Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, amesema ipo haja ya Mwenge wa Uhuru
kurithiwa kizazi hadi kizazi kutokokana na falsafa safi aliyoileta raisi
wa kwanza wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius
Nyerere.
Alisema falsafa hiyo ilieleza kwamba Mwenge unawashwa ili ulete matumaini palipojaa dharau na chuki; na kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania
Dk. Sheni alitasema hayo alipokuwa akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi waliofika katika viwanja vya Chokocho katika sherehe za uwashaji wa mbio za mwenge wa uhuru.
Alisema Watanzania hawanabudi kuthamini mbio za Mwenge wa Uhuru kwani zimeleta heshima kubwa kwa Watanzania ndani na nje ya nchi na kwamba malengo na maudhui ya kuwashwa kwa Mwenge huo yana faida makubwa kwa Watanzania.
Alisema kuwa mbio hizo zina historia na umuhimu mkubwa kwani zimeanzishwa na wasisi wa Taifa yaani hayati Nyerere na hayati Abeid Amani Karume.
Alifafanua kuwa tokea kuwashwa kwa Mwenge huo miaka kadhaa iliopita Tanzania imekuwa ni nchi ya historia kuwa ni nchi ya amani barani Afrika, kwa vile Mwenge umeacha maeneo ya hekima ambayo yalitolewa na hayati Mwalimu Nyerere, wakati alipoanza kuuwasha Mwenge huo mwaka 1967.

CHANZO:
NIPASHE
uchambuzi wa ukadirifu kuhusu mwenge wa uhuru
Mwalimu
Julis Kambarage Nyerere falsafa yake kuhusu mwenge ilikuwa kama
ifuatavyo;, “Sisi Watanganyika, tunataka kuuwasha mwenge na kuuweka juu
ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale
ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa
dharau”.
Mwenge
huo uliwashwa Siku ya uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961, Baba wa Taifa
aliwasha Mwenge na baadaye ukapelekwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro
Je mwenge huu ulikuwa na maana gani kwa Taifa?
· kwa ufupi, ulikuwa ni
alama ya uhuru wetu kuona mapungufu yetu sisi wenyewe katika ujenzi wa
Taifa letu
· Falsafa
hiyo inalenga kuwaunganisha Watanzania, unatumika kukemea waovu, unatumiwa na
serikali kupitisha ujumbe na kuzindua miradi ya maendeleo inayoleta matumaini
kwa Watanzania
· mwenge
ulikutumika kuhimiza uzalendo, kuhimiza uwajibikaji, kueneza ujumbe juu ya
athari za rushwa, ukimwi, uzembe na kadhalika;
· Mwenge ni
ishara ya mshikamano wa udugu wa kitaifa
· Mwenge
ametumika kama chombo cha kuchochea maendeleo kupitia kauli mbio yake amabyo
imekuwa ikitolewa kila mwaka na tukizingatia kuwa mwenge unafika katika
kila kona ya nchi yetu.
JE MALENGO YA MWENGE WA UHURU YAMEONYESHA
MAFANIKIO?
· Mwenge
umekuwa ukitukumbusha kuhusu kuthamini uhuru wetu kama taifa ambalo tunatakiwa
kusimama imara kwa kuzingatia misingi ya imani upendo, amani na utulivu.
·
Mwenge pamoja na tofauti zetu za makabila, dini na vyama vya siasa sisi kama
Watanzania katika kipindi hiki cha zaidi ya miaka 50 bado tunahimizwa
kusimama kama Taifa moja na kuhakikisha kuwa Taifa letu haliyumbishwi na
watendaji wabovu, wazembe, wala Rushwa, Mafisadi na wanaoeneza chuki za
kuligawa Taifa kwa njia yeyote ile iwe ni Dini, Ukabila au Vyama vya siasa.
·
Katika kusherekea Mwenge wa Uhuru falfasa ya Mwenge inatakiwa ibaki imara ila
utekelezaji wake unatakiwa kubadilika kulingana na hali halisi ya vyama
vingi, upana wa demokrasia, na uzembe wa uwajibikaji;
·Sheria inatakiwa iendelee kufuatwa na wale wote wanaovunja sheria wachukuliwe hatua kali bila kujali nafasi zao kwa kufanya hivyo tutafanikiwa kurejea nuru yake ile ile tukapousimika tena tarehe 9 december 2011, kilele katika Mlima Kilimanjaro;
· Mwenge kwa sasa uwamulike
; wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo uwajibikaji ni
dhana ambayo kwa sasa kama Taifa tunaihitaji sana
· Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete sisi kama watanzania tutaendelea kukuhimiza wewe kama
Rais wa nchi pamoja na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuwapigania watanzania
katika kufikia nchi ahadi ambayo itakuwa na falfasa ya maisha Bora kwa kila mtu
yanawezekana kama serikali itafanikiwa kushinda vita dhidi ya mafisadi na
wahujumu wa maendeleo ya wananchi wa Tanzania kupitia kodi zetu;
·
Kodi zetu na Misaada kutoka kwa wafadhili itumike kwa masilahi ya Wananchi na
sio watu wachache ambao wanatumia nguvu kubwa katika kuhujumu;
SISI KAMA WATANZANIA TUNA
SABABU,
NIA,
NA UWEZO,
WA KUPAMBANA NA WAHUJUMU wa AMANI,
MAENDELEO NA UTULIVU AMBAO MWENGE WA UHURU UMEKUWA UKIENEZA KWA MIAKA HAMSINI (50) SASA;
TAZAMA RAMANI kweli TANZANIA ni NCHI NZURI lakini wajanya wachache wameanza kuhujumu amani na utulivu wetu kwa faida yao. Tunaendelea kuwaomba viongozi wetu msichukulie rahisi rahisi hii hali ya uvunjaji amani inayoendelea.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
No comments:
Post a Comment