Mitihani kidato iv kusahihishwa upya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Tume ilioundwa na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda kuchunguza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka
jana, LEO imeitaka serikali ifute matokeo yote na mitihani isahihishwe
upya.
Akisoma ripoti ya Tume hiyo hivi punde
bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia sera na uratibu, William Lukuvi amesema kwamba mitihani
hiyo inapaswa kusahihishiwa kwa kuzingatia vigezo vilivyotumika katika
kusahihisha mitihani ya kidato cha nne mwaka 2011.
Mwaka jana matokeo ya wanafunzi wa
kidato cha nne yalikuwa mabaya kuliko matokeo mengine yaliowahi kutolewa
na Baraza la Mitihani la Taifa. Wanafunzi walifeli kwa asililimia 60.
Kutokana na matokeo ya tume hiyo, Lukuvi ameipongeza tume hiyo kwa kutoa matokeo hayo.
Wataalamu wa elimu wanasema kwamba
endapo serikali itatekeleza pendekezo hilo itaingia kwenye gharama kubwa
ambazo pengine zitaigharimu serikali.
Chanzo: Habarimasai.com
No comments:
Post a Comment