Azam FC
Jana katika uwanja wao wa nyumbani
Chamazi, Azam fc wameshuka dimbani kuvaana na maafande wa Mgambo
Shooting kutoka mkoani Tanga “Waja leo waondoka leo” huku wakihitaji
sare ama suluhu ili kupata pointi moja na kujihakikishia nafasi ya pili
msimu huu.
Hatimaye dakika tisini zilimalizika
kwa wachezaji John Bocco “Adebayor” aliyejuta na kuwaomba radhi
watanzania kwa kukosa penati muhimu nchini Morroco, Kipre Herman
Tchetche pamoja na Attudo kufunga bao moja moja na kurudisha furaha
kubwa kwa mashabiki, viongozi na benchi la ufundi la klabu hiyo chini ya
kocha Muingereza Sterwat John Hall.
Sasa Azam wametetea nafasi yao ya
umakamu bingwa baada ya kufikisha pointi 51 na kuwachinjilia mbali
wekundu wa Msimbazi Simba waliokuwa wanawania nafasi hiyo.
Afisa habari wa klabu ya Azam fc Jafar
Idd Maganga amesema ushindi wa leo umetokana na mipango waliyojiwekea
tangu wapoteze mchezo nchini Morroco.
Jafar alisema baada ya kutolewa na FAR
Rabat walisikitika sana na wakajipanga kurejea tena katika mashindano
hayo mwakani na mipango yao ilikuwa kushidna mchezo wa leo ili kuitwaa
nafasi ya pili na kuiwakilisha nchi kwa mara nyingine michuano ya
kimataifa na hatimaye wameweza leo hii.
“Azam imedhihirisha kuwa ni timu nzuri
na inacheza soka safi, tutaendelea kuwapa burudani mashabiki wetu na
sasa tunajipanga zaidi kufanya vizuri michuano ya kimataifa zaidi ya
mwaka huu”. Alisema Jafar.
Jafar aliongeza kuwa baada ya ushindi
wa leo wataendelea kukaa kambini kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya
maafande wa JKT Oljoro katika dimba la Shekh Amri Kaluta Abeid jijini
Arusha.
Azam fc msimu wa mwaka jana walikuwa
katika kinyang`anyiro cha kuwania ubingwa na Simba, mwaka huu Simba
kajitoa na kuwaacha wana lambalamba hao kubaki na wanajangwani katika
mbio za kuwania ubingwa, lakini mbio hizo zimeishia ukingoni kwa Yanga
kutwaa taji msimu huu na kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa
barani Afrika mwakani.
Chanzo: www.fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment