WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 15, 2011

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUTIMIZA MIAKA 17 YA NDOA LEO NOVEMABER 16 2011










Tunapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kutuwezesha kutimiza miaka 17 ya maisha ya ndoa; mwezi  wa November Tarehe 16, 2011 ni sawa na miaka 17 iliyopita  Mke wangu Mpendwa Grace Peter Myamba (Teacher au Mama Rose) pamoja nami Emmanuel Alois Turuka  tuliunganishwa kuwa  mwili mmoja katika ndoa Takatifu;


Tarehe 16 November 2011 tunamshukuru  Mungu kwa kutuwezesha kutimiza miaka 17 ya ndoa  iliyojaa upendo na furaha pamoja na binti yetu mpendwa Rose Turuka.
Tulikuwa vijana wakati tunaoana na tunazidi kumshukuru Mungu kwani wakati tulio nao ndoa nyingi  hazidumu kwa muda mrefu au kwa miaka mingi.

Katika miaka hii 17 ya ndoa Grace amekuwa kiongozi, mshauri na mama  mtendaji ndani ya familia yetu na nje ya familia yetu amekuwa kimbilio la wale wenye mahitaji ambayo yako ndani ya uwezo wake wa kusaidia kulingana na neema ya Mungu kwa maneno mengine Katika hii miaka 17 Grace amekuwa Mama  wa watoto yatima na wale wanaohitaji msaada bila kujali imani yao au wapi wanatoka;


Ni ukweli ambao haupingiki kuwa ndoa yenye Baraka na inayodumu inahitaji sana matunzo ya hali ya juu na ujasili wa kuifanya iwe bora,(commitment); na ndoa bora hutengenezwa na wana ndoa wenyewe na si vinginevyo,; ndoa bora hujengwa katika mafiga matatu figa la upendo, figa la  msaamaha na figa la mawasiliano bora.


Katika miaka hii 17 tumejifunza kuwa Ndoa bora hujengwa katika msingi wa mawasiliano mazuri miongoni mwa wanandoa wenyewe, bila mawasiliano hakuna ndoa bora. 


katika miaka hii 17 Daima tumekuwa na mawasiliano ya karibu kuhusu nini kifanyike na kinachoendelea katika maisha yetu familia. Mawasiliano baina ya mume na mke yanajumuisha daima mipango iliyokusudiwa au kuimarisha zaidi mitazamo hasi au chanja. Mawasiliano pekee, yatasaidia kubadilisha tabia ambayo sio nzuri ambayo inaweweza kufoofisha uimara wa ndoa;


Katika hii miaka hii 17 tumejifunza kuwa Ndoa bora hujenga katika misingi ya furaha kama vile mazungumzo yanayopelekea vicheko, utani, na vitu vya namana hii ambavyo ni silaha muhimu sana katika kuimarisha ndoa bora;




Katika hii miaka 17 tumejifunza kuwa  ndoa inakuwa na matarajio tofauti ya kulea zaidi familia ambayo imepata kibali mbele ya Mungu. Pamoja na mafanikio yote ambayo yanaweza kuwepo katika ndoa bora  lakini kujitoa bila unafiki wa kila mtu ni jambo la muhimu zaidi na zaidi katika kudumisha ndoa bora.




Katika miaka hii 17 tumejifunza kuwa sisi kama wanadamu ambao tumeunganishwa na Ndoa Takatifu bado tunatakiwa kumshinda  ibilisi dhidi  udhaifu au mapugufu yetu  na yatupasa kujua kuwa sisi ni binadamu ambao sio wakamilifu tuna mapungufu mengi ambayo yataweza tu kwisha kwa upendo, msamaha na neema ya Mungu. “Majani yanakuwa ya kijani kama yanamwagiliwa, na ndoa bora ni ile ambayo inaudumiwa kulingana na bibilia inavyotufundisha”. 


Katika miaka hii 17 tumejifunza kuwa Mtikisiko ndani ya ndoa si mwisho wa ndoa bora ni kama tu dhoruba ambayo inaweza kuepushwa kwa kufahamu kwa nini tatizo lilitokea na kujirekebisha mara baada ya kosa kutokea. Ni ukweli ambao haupingiki kuwa pale ambapo udhaifu  hujitokeza  na wana ndoa wakashinda udhaifu huu  ndoa bora hujengwa katika msingi huo. Tunamshukuru Mungu kwani yeye alijua alichotupangia, kwa ajili yetu, na akatuandalia kalenda bora ambayo bado tunaendelea kutembea juu yake ama kweli  kila alichokichagua Mungu ndicho sahihi.

Tumejifunza kuwa katika miaka hii 17, Kumweka Mungu kwanza katika ndoa, huleta furaha ya kweli (joy) faraja na ulinzi. Kumweka Mungu kwanza maana yake mume na mke wanaishi kwa utii na kufuata amri za Mungu mwanzilishi wa ndoa; tunamshukuru Mungu katika kipindi hiki chote tumekuwa tukiwanaomba Mungu pamoja na kuwa na mahusiano yanayoongozwa na Mungu. Kwa vipimo vya kibinadamu huwezi kuwa na furaha siku zote kwa safari ndefu kama ya ndoa furaha ya kweli hupatikana kwa kumuweka Mungu namba moja.


“Mwanandoa mwenye busara hawezi kumuaibisha mwenzi wake bali ataongea kwa hekima na kumaliza tofauti zozote kwa upendo. Kawaida wana ndoa bora hawaangalii mapungufu zaidi bali wanaangalia uwezo na kurekebisha udhaifu wa mwenzake; Biblia inakumbusha kuwa kwa maombi udhaifu hujitenga ”. "Macho ya Bwana ni juu ya haki, na masikio yake husikiliza sala zao, lakini uso wa Bwana ni juu ya watendao maovu" (1 Petro 3:12).

Mungu anajua maumivu na furaha ya ndoa, naye anaelewa tamaa za mwili, yote yanawezekana kwa utia na kusikilizana. Utii kwa Mungu daima huleta furaha (Warumi 16:19).

Katika miaka hii 17 tumeishi kwa kutekeleza wajibu miongoni mwetu, tumejitoa kutimiza mahitaji, kwa njia ya furaha na kuvumiliana; uvumilivu hujenga msingi bora wa upendo, na kuisaidia Ndoa takatifu kusimama imara, kwani mume na muke wanaahidi kubaki pamoja katika mapendo mpaka kufa;

katika hii miaka 17 tumejifunza kuwa inatupasa sisi kama wanandoa kufanya maamuzi wa ya kila siku kwa kuweka Mungu  mbele  kwa kufanya hivyo na, ndoa yako itakuwa na uwezo wa kukabili aina yeyote ile ya dhoruba ambayo inaweza haribu ndoa hiyo. mgogoro haina maana ndoa imeshindikana. Migogoro ni kama dhoruba  kubwa, inatisha na ni hatari. migogoro ndani ya ndoa inaweza kuwa mwanzo mpya. Tumejifunza kuwa  kutokana na maumivu yanayoweza kutokea ndani ya ndoa, NDOA bora huzaliwa.

Mwenyezi  Mungu, asante sana kwa kutuchagua sisi kuwa wanandoa na kutusaidia kuishi pamoja katika miaka hii 17. Tunajua kwamba ulikuwa na mpango na kusudi kwa ajili ya ndoa yetu, na sisi tunazidi kukuomba uzidi kutujalia neema ya utakaso katika maisha yetu ya kila siku ya ndoa; utujalie neema ya kuendelea kusameheana na kuondoa ubinafsi miongoni mwetu. 


Tunazidi kukuomba uendelee kutupa neema ya kukuweka wewe  kwanza katika kila jambo tufanyalo; tunaomba uzidi kubariki ndoa yetu mingi inayokuja  nasi kama wana ndoa tuzidi kupendana na kudumisha amani na kuendelea kuilea familia yetu kulingana na mafundisho yako kama tulivyoagizwa kupitia Bibilia Takatifu 


3 comments:

  1. Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki tumejifunza mengi toka kwenu na tutaendelea kujifunza; ni faraja ya hali ya juu sana na mna kila sababu ya Kumshukuru Mungu.

    ReplyDelete
  2. Mbarikiwe sana Jamani endeleeni kudumisha upendo amani na moyo wa kuzidi kusaidia

    ReplyDelete