MAENDELEO
YA NCHI YANATEGEMEA SANA MAONO (VISION) YA KIONGOZI AMBAYE YUKO MADARAKANI.
Give a person a fish: you have fed the person for
today. Teach a person to fish: you have fed the person for a
lifetime.”
Kumpa
mtu samaki utakuwa umemlisha katika siku ya leo.ukiweza Kumfundisha
mtu namna ya kuvua samaki utakuwa umeweza kumsaidia kumlisha katika
maisha yake yote.
Teach the person how to process and package fish for export and
market it, and you have stimulated economic development.
Ukiweza
kumfundisha mtu namna ya kutengeneza na kusafirisha na kuweza kuuza samaki
katika masoko ya nje; utakuwa umefanikiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi
Park Chung Hee alikuwa kiongozi wa Korea ya Kusini kuanzia mwaka 1961-1970 alipo uwawa.Park Chung Hee alikuwa dikteta lakini alikuwa Rais ambaye alifanya Korea ya Kusini leo hii kuonekana tajiri. Alipoingia madarakani mwaka 1961 alikuwa na vision na vipaumbele ya maendeleo ya nchi yake kwa kutilia mkazo maendeleo ya Elimu, kukuza technologia (ICT),Kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwa na nidhamu ya kazi (dicpline) na kusimamia ukaaji wa Nishati.
Kwa taathimini ya kiuchumi
wakati Park
anaingia madarakani uchumi wa Korea ya Kusini ulikuwa sawa na hali ya uchumi tunaoulaamikia sisi watanzania yaani
uchumi duni na maisha magumu;
Kutokana vision na
uzalendo wake kwa kujitoa kwa utendaji bora na usimamiaji bora wa
rasilimalia za taifa lake leo hii Korea
ya Kusini ni moja ya nchi zenye uchumi imara dunia na inashindana na hata
kuogopewa na nchi ambazo ni tajiri duniani.
Ni takribani zaidi ya miaka 30 toka alipouwawa lakini tafiti zinaonyesha kuwa amebaki kuwa na rekodi bora ambayo imeisaidia nchi yake katika umaarufu ambao Korea ya Kusini inafurahia leo; Park alisaidia sana katika kusimamia ukuaji wa uchumi na usambazaji wa kasi wa uwiano wa kipato, ikilinganishwa na mataifa mengine. Kwa usimamiaji wake bora wa maendeleo kwa wote, Rais Park ilijulikana kama "unforgettable" miongoni mwa Wakorea kwa sababu ya ujuzi wake na nguvu ya usimamiaji wa maendeleo kwa wote.
Kwa nini alifanikiwa katika
kuboresha uchumi wa nchi yake?
Rais Park alikuwa na tabia moja mimi
naiona ni nzuri ambayo iliwashangaza waandishi wengi ndani ya ofisi yake kuwa kuta zilitapakaa
na michoro ya takwimu, ikiwa ambazo zilikuwa zikionyesha mwenendo wa biashara, ukusanyaji wa kodi na taarifa
za maendeleo ya viwanda ambayo
katika nchi yeyote ile ni nguzo imara ya maendeleo. Kiongozi yeyote mwenye maono ya namna hii lazima awe kiongozi bora kwa
maendeleo ya nchi yake.
Swali hapa viongozi wetu
wanatumia muda wao mwingi wakiwa ofisini wanakuwa wanangalia data za aina gani?
Kusoma magazeti?
Je viongozi wetu wanakuwa na muda wowote wa kufuatilia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia ofisi zao?
Kusoma magazeti?
Je viongozi wetu wanakuwa na muda wowote wa kufuatilia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia ofisi zao?
Jambo jingine ambalo ni msingi sana ambalo
pengine viongozi wetu wanatakiwa kulitilia mkazo wanapo yaangalia maendeleo ya kiuchumi kwa nchi yetu kwa kuendelea kutilia mkazo katika kujenga uwezo wa kiufundi unaotokana na elimu ubora
katika fani ya sayansi na teknolojia. Uwezo wetu wa kiufundi ni nguvu itakayo
weza kutoa njia kadhaa za maendeleo ya kiuchumi na mvuto wa makampuni ya kitaalam ya kimataifa kuwekeza ndani ya Taifa letu kwa faida ya Taifa:
Kama taifa “pengine” tuna tunatumia misaada vibaya, lengo la misaada ambayo nchi Hisani hutoa kwa taifa ni katika katika kutatua kero ya uchumi unaotusumbua na na kuyafanya
maisha ya watanzania kuendelea kuwa duni. Matumizi bora ya misaada ya kigeni, katika
miradi ya miundombinu sahihi ni suluhisho namba moja wa umasikini wetu.
Watendaji wetu kuanzia
Kiongozi wa juu kabisa wa Serikali yaani Rais na wengine wote wanaomfuata
wanatakiwa wawe na uwezo wa Kujenga kuboresha uchumi, kupitia sera za mitazamo yakimaendeleo kwa kukuza
mifumo ya kiutawala na sera zinazolenga zaidi katika kusimamia maisha na ukuaji
wa uchumi wa nchi.
Nimejaribu kueleza hayo
yote ili kuonyesha kuwa bila kuwa na uongozi wenye maono usiotafuta faida yake
wenyewe, usiokuwa tayari kuwawajibisha watendaji wabovu na wanaokiuka maadili uvunja
sheria hatuwezi kutoka hapa tulipo,
tutaendelea kufurahia kauli mbiu ambazo
hazina maana wala msingi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa. Kama historia
inavyo onyesha kuwa Rais Park
aliingia madarakani kwa kupindua uongozi ulikuwa madarakani lakini lengo lake lilikuwa maendeleo
ya Korea kusini katika hali yeyote na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi chake kama kiongozi wa nchi.
Je kwa nini sasa Nchi yetu tunafarijika ndani ya
demokrasia lakini tunashindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake?
Kama taifa viongozi wetu
wangeweza kuiga namna bora ya usimamiaji katka kutekeleza majukumu yao:
Swali la msingi je kuna
tija au mabadiliko yeyote yanayotokana na utaratibu huu wa usimamiaji?
Tofauti na Rais Park
yeye alikuwa na wasiwasi mkubwa katika kupima matokeo,na alikuwa hana mchezo
hata kidogo katika hili alikuwa hana msamaha kwa wale wote ambao hawakufikia malengo
ambayo alikuwa amewapangia wengi waliathibiwa kwa kufukuzwa kazi bila huruma na hii ilikuwa inatoa changamoto kwa wale wote ambao walikuwa wamekabidhiwa
madaraka kwa ajili ya Taifa kuwa wawajibikaji. kwani ufanisi ulukuwa unapimwa kwa uwajibikaji na sio propaganda za kisiasa.
Serikali yetu ina hili
tatizo la ufuatiliaji na uwajibishaji wa mara moja; uwajibikaji na uwajibishaji hauko katika kamusi yaviongoziwetu. pengine hili linatokana na namna watendajiwanavyopatikana; Je watendaji wetu wanapatikanaje? kupitia elimu yao? utashi wa kisiasa wa chama kilicho madarakani? au kwa misingi ya urafiki na undugu?
kama majibu ya maswali hapo juu yatalenga zadi katika utashiwakisiasa, urafiki na undugu basi uwajibishai wowote utafanyika baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi; na vision za viongozi wetu zitabaki zaidi za kwenye makaratasi ambazo zinakosa sana kipaumbele na kuthubutu.
kama majibu ya maswali hapo juu yatalenga zadi katika utashiwakisiasa, urafiki na undugu basi uwajibishai wowote utafanyika baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi; na vision za viongozi wetu zitabaki zaidi za kwenye makaratasi ambazo zinakosa sana kipaumbele na kuthubutu.
Je baraza jipya litaleta
ufumbuzi wa tatizo la umasikini?
