UWAJIBIKAJI WA
PAMOJA WA WANASIASA NA VYAMA VYAO JE UNAPUNGUZA UWAJIBIKAJI WA MWANASIASA MMOJA MMOJA KATIKA
KUTETEA MASILAHI YA WANANCHI?
Ni kweli kuwa Wanasiasa wengi huwa na
uadilifu wa kutosha kupinga matendo maovu ambayo mengine hufanywa na viongozi
ndani ya chama chao kama ufisadi na rushwa; lakini wakati mwingine nguvu hizo
huishia ukingoni kutokana na shinikizo kubwa la chama chake, pale
anapolazimishwa kufuata msimamo wa pamoja wa chama katika kufanya maamuzi; na
pale itakapo tokea tu muhusika huyo amefanya maamuzi kinyume na uwajibikaji wa
pamoja wa chama ni rahisi sana kutengwa na kuonekana msaliti:
Kutokana na shinikizo hilo baadhi ya wanansiasa wazuri na waadilifu watetezi wa wanyonge hubaki wamevaa ngozi ya unafiki. kwa msimamo huu ni kweli ambao haufichiki kuwa sio kila mwanasiasa ni mla rushwa au fisadi bali baadhi ya wanasiasa huwa na sifa mbaya kwa sababu nguvu ya uwajibikaji wa pamoja wa kichama.
Kutokana na shinikizo hilo baadhi ya wanansiasa wazuri na waadilifu watetezi wa wanyonge hubaki wamevaa ngozi ya unafiki. kwa msimamo huu ni kweli ambao haufichiki kuwa sio kila mwanasiasa ni mla rushwa au fisadi bali baadhi ya wanasiasa huwa na sifa mbaya kwa sababu nguvu ya uwajibikaji wa pamoja wa kichama.
Nafikiri inafurahisha sasa
kuona kuwa Wanasiasa wengi wameanza kuhodhi sifa mbalimbali za utaalam “professionalism”
tumeanza kuona namana wabunge wenye sifa hizo wanavyoweza kujenga hoja na
kuvuta hisia za watu wengi, na hata kuleta changamoto katika shughuli zao za
siasa. Jingine ambalo tumejifunza tumeona kuwa “professionalism” husaidia kuzingatia
maadili ya utendaji kazi na hulka ya kujiamini na kuwa tayari kukosoa ,kukosolewa na kufanya maamuzi mazito hata wakiwa katika
msimamo wa pamoja ya kichama hawaburuzwi
kihoja.
Pamoja na dhana ya kuwa
lengo la kuwa chama cha siasa chochote, lengo la kwanza kabisa ni kushinda
uchaguzi. Na kuna tofauti kati ya mwanansiasa mtaalam njisi ambavyo ana fanya
kampeni walio wengi maadili ya husadia kupunguza kampeni chafu. Maadili ni
muhimu zaidi na katika siasa na kwa maendeleo ya wananchi. Maadili ya kweli
yatapunguza wanasiasa kujishughulisha na rushwa.
Katika demokrasia wananchi
ndio wenye dhamana na uwezo wa mwisho wa kumrejesha mwanasiasa kuendelea kuhozi
madaraka; pamoja na umaarufu wake, uadilifu na utaalam katika kushughulikia
maswala ya siasa bila ridhaa ya mwananchi sio rahisi kurejea madarakani;
historia ya vyama vingi na
chaguzi za Zambia zinaainisha kuwa ukomavu wa demokrasia ndani ya Zambia wananchi
ndio wenye sauti ya mwisho wananchi wa Zambia wanapima na kuamua kulingana na
utendaji wa viongozi wao na sio ushabiki wa vyama;
Tatizo la kushabikia sana
vyama ndilo linaloponza sana maendeleo ya nchi nyingi za kiafrika; wananchi
wanakumbatia zaidi chama na sio utendaji wa viongozi wa vyama vyao;
Kama wananchi tunatakiwa
kuanza kuangalia upya maamuzi yetu dhidi ya viongozi wetu; tunahitaji viongozi
waadilifu na viongozi wa namna hii wataweza
kuchukua hatua kwa maslahi ya jamii kwa manufaa ya wote, na wanaweza kubaki
madarakani kwa muda mrefu iwezekanavyo kulingana na utaratibu wa nchi husika na
kukendelea kukubalika kwako kwa masilahi ya wengi; Katika mfumo wa kidemokrasia
wa serikali, ambapo nguvu ya utawala ina inapatika upya kila baada ya miaka
mitano na wananchi ndio wenye dhamana ya kuwarejesha madarakani.
