JE AMANI TUYAHUBIRI
SASA KUELEKEA MIAKA HAMSINI YA UHURU WA TAIFA LETU INAMWELEKEO WA KULETA
MATUMAINI NA MAENDELEO KWA TAIFA LETU?
JE AMANAI HUZAA UPENDO MIONGONI MWETU?
JE HIVI SASA TUNAHUBIRI AMANI AU UNAFIKI WA KUBOMOA TAIFA kwa masilahi binafsi?
Mwandishi Ezekiel Kamwaga, KATIKA MOJA YA MAKALA
ZAKE aliwahi andika kuwa “Bila ya UPENDO miongoni mwa
Watanzania, taifa hili halitakwenda popote. Tutabaki tu kuwa nchi ya manyang’au”.
Wakati tuapojianda
kusherekea miaka hamsini ya uhuru wa
taifa letu kuna mambo mengi tumejifunza na tunaendelea kujifunza katika
kuhakikisha kuwa amani ambayo waasisi wetu wametuachia hatuko tayari kuipoteza; tatizo langu je mikakati yetu ya
kudumisha amani yetu ni imara au inayumba kwa hivi sasa? Na kama inayumba
inayumbishwa na nini?
Ni ukweli ambao hatuwezi
kuuficha kuwa kwa hivi sasa wananchi wengi
wanajaribu kutathimini uzoefu wa sera za vyama vyao ambao ndio chimbuko linalotumika kuidumisha amani nchini. wananchi
na wananchama katika kipindi hiki cha sasa wanachukua kwa hamu fursa hii ya demokrasia ili kushiriki katika shughuli za vyama vyao katika
kuleta maendeleo, lakini pengine kwa wengine wanaishiwa na hamu mara moja baada
ya kuona pengine ni kwa namna gani chama kinaweza husika katika kuhatarisha
amani kwa kuleta vurugu, na hivyo kuhatararisha utawala wa sheria ndani ya demokrasia huru ambayo huwa kama ni kikwazo kwenye fikra bunifu katika fursa ya kujenga amani ya kweli.
Kama nilivyowahi kusema
huko nyuma katika makala zangu kuwa tusipo ongeze jihudi za uwekezaji wa elimu ya uraia (civic education)
kwa wananchi na wanachama wa vya vyama mbalimbali vya siasa amani tunayotamani
kuitunza itabaki kuwa ni ndoto; ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaelewa haki
zao za msingi na matumizi ya sheria ndani ya demokrasia, hii ni fursa pekee
katka kuhakikisha kuwa tunakuwa na amani
yenye vigezo vya juu vya ubora, lakini tukishindwa kufanya hivyo tutaendelea kudhoofisha
sana juhudi zetu za kudumisha amani na upendo katika taifa letu.
Katika kipindi hiki tukiwa
tunajiandaa kusherekea miaka hamsini ya uhuru
wa taifa letu si vibaya kujiuliza amani bora inapatikanaje? