Kitaifa
- DODOMA: Hotuba mbadala (ipo kwenye post inayofuatia hapo juu) iliyokuwa inasomwa na Waziri Kivuli wa Wizara ya Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi (Sugu), imesitishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda hadi ipitiwe na Kamati ya Bunge ili kuhariri kile alichokitamka kuwa ni "kauli za uchochezi", kadiri ilivyotolewa taarifa na Mbunge wa Mbozi, Godfrey Zambi kuwa ukurasa wa kwanza hadi wa kumi na nne una lugha hizo. Kikao cha Bunge kimesitishw hadi saa 11 jioni.
- TANGA: Jeshi la Polisi linawashikilia watu 15 wanaotuhumiwa kuchoma moto Kanisa la Bethania huko Donge, Tanga, Ijumaa iliyopita usiku. Kamanda Massawe amesema baada ya mahojiano na watuhumiwa, ndipo watalapoamua ikiwa walishiriki katika uhalifu huo ndipo wafikishwe mahakamani kwa mashitaka.
- MTWARA, Baraka Mfunguo: Siku ya Jumatano huduma zitasimama tena ili kusikiliza bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo huduma za mabasi yaendayo mikoani na Dar es Salaam nazo zitasimama. Kikubwa ni wananchi kutaka kujua mustakabali wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar na Msimamo wa Serikali ni upi.
- IRINGA: Jana katika kitimutimu cha askari polisi kuwatimua wamachinga, mtangazaji wa kituo cha Nuru FM Hussein Farahan alijikuta anashushwa kutoka kwenye pikipiki na kupigwa na askari huko Mshindo. Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda amesema kmbali ya mtangazaji huyo kukamatwa, pia wapo askari polisi waliokamatwa kutokana na kutofahamika na kuwa askari hao ni wanachuo ambao wapo mjini hapa kimasomo. Watu hao kwa sasa wameachiwa huru. Kamuhanda amesema kuwa waliokamatwa hadi saa 3 usiku walikuwa ni watu zaidi ya 100 na kuwa baadhi yao wameachiwa na wanaoendelea kushirikiliwa ni 80, ambao watafikishwa mahakamani .
- ARUSHA: Wafuasi wa CHADEMA wanashikiliwa Polisi kwa tuhuma za kufanya vurugu nyumbani kwa mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Kaloleni, Emmamuel Meliali.
- DODOMA: Habari kutoka ndani ya kikao cha CCM Dodoma zinaema mawaziri watatu wamekubwa na kadhia ya kijiuzulu kabla ya kulazimishwa na Rais. Mawaziri hao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Dk. Shukuru Kawambwa, kutokana na matokeo mbaya ya mitihani ya kidato cha nne. Mwingine ni Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara ambaye yeye alituhumiwa kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari na hivyo kufanya chama pamoja na serikali yake kushambuliwa, vile vile kushindwa kushughulikia suala la ukosefu wa ajira kwa vijana. Mwingine ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David Mathayo. Nao Wabunge, Kangi Lugola (Mwibara) na Deo Filikunjombe (Ludewa), walishambuliwa kwa kukikosoa serekali ndani ya Bunge kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwapa nafasi wapinzani kuishambulia serikali. Wabunge hao hata na hivyo hawakuwa wamehudhuria kikao hicho.
- Chama cha Wananchi (CUF), kimekana kuhusika na vurugu zinazotokea katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na kwamba zinatokana na sera mbaya za Serikali za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
- KILIMANJARO: Gari aina ya Toyota Landcruiser linalotumiwa na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Mkoa wa Arusha, lilikamatwa juzi saa 4:00 usiku huko Himo, Moshi Vijijini, likiwa limesheheni magunia 18 ya bangi, likiisafirisha kwenda Tarakea, Rombo. Polisi wawili akiwamo dereva wa gari hilo wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Himo na gari lipo Makao Makuu ya FFU, Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro.
- Mrisho
Ngassa amerejea kwenye klabu yake ya zamani ya Yanga kwa mkataba wa
miaka miwili uliosainiwa asubuhi ya leo katika makao ya klabu hiyo
makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Kimataifa
- UINGEREZA: Klabu ya Chelsea iko tayari kuingia hasara ya Sh4 bilioni kwa kumuuza mshambuliaji wake Fernando Torres aliyenunuliwa kwa Sh 6 bilioni katika juhudi za kumnasa Wayne Rooney kutoka Manchester United.
- KENYA: Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga amekanusha madai kuwa ameahidiwa kazi serikalini na Rais Uhuru Kenyatta. Amesema tayari ana kazi ya kutumikia Wakenya.
Source: http://www.wavuti.com/
No comments:
Post a Comment