JE SERIKALI ZETU ( JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR) ZIMEGUNDUA NINI?
Kwa niaba ya Blogs ukadirifu na mungupamojanasi, tumepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya meli ya MV SKAGIT,iliyokuwa
ikisafiri kutoka Dar kuelekea Zanzibar, ambayo imesababisha watanzania wenzetu
zaidi ya 40 kupoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa. Napenda
kuungana na watanzania wote katika kutoa mkono wa pole kwa familia na ndugu
zetu ambao wamepotelewa na wapendwa wao katika ajali mbaya na ya kusikitisha ya
Mv. Skagit ambayo ilitokea tarehe 19 July 2012. Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema
tunaomba aendelee kuwafariji majererui
wa ajali hii na kuwawezeshe kupona haraka ili waendelee na majukumu yao ya
kulijenga Taifa.
Kama watanzania
tutaendelea kumshukuru Mungu kwa ndugu zetu ambao wametangulia mbele ya haki kutokana
na ajali hii pamoja na ukweli kuwa ajali hii ni uzembe mkubwa sana unaotokana
na mikono ya baadhi ya watendaji na wasimamizi wa sheria za usalama wa abiria
ambao wamekabidhiwa Dhamana ya usimamizi
wa sheria hii kwa masalahi ya Taifa; lakini kwa makusudi au katika kutimiza
haja zao binafsi wanasababisha maafa makubwa kwa Taifa.
Ninajaribu kutafakari katika
makala hii, matukio makubwa ya ajali za majini achana na ajali mbaya
zinazohusiha barabara. Kama Mtanzania najaribu kujiuliza maswali mengi ambayo
hayapati majibu; lakini swali langu kubwa ambalo litatawala makala hii ni hili:
Je baada ya
tukio baya ambalo lilikuwa kubwa na la
kusikitisha sana ambalo lilihusisha Mv Bukoba May 21,mwaka 1996 ambapo zadi ya
watu 800 walipoteza maisha, kwa nini sisi kama Taifa tumeruhusu ajali nyingine
mbili mbaya kutokea katika pwani ya Zanzibar katika kipindi ambacho hakizidi
mwaka mmoja?
Lakini kabla ya kufikiri
kuwa sasa mambo yote ni sawa Hata mwaka
haijapita tangu ajali mbaya ya MV Spice Islander iliyozama pwani ya nungwi na kuua
watanzania wenzetu zaidi ya 200. Na hata mwaka haujeisha wiki hii
tumeshuudia kuwa Mv. Skagit ambayo
ilikuwa na abiria zaidi ya 200 nayo ikipatwa na ajali mbaya na kupoteza zaidi
ya watanzania 40 katika pwani ya chumbe.
Tukijaribu kusahau ajali
ya Mv. Bukoba takribani miaka kumi na tano iliyopita; pamoja na msemo wa
Kiswahili usemao kuwa “ajali haina
kinga” lakini ajali hizi mimi binafsi zinanirudisha
katika kipengele kimoja kikubwa kuwa kama Taifa tumeshindwa kusimamia sheria
zetu sihusuzo usala wa Raia wakiwa safarini; hapa mimi naweza kusema kuwa
ninapima uwezo dhaifu wa wahusika ambao kama Taifa tumewapa dhamana ya
kuzisimamia sheria zetu.
Tatizo nyingine kuna ugumu
gani wa kutunza kumbukumbu za wasafiri ambao wanasafiri na chombo husika; tumekuwa
Taifa ambalo hata takwimu za abiria ambao wamesafiri au wamehusika na ajali
hazipo kama ziko haziko sahihi; Ajali ikitokea ndipo taarifa zinaanza
kutafutwa; matokeo yake taarifa zinazotolewa zinatofautiana, na inakuwa ni aibu
kubwa kwa pengine kuwaeleza wananchi taarifa ambazo sio sahihi:
Ama kweli ni aibu kubwa
inakuwa kwa Waziri mwenye dhamana anapotamka takwimu ambazo sio sahihi na
zinaendelea kubadilika kulingana na mazingira ya uokoaji; ni ikitokea kuwa mimi
ni waziri mwenye dhamana na sina uhakika na usahihi wa takwimu hizo, sitaweza
kutamka takwimu hizo kwani kwa kufanya hivyo tunaendelea kuimarisha mfumo
mbovu wa ukusanyaji wa takwimu za
wasafiri.
- Je vyombo vyetu vya majini hufanyiwa ukaguzi wa kina vinapoingizwa nchini wakati wa kusajiliwa, kubaini kuwa chombo kinafaa kwa matumizi ya kweli ya binadamu?
- Je wakaguzi wa wizara hufanya nini au hukagua nini kabla ya chombo kuondoka?
- Je usalama wa Taifa ambo wanakuwa katika bandari zetu wnafanya nini wananagalia nini yaani hata abiria wakijazwa wao hubaki kimya bila kutoa taarifa katika ofisi husika?
- Kwa maneno mengine kwamba vyombo vyetu vinapoondoka bandarini havikaguliwi?
- Watanzania wengi tunaendelea kujiuliza kwa nini meli ijaze kupita kiasi?
- Ni nani msimamizi wa meli zetu na kwa nini meli zetu zisichukue watu kulingana na uwezo wake?
- Sasa tufanye nini katika kuzuia ajali hizi zisiendelee kumaliza Taifa letu katika siku za usoni?
