WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, September 18, 2012

Neno La Leo: Unapotongozwa Na Usiyemdhania, Jitathmini...



Ndugu zangu,

Maishani wengi wetu tumetongozwa, iwe kwa mwanammke au mwanamme.

Juzi hapa nikiwa kwa Bi Mkora pale Msamvu,  akanilalamikia hili, kuwa siku hizi ameanza kutongozwa na hata ambao hakuwadhania.

Ama , makubwa hayo. Lakini, akaniomba nimpe tafsiri ya jambo hilo.Nikamjibu,  kuwa mwanadamu ukianza kuona unatongozwa na wale ambao hukuwadhania, basi, uanze kwanza kujitathmini, maana,  kuna mawili; 

Ama, ulivyo sasa na mwenenendo wako, ikiwamo staili yako ya maisha, na hata mavazi yako, yamewafanya wale ambao hukuwadhania , kuanza sasa kukutongoza, au, kwa mabadiliko hayo, wale ambao walikuwa wakikutongoza zamani wameacha sasa kukutongoza, na kuwa sasa unatongozwa na wapya wenye kuvutiwa na mabadiliko hayo yenye kukuhusu wewe.

Lililo jema kwa mwanadamu, ni  kwa wale waliokuwa wakikutongoza zamani kuendelea kukutongoza, na juu ya hapo, ukapata watongozaji wapya. Hivyo, personal transformation ( Mabadiliko binafsi) uliyoyapitia yatakuwa yamefanikiwa.

Na katika hili unaweza kuzama kifikra. Ukaangalia hata kwenye chama cha siasa. Kama chama cha siasa kitaanza kukimbiwa na wale waliokuwa wakikimbilia zamani, na kupata wakimbiliaji wapya, basi, hapo kuna tafsiri kama ya hapo juu. Nacho kitahitaji kujitathmini.

Wajumbe nakaribisha hoja zenu...

Maggid ( Mwenyekiti Wenu)

No comments:

Post a Comment