Mbeya. Rais Jakaya Kikwete
amesema kuwa kuna haja ya kuruhusu ajira za walimu kutoka katika nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kupunguza tatizo la upungufu
wa walimu wa sayansi na kuboresha kiwango cha Elimu ya Tanzania.
Kauli hiyo ya Rais imekuja baada ya Shirikisho la Wamiliki, Mameneja wa shule na Wakuu wa vyuo Binafsi Tanzania (Tamongsco) kumweleza kuwa walimu kutoka nchi za Afrika Mashariki wamekuwa wakilazimika kulipia dola 1,500 kwa ajili ya kibali cha kuja kufanya kazi hapa nchini.
Kikwete alisema kuwa katika mambo ambayo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubalina katika suala la ajira ni pamoja na kila nchi kueleza ajira ambazo inazifungua na ambazo itazifunga nchini kwake.
“Katika suala la hili la gharama kubwa
wanazolipa hawa walimu wanaotoka katika nchi za Jumuia ya Afrika
Mashariki litakwisha kwani tumekubaliana kuwa kila nchi itaeleza ni
ajira zipi ambazo itazifungua na zipi itazifunga hivyo katika sekta ya
elimu kuna haja ya kuachia ili tuweze kuwapata hao walimu” alisema.
“Kuna jambo ambalo tumesema kuwa Tanzania
tunahitaji walimu wa somo ya Sayansi, Kiingereza na Hisabati ili kuweza
kuboresha elimu katika nchi yetu kwa kumaliza tatizo hilo la upungufu
wa hao walimu,”alisema.
source: mwananchi
source: mwananchi
No comments:
Post a Comment