Wekundu wa Msimbazi
WEKUNDU wa msimbazi Simba leo hii
wametoa dozi nyingine kwa maafande wa Mgambo Shooting kutoka mkoani
Pwani baada ya kuwatungua bao 1-0 sifuri katika mchezo wa ligi kuu soka
Tanzania bara.
Mchezo huo uliotawaliwa na soka la
ufundi umepigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam na
kushuhudiwa na mashabiki wengi wa Simba wenye matumaini makubwana kikosi
chao kipya.
Mnyama sasa amefufua matumaini ya
kucheza michuano ya Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
JKT Mgambo leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na
refa Andrew Shamba, aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Abdallah Mkomwa
wote kutoka Pwani, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na kiungo hatari
wa pembeni, Haroun Athumani Chanongo dakika ya nane, ambaye aliombea
mpira katikati ya Uwanja na kuanza kuwapangua mabeki wa Mgambo kabla ya
kumchambua kipa Godson Mmasa.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC
itimize pointi 45, sasa ikizidiwa tatu na Azam FC inayoshika nafasi ya
pili, ambayo Jumapili itamenyana na Mgambo kwenye Uwanja wake wa Azam
Complex, Chamazi.
Katika mchezo wa leo, kocha Mfaransa
Patrick Liewig aliwapumzisha wachezaji kadhaa tegemeo, Mrisho Ngassa,
Shomary Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu na Mussa Mudde kuelekea
mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga Mei 18.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Juma
Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’/Omary Salum, Haruna Shamte, Miraj Adam,
Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucian
‘Gallas’/Rashid Ismail, Amri Kiemba, Ramadhani Singano ‘Messi’/Salim
Kinje na Haroun Chanongo.
JKT Mgambo; Godson Mmasa, Salum Mlima,
Ramadhani Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga,
Chande Magoja/Mussa Gunda, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga
na Nassor Gumbo.
Chanzo: www.fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment