Dar es Salaam.Licha ya kufanikiwa kutwaa taji,
Yanga imeshindwa kufikia rekodi ya watani zao Simba waliyoweka msimu
uliopita iliponyakua ubingwa kwa kujikusanyia pointi 62.
Yanga mwishoni mwa wiki iliizabua Simba mabao 2 -
0, na kutangazwa mabingwa wapya wa msimu wa 2012-2013 ikiwa na jumla ya
pointi 60, ambazo sawa na tofauti ya pointi mbili.
Katika upachikaji mabao, Yanga imetoshana nguvu na
mtani wake Simba, ambayo msimu wa 2011-12 ilitumbukiza wavuni mabao 47,
idadi iliyofikiwa pia na Yanga msimu huu.
Katika ulinzi, Yanga imeshidwa kupiku rekodi ya
Simba ambayo mpaka ina kamilisha msimu wa iliruhusu mabao 12 pekee
wakati Yanga imemaliza msimu huu imefungwa mabao 14.
Pia, msimu wa 2011-12, Yanga ilihitimisha msimu
ikiwa imetunguliwa mabao 30, tofauti na Simba ambayo licha ya kumaliza
nafasi ya tatu msimu uliomalizika
ilibwagizwa mabao 23.
Katika hatua nyingine, ukata wa mabao ulionekana
kuuvamia msimu wa 2012-13 uliofikia tamati Mei 18, ambapo mabao 370
pekee yaliyotinga nyavuni.
Idadi hiyo ni pungufu ya mabao 40 ambayo
yalishuhudiwa yakitinga nyavuni msimu wa 2011- 2012, ambao jumla ya
mabao 410 yalitazamwa yakigusa nyavu.Text inakuja hapa.
source: mwananchi
source: mwananchi
No comments:
Post a Comment