Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bw ,Benard Membe akiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu mkoa wa Iringa wanaotoka mkoa wa Mtwara na Lindi jana |
Waziri Membe |
Na Francis Godwin,Iringa
HUKU hali ya mambo ndani ya
chama cha mapinduzi (CCM) kuwa si shwari kutokana na makada wake
kuendelea kupigana vikumbo ikiwa ni sehemu ya harakati mbio za urais
mwaka 2015 , waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe
ameibuka na kutoa ya moyoni kuwa atakuwa tayari kuwania urais mwaka
2015 iwapo wananchi wataona anafaa na watamtaka agombee nafasi hiyo.
Pia waziri Membe alisema kuwa
hali ya nchi inavyokwenda kwa sasa si shwari kutokana na baadhi ya
wabunge wa CCM na vyama vya upinzani kuendelea kuzungumza ovyo
ovyo juu ya chama na serikali jambo ambalo ni hatari zaidi kwa
Taifa.
Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akijibu maswali ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusu mbio hizo za Urais .
mtandao huu ulifanya mahojiano
hayo mjini Iringa baada ya kumalizika kwa kongamano la wana vyuo
vya elimu ya juu mkoani Iringa kongamano lililofanyika katika ukumbi
wa St. Dominic ambako alikuwa mgeni rasmi waziri Membe alisema kuwa
pamoja na kauli yake ya kwanza kwa Taifa kuwa muda bado kufika wa
kufanya hivyo .
Waziri huyo alisema kuwa
mbali ya kuwa muda wa kutangaza kuwania nafasi hiyo bado haujafika
na chama chake kina utaratibu wa kutangaza mara baada ya muda
kufika ila kwa mtazamo wake kama alivyopata kuueleza umma awali
alipozungumza na vyombo vya habari juu ya mbio hizo za urais
,alisema kuwa anaheshimu sana taratibu za chama .
" Naomba kurudia tena mimi
nilishapata kuueleza umma kuwa muda bado haujafika wa kutangaza
kugombea Urais ....ila nasema hivi natagemea sana ushauri wa
watanzania iwapo wataniona nafaa na kunitaka nigombee nitapima
mawazo yao na iwapo ni wananchi wengi watakaoniunga mkono kutaka
nigombee basi nitachukua fom na kuijaza ili nigombee nafasi hiyo
kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu " alisema waziri Membe
kuwa kama wananchi watasema jaza fom na nikaona ni sauti ya wengi nitajaza fomu ya kuwania kiti cha urais
Pia alisema kuwa hadi sasa
hali ya nchi inazidi kwenda vibaya kutokana na kila mtu kuzungumza
mambo bila kuthathimini na kuwa mbaya zaidi hata baadhi ya
wabunge wa CCM nao wamekuwa si msaada kwa chama kutokana na mambo
wanayozungumza dhidi ya serikali na chama.
Kuhusu mwenendo wa bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sasa waziri Membe alisema kuwa
kwa upande wake amepata kukaa bungeni zaidi ya miaka 15 toka
bunge la spika Pius Msekwa hadi sasa chini ya spika Anne Makinda ila
anachokiona ni baadhi ya wabunge kukosa maadili na kuzungumza mambo
bila kuzingatia kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari zaidi.
Alisema kuwa bunge
linalotazamwa na watanzania ni lazima liwe bunge lenye mfano wa
kuigwa na lenye kuzingatia maadili katika kuzungumza ila kwa sasa
ndio maana bunge linaendelea kupoteza mwelekeo wake .
"Bunge linapoteza mwelekeo
kutokana na mawazo ya baadhi ya wabunge wakifikiri wakisema ovyo na
kutumia lugha kali katika kuzungumza basi wao ndio wanaonekana
ni wabunge bora kitu ambacho hakipo ....kwani kuwa mbunge ni pamoja
na kujiheshimu na kutumia lugha nzuri katika kuwakilisha wapiga kura
wako bungeni"
Waziri Membe alisema kuwa
kitendo cha baadhi ya wabunge kutotumia busara katika kujadili
mambo bungeni si ubunge mzuri na watambue wazi kuwa wananchi wao
wanawatazama na hukumu yao itatolewa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu
kama hivyo wanachokifanya ni kuwawakilisha wananchi ama
kujiwakilisha wao.
"Nawaomba wabunge kuwa
wazalendo na kuwawakilisha wananchi waliowatuma badala ya
kuligeuza bunge kama sehemu ya kuonyesha ujuzi wa kuzungumza ovyo
....nasema tuwaogope wananchi mwaka 2015 watatoa adhabu kwa kila
mbunge kwa sasa wananchi wanakusikiliza na kunakutazama ila muda
ukifika watakuacha"
Alisema kuwa wabunge wengi ni
vijana na wanafikiri kusema vibaya juu ya CCM ndio ubunge bora
ila watu watafanya uchunguzi wa kutembelea jimbo la mbunge husika
na kuangalia kuwa amefanya nini katika jimbo lake na watakupima kwa
kazi uliofanya na sio ukali wako bungeni.
Aidha waziri Membe alisema
kuwa baadhi ya wabunge wa CCM wamekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi
katika majimbo yao na pia wamekuwa msaada kwa chama na serikali
chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa msaada mkubwa wa kusukuma mbele
maendeleo ya Taifa ila baadhi yao wapo kwa ajili ya kuonyesha uwezo
wao wa kusema ovyo.
source: www.francisgodwin.blogspot.com
No comments:
Post a Comment