“watanzania wana matumaini makubwa na serikali
yetu, tusiwaangushe. Njia pekee kwetu sisi ya kutowaangusha ni kufanya kazi kwa
bidii”.
Nionavyo mimi Katika
baraza la jipya tunao Mawaziri ambao wanaweza wakaivusha Tanzania na kupeleka katika nchi ya ahadi iliyojaa
maisha bora kwa kila mwananchi. mawaziri kama Dr.Mwakyembe, Prof. Tibaijuka, Sitta na kadhalika.
Ngoja nimchambue kidogo utendaji mzuri wa Dr. John Pombe
Magufuri, pamoja na mapungufu yake kama binadamu;
Magufuri ni miongoni mwa viongozi wachache ambaye daima huwa anathubutu na daima amekuwa akijielemisha ili kuzielewa
zaidi sheria za nchi na wizara husika;
ni msimamiaji mzuri wa sheria katika utendaji wake sio mnafiki katika utendaji wake hata kama
wakati mwingine maamuzi yake yanakuwa kero kwa kwa watendaji wenzake na wananchi
ambao wanakiuka sheria za nchi na zinasababisha utumiaji wa nguvu na ugumu wa
utendaji na utoaji wa hudumu ya uhakika kulingana na sera au maagizo ya
serikali kuu;
Kimsingi kama
nilivyoainisha hapo juu inawezekana magufuli akawa na madhaifu yake lakini
huwezi kuondoa ukweli kuwa ni miongoni mwa mawaziri wachache sana ambao tunao wanaofanya
vizuri kazi za kusimamia hata kuchukua hatua kali kwa wakati. Hilo hata
wananchi wa kawaida wanalijua na jamii ndio inayo msafisha daima.
Angalia jinsi
anavyosimamia sheria namba 18 ya mwaka 2007 ambayo ilisainiwa na Rais mwenyewe
ambayo inakataza watu kuingilia eneo la hifadhi ya barabara kwa kujenga makazi
au kufanya biashara; pamoja na Mheshimiwa Rais na waziri Mkuu kumpunguza kasi
lakini msimamo wake uko pale pale.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Sadiki aliwahi sema kuwa “Hatukatai hata kama ana upungufu wake, basi
apewe sifa katika yale mazuri anayoyafanya, lakini ukweli ni wazi kuwa Magufuli
ni kiongozi mchapakazi na msimamizi mzuri wa sheria na hilo halipingiki,”
Akiendeleza sifa hizo Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, alisema siku zote
utendaji kazi wa Magufuli unafuata sheria na taratibu “Mnyonge mnyongeni lakini
haki yake mpeni, wengi tunamtambua Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya,
tunakuomba uendelee kufanya hivyo hivyo wala hutofeli na ukiendelea na moyo huo
sote hatutafeli,” aliongeza Kabaka.
Tunacho washauri Mawaziri katika
baraza hili jipya wanatakiwa wachukue tahadhari mapema wasiendelee kufanya kazi
na watendaji wabovu; Kumbuka, samaki mzuri akichanganyika na samaki waliooza
lazima achafuke uvundo.Mawaziri wetu wanatakiwa wajipange upya waache porojo za
kujitetea kwa maneno wajitete kwa vitendo ambavyo vina tija kwa wananchi kwa
maendeleo ya Taifa; Tuna imani na nanyi kama mawaziri wapya tunawatakieni kila la kheri na fanaka katika
kumsaidia mheshimiwa Rais wetu katika
kutimiza kauli mbio ya maisha bora kwa wote.
Viva baraza letu
la mawaziri tunaamini kuwa baraza hilo litakuwa la kiutendaji zaidi. Litachukua
mazuri ambayo Rais Park wa korea ya kusini aliyatumia katika kuboresha uchumi wa
nchi yake. Nafikiri inawezekana kuiga na kuleta katika tamaduni yetu kwa ajili
ya maendeleo ya Taifa letu.
No comments:
Post a Comment