Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Shughuli ya uchangiaji wa Mfuko wa watu wenye ulemavu Zanzibar huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort iliyopo nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mbali na Rais wa Zanzibar Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd nao wanatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi mbali mbali watakaoshiriki katika shughuli hiyo. Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Kamati inayoshughulikia shughuli hiyo imeeleza kuwa watu maarufu wapatao 300 wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu,Makamishna na Wakurugenzi pamoja na Wafanyabiashara wanatarajiwa kuhudhuria shughli hiyo ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake. Ratiba hiyo imeonesha kuwa mbali na kuchangia kutakuwepo na ngoma ya watu wenye ulemavu pamoja na mashairi na kuoneshwa Filamu inayohusu watu hao.
Aidha vitu mbalimbali vinatarajiwa kunadiwa katika shughuli hiyo ambapo washiriki wanatarajiwa kununua vitu hivyo lengo likiwa ni kutunisha mfuko huo wa Walemavu. Ratiba hiyo pia imeonesha kuwa kutakuwepo na uzinduzi wa Tovuti ya watu wenye ulemavu Zanzibar itakayoonesha mambo mbali mbali yanayowahusu yakiwemo uchangiaji wa watu hao.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 26/09/2012

No comments:
Post a Comment