Lazima tukubali kuwa kujifunza kutokana na
ajali hizo kuwa vyombo vingi vya usafiri vibovu ambavyo vinanunuliwa kuletwa
kwetu baada ya kutumika sana katika nchi husika na kisha hupakwa rangi na
kufanyiwa matengenezo madogo ka msingi huu vimekuwa vimepoteza sifa ya
kusafirisha abiria na mizigo yao; kwa sababu ya ubovu wa vyombo hivyo na kwa
sababu ya ukiukwaji wa sheria ambao huwafanya wamiliki kupakia abiria wengi
kuliko uwezo wake nap engine ikitokea hali ya hewa mbaya (upepo ambo
utasababisha mawimbi makubwa) chombo kama hicho hakiwezi kuhimili kishindo
itaishia kukosa mwelekeo na hatamaye kupinduka tu.
Wengi tunajiuliza ilikuwaje
mamlaka zinazohusika zikaruhusu meli iliyobeba abiria zaidi ya uwezo wake ikaruhusiwa
kusafiri? Au pengine wahusika wa usalama
wa abiria bandari walipokea chochote ndipo wakaruhusu meli kuondoka? Lazima
tukubali kukosolewa ajali hizi zote sababu yake kubwa ni uzembe wa utendaji
kazi wetu; uzembe huu ulisababisha yaliyotokea
Mv Bukoba, mv spice islander na sasa Mv Skagit bado tumekuwa wagumu wa
kujifunza.
Je
Professionality ya manahodha wetu iko wapi? Ningekuwa mimi nahodha
ningethubutu kusema hatuondoki hapa mpa abiria wapunguzwe. Vile vile katika hali mbaya ya hewa ninge
sitisha safari kwa usalama wa Watanzania wenzangu. Tumeyaona haya katika nchi
za wenzetu ambao wanaheshimu sheria za usalama wa abiria:
Je Concord
baada ya ajali ziko wapi? Nimeshangaa
tu kwa nini mnjanja mmoja hajezinunua na kuzileta kwetu kwenye nchi ya
majaribio ya vitu chakavu na vyema matatizo ya kiufundi:
Ni aibu kubwa sana kwa wataalamu
ambao ndio wanatumaliza kwa tamaa zao binafsi ambao wanashindwa kuwashauri
wamiliki wa meli aina gani ya meli wanunue wameshindwa kutumia maadili ya kazi zao katika kuwasaidia wamiliki
kufanya uamuzi sahihi. Sasa fikiria taarifa za kuwa Mv. Skagit kabla ya kuja
kwetu; Undani wa ajali ya meli hii ni kama ifuatavyo: Meli iliponunuliwa
ilikuwa tayari imekwishatumika. Meli hii ina miaka zaidi ya 35 ya uhai wake
sasa mmiliki wa chombo hiki alipata ushauri kabla ya kununua chombo hiki au
alipuuzia ushauri?
Tunaomba serikali zetu ziangalie zaidi katika Viwango (standards) za meli zetu hapa naendelea kujiuliza kuwa je kweli tuna meli zenye viwango kulingana na bahari Zetu?
Tunaomba serikali zetu ziangalie zaidi katika Viwango (standards) za meli zetu hapa naendelea kujiuliza kuwa je kweli tuna meli zenye viwango kulingana na bahari Zetu?
Wataalamu wetu naamini
kabisa wanao uwezo uwezo wa kuangalia mambo haya kisayansi na kuyaelewa na kuja
na mapendekezo ya kisayansi yanaweza kutunaweza kuondokana kwa kiasi kikubwa cha ajali hizi kama
tutafanikiwa kuandaa utaratibu wa Usimamiaji wa sheria za usalama wa abiria kwa
msingi wa maadali yake; pamoja na kuzingatia Usimamiaji na ubora wa vyombo vya
usafiri na ukaguzi wa kuona kama vinafikia kiwango kinachostahili
Je
sisi watanzania ni kweli wavivu
wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi
kama abiria kwani chombo cha usafiri kikijaa tunalazimishwa kupanda?
Jamani kwani sisi kama
wananchi huru tunakuwa tayari kupanda chombo wakati tunaona hali ya chombo? Na
wala sio shetani kama tunavyojiambia na tunayaweka maisha yetu rehani tena kwa
makusudi na lolote baya likitokea tunaanza kulaumiana.
baada ya matukio haya yoye pengine ni wakati muufaka kwa serikali kufikiria ununuzi wa meli kubwa kama ilivyokuwa huko nyuma ambayo inaweza kukidhi haja ya watanzania wanyonge. Pengine kwa njia hii tunaweza kujenga msingi madhubuti kuhakikisha uzembe wa aina yoyote ule unaepukwa kulinda isije kutokea ajali kama hizi.
Kama
mheshimiwa Raisi
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Shein ambaye
alisema kuwa “Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema
tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa ni kuokoa
maisha ya watu” maneno haya ni mazito lakini hatutatenda
haki kama hatutaendelea kuwakumbusha watendaji husika umuhimu wa kurekebisha
vyanzo vya ajali kama nilivyoainisha
hapo juu ili kuliepusha taifa hili kuwa na wasimamiaji wabovu wa sheria na
kuiepusha nchi yetu nzuri Tanzania katika majanga ya ajali za
kila siku;
MUNGU IBARIKI TANZANIA
No comments:
Post a Comment