Dodoma/Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete
amemwagia sifa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hatua ambayo
inaweza kutafsiri mengi katika medani ya siasa nchini.
Akizungumza na wabunge wa CCM kwenye Ukumbi wa White House Dodoma juzi, Rais Kikwete ambaye pia mwenyekiti wa chama hicho, alisema nguvu za Lowassa pekee zinatosha kushinda uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.
Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli, ambako Lowassa amekuwa mbunge wake tangu mwaka 1995.
Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza
kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa
Makuyuni, baada ya kuwa ametoa ruksa kwa makada wa chama hicho wanaotaka
urais kuanza kujipitisha pitisha miongoni mwa wanachama wa chama hicho.
Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa wanaCCM wanaotaka kumrithi Rais
Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
“Sina tatizo na pale Makuyuni, najua muscles (misuli) za Mzee Lowassa zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?” alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM akimnukuu Rais Kikwete.
Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Makuyuni unaotarajiwa kufanyika Juni 16, mwaka huu, utakuwa wa ushindani mkali kati ya CCM na Chadema ambao historia yao kisiasa mkoani Arusha ni ya uhasama.
Katika uchaguzi huo, unaofanyika baada ya kifo cha
Abdillah Warsama (CCM), chama hicho kitatetea nafasi yake kwa
kumsimamisha Godluck Lerunya na Chadema ni Japhet Sironga.
Mbali na Kata ya Makuyuni, uchaguzi wa udiwani mkoani Arusha utafanyika pia katika Kata za Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai, kutokana na waliokuwa madiwani wa kata hizo (Chadema), kufukuzwa na chama chao.
“Mnaweza kuchafuana leo, kesho mkapata mgombea mwenye nundu nyingi na mabandeji kila mahala, halafu mkapata shida kumnadi,” alisema.
Siyo mara ya kwanza kwa Kikwete kumsifia Lowassa kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka jana huko Longido wakati akikabidhi ng’ombe.
Pia aliwahi kumsifia wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 wakati Kikwete alipomwelezea Lowassa kama Mbunge makini na kuwaomba watu wa Monduli kumchagua tena.
Hata hivyo, alipoulizwa kama baada ya kuruhusiwa
kuanza kujipitisha kwa wanaCCM kama anataka kuwania urais, Lowassa
alijibu kupitia watu wake wa karibuni kuwa asingependa kuzungumzia suala
hilo hasa baada ya Rais kutoa kauli hiyo.
Rais Kikwete aliwaeleza wabunge hao kuwa si kosa kwa watu kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo urais mwaka 2015.
“Wabunge na mawaziri wenye nia ya kutangaza nia ya kugombea urais wawe huru, kwani hiyo ni haki yao, isipokuwa wafanye kwa wema bila kukivuruga chama na kuwagawa wanaCCM katika makundi. Sioni tatizo watu kujipitisha. Sisi sote hapa tulijipitisha. Lakini tufanye hivyo kistaarabu bila kuvurugana.”
“Mkutano kama huu nchi kama Kenya watauripoti vizuri na kwa undani hivyo mfanye hivyo si kila kitu urais 2015,” alisema Membe. Mkutano huo utaanza Mei 28, hadi Juni Mosi na utajadili jinsi gani sayansi na teknolojia vinaweza kutumika kuzikwamua kiuchumi.
chanzo: Mwananchi: Imeandikwa na Kizitto Noya, Habel Chidawali na Boniface Meena.
Kutangaza nia ruksa

Aliwaagiza wabunge wa chama hicho kwenda majimboni mwao kusikiliza kero za wananchi badala ya kusubiri wakati wa uchaguzi.
Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe ambaye naye anatajwa kuwa miongoni mwa wagombea
amewataka waandishi waache kuandika kila siku habari za urais na badala
yake waandike mambo ya maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya
kukutana na mabalozi wa nchi zinazoendelea kuhusu Mkutano wa Smart
Partnership, unaotarajiwa kufanyika nchini, Membe alisema ni vizuri
yakaandikwa mambo ya maendeleo na si kila wakati kuandika mambo ya
urais.
“Mkutano kama huu nchi kama Kenya watauripoti vizuri na kwa undani hivyo mfanye hivyo si kila kitu urais 2015,” alisema Membe. Mkutano huo utaanza Mei 28, hadi Juni Mosi na utajadili jinsi gani sayansi na teknolojia vinaweza kutumika kuzikwamua kiuchumi.
chanzo: Mwananchi: Imeandikwa na Kizitto Noya, Habel Chidawali na Boniface Meena.
No comments:
Post a Comment