanzania wengi mna maisha magumu,
lakini sehemu ya ugumu huo wa maisha yenu umetokana na kasumba ya uvivu wa
kutofanya kazi kwa bidii
Nakumbuka sana maneno ya
Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere ili nchi iendelee inahitaji: watu, ardhi,
siasa safi na uongozi bora. Ni bahati mbaya kwamba wengi wa wanasiasa wetu wa
leo si bora na wala hawaendeshi siasa safi, na hali hii inatupeleka kubaya!
Ushindani wa siasa unapandikiza chuki ndani ya nchi, na kusababisha vurugu
ambazo hazina masilahi kwa wanyonge ili inawatengenezea njia wachache namna ya
kujiimarisha zaidi kimasilahi kwa siasa ambazo hazina Tija;
Wakati nu huu kwa wananchi kuanza kuwauliza viongozi wa vyama
wanakusaidiaje wewe mnyonge ambaye huna dawa, huna maji safi na salama, huna
barabara ambayo inaweza kupitika mwaka mzima, huna shule bora kwa ajili ya
watoto wetu, huna uhakika na maisha yako ya kesho; nafikiri lazima tukubali
kubadilisha ushabiki wa kisiasa ambao hauna tija kwa walalahoi:
No comments:
Post a Comment