Nchi ya Zambia
imetufundisha kuwa hakuna kiongozi anayemiliki watu, hakuna chama chenye
hatimiliki ya kuwa na kundi la wananchi kama itakuwa hivyo basi kuna tatizo na
wananchi katika nchi hiyo; wananchi mara zote wanategemea na wanataka mabadiliko makubwa ya kiuchumi hawahitaji
propaganda za chuki, wanahitaji kufaidi raslimali zao wazambia walikuwa wanashangaa utajiri wote
unaotokana na shaba unakwenda wapi? Pale ambapo hawakuridhika hawakuwa na
papara walisubiri tu wakati ulipofika walimweka pembeni kiongozi na kumpa
dhamana kiongozi mwingine. Lazima tukubali kuwa katika nchi zilizopo kusini mwa
Afrika Zambia ni moja ya changamoto za
mabadiliko ya kisiasa:
Maamuzi ya wananchi katika
awamu tofauti Zambia umeendelea kuwashangaza viongozi walioko madarakani
kuanzaia enzi Kaunda, pamoja na ukongwe
wake wa kutawala kwa miaka 27 hadi awamu ya Banda; Kiini cha msukumo huu nini?
Wananchi wanatamani kupata maisha bora; na kuwa viongozi wenye kiwango cha juu
kabisa cha uadilifu kuweza kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo sio kwa
nadharia bali vitendo;
Viongozi wetu wa vyama vya siasa wamesahau kuwa, Kimsingi, raia huzaliwa wakiwa huru dhidi ya mikingamo ya kijamii, kwa lugha ya kitaalamu tabula rasa. Lakini mikingamo hii ya kijamii huingizwa katika fikra za wananchi kupitia itikadi na elimu ya siasa katika vyama ambavyo wanafuata; na wakati mwingine hata kupitia shule na sehemu za ibada.
Cha ajabu haitoshi
kuivuruga jamii peke yake tumeona na tunaendelea kuon kuwa viongozi wetu wa
kisiasa hapa nchini wamekuwa wakigombana kila mara katika mambo ya msingi na
yasiyo na msingi. Kugombana si kubaya kama kunaleta tija, lakini kule kugombana
kunakofanywa kwa misingi ya kujitafutia umaarufu kunasabaisha viongozi
kushindwa kutekeleza majukumu yao ambayo yanatokana na ahadi wakati wakiomba
ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi, ni dhambi ambayo haiwezi kuvumilika hata
kidogo.
Wakati tunaelekea
kusherekea miaka hii 50 ya uhuru wetu
itakuwa busara kama serikali kwa upande mmoja , vyama vya siasa kwa
upande mwingine kupunguza matumizi nguvu ya kiuchumi katika maswala yanayohusu
zaidi umaarufu wa kisiasa na kupeleka nguvu hizo katika maswala ya kijamii;
bado wananchi wetu hali zao bado ziko duni sana (masikini), tunahitaji barabara
bora; huduma za afya nzuri, elimu bora kwa vijana wetu; ajira za kutosha kwa
wenye sifa za kuajiriwa;
Kama Rais Kenedy wa
Marekani alivyowahi kusema ‘Wewe UMELIFANYIA NINI TAIFA LA TANZANIA’ ni wajibu
wa msingi kabisa kwa wale wote ambao wamepata ajira ya serikali kutimiza wajibu
wao; ni aibu kubwa pale inapogundulika kuwa wafanyakazi wengi wa serikali
wanafanya kazi chini ya masaa nane; tusitarajie maisha bora kama sisi kama
watumishi wa umma hatutawajibika ipasavyo; tutimize wajibu wetu kwa maisha bora
kwa kila mtu,
MUNGU
IBARIKI TANZANIA TUNAVYOELEKEA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU
No comments:
Post a Comment