WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, May 11, 2013

yanga yatenga Sh150m kuiua simba

yanga 45743
Yanga
YANGA imeweka fungu la Sh.150 milioni mezani kuwapa motisha wachezaji wake iwapo wataifunga Simba Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mgawo huo kila mchezaji atalamba  shilingi milioni tano taslimu.

Hiyo ni kama advansi. Uongozi pia umetenga fungu jingine la Sh.100 milioni kwa ajili ya sherehe za Jangwani baada ya mechi ya Simba, kwenda Bungeni, Dodoma pamoja na Zanzibar.

Awali Yanga walikuwa wamewaahidi wachezaji wake zawadi ya Sh.100 milioni lakini jana Ijumaa Ibrahim Akilimali ambaye ni Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga alitamka kwamba wameongeza Sh. 50 milioni na kufanya ziwe Sh.150 milioni kwa timu tu.

Hiyo inamaanisha kwamba katika wachezaji 30 kwenye mgawo huo kila mmoja anakunja shilingi milioni tano na chenji chenji.

Akilimali alisisitiza kuwa fungu hilo litahusisha zawadi ya Sh. 70 milioni ya bingwa wa Bara.

Katika hatua nyingine, Yanga imeondoka jana Ijumaa kwa mafungu matatu kuelekea Pemba, Zanzibar kuweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao Kocha Ernest Brandts amesisitiza kuwa anataka mvua ya mabao.

Fungu la kwanza la wachezaji liliondoka  asubuhi, la pili likaondoka jioni na la tatu litaondoka leo Jumamosi alfajiri.  Kutoka Dar es Salaam mpaka Pemba kwa ndege ni mwendo usiozidi dakika 45.

 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

No comments:

Post a Comment