WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 31, 2015

BAADHI YA MATUKIO YALIYO TIKISA TAIFA KATIKA MWAKA 2015mwaka 2015 kama taifa tumeshuhudia ajali nyingi sana zikiendelea kudhoofisha uchumi wa taifa letu kwa kuwapoteza watanzania wenzetu wengi ambao wamefarika katika ajali zilizosababishwa na ajali nyingi za barabarani kama makala ya hapo juu ilivyoelezea. umekuwa mwaka wa huzuni kubwa kwani kuna baadhi ya ajali tungeweza kuzizuia kama wahusika wangekuwa makini.
Katka mwaka wa 2015 Mheshimiwa Zitto aliaga rasmi kuachana na chama cha CHADEMA; lilikuwa ni tukio ambalo liligusa nyoyo za wapenzi wengi wa siasa wale wa upinzani na wa chama tawala pia.Katika Mwaka huu wa 2015 Mheshimiwa Lowassa alikihama chama cha mapinduzi na kujiunga na chama cha Upinzani CHADEMA ili kuweza kuwania kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.DR. John Pombe Magufuli aliteuliwa na chama chake ili kuogombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi, kutoka kuwa hakuwa na makundi ndani ya chama hicho , uwajibikaji wake uadilifu wake ndivyo vilimfikisha hapo alipofika.Katka Mwaka wa 2015 tulishuhudia Prof Ibrahim Lipumba akiamua kuacha na siasa kama mwenyekiti wa CUF na Mwenyekiti Pacha wa UKAWA, kwa kuto ridhika na taratibu ndani ya UKAWA katika harakati za kumpata mgombea urais kupitia muungano huo.


Dr Slaa pia katika mwaka huu wa 2015 aliamua kuachana na siasa akiwa kama katibu mkuu wa CHADEMA. hilo lilitoka na tofauti zilizojitokeza ndani ya UKAWA. lilikuwa ni tukio lililovuta hisia za wengi.Tukio nyingine kubwa katika mwaka wa 2015 ni CCM kushinda uchaguzi Mkuu uliofanyika October 2015 ; ambapo mgombea wa urais wa CCM Dr. JPM na Makamu wa Kwanza Mwanamke katika historia ya Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan walikabidhiwa vyeti vya ushindi.DR. JPM awashukuru wana CCM kwa kumchagua na kuanza kuwasha cheche kuhusu unafiki wa baadhi ya wanachama wa chama hicho


Tumeshuhudia Rais DR. JPM akianza kazi kwa ujasili wa kuwa tayari kutumbua majipu ambayo yamerudisha sana nyuma maendeleo ya watanzania.

katika mwaka huu 2015 tuliona wananchi kuguswa na hotuma ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alipofungua Bunge la 11 kwani ilikuwa imegusa kiu yao na matarajio yao ya muda mrefu. ilikuwa hotuba ambayo imeonyesha mwelekeo wa serikali yake kwa kipindi cha miaka 5 ya utumishi wake kwa umma wa watanzania hasa wanyonge.


Ilikuwa shangwe na vigelegele wakati DR.JPM alivyofanya ziara za kushitukiza na kugundua jinsi watanzania walivyokuwa wakikosa hudumu muhimu kwa uzembe wa wa watendaji, hivyo Katibu Mkuu Kiongozi alitoa mchumuisho wa ziara ya Mheshimiwa Rais na majumuisho ya uwajibikaji kwa wazembe.


Katika mwaka huu wa 2015 Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara ya Ghafla Bandarini Na TRA na kujionea njinsi Taifa lilivyokuwa likipoteza kiasi kukubwa cha mapato kwa Tamaa ya watendaji wachacche ambao walikuwa hawana maadili.  ziara hiyo iliweza kubadilisha ukusanyaji wa mapato na serikali kuanza kupata mapato mengi zaidi.


Katika mwaka wa 2015 tumeshuhudia jinsi Rais Dr. JPM akishiriki kufanya usafi wa mazingira. Lilikuwa ni tukio ambalo liliweza kumjumuisha kila mtu kushiriki kufanya usafi ikiwa na sehemu ya kusherekea siku ya kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu.

Tunawatakieni sherehe njema za kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 kwa amani na utulivu na tuendelee kumwombea Rais wetu ili katika mwaka huu wa 2016 aendelee kutekeleza majuku yake, kwa kasi kwa faida ya watanzania kama alivyoanza. Mwenyezi Mungu amjalie afya njema  Amen
.

No comments:

Post a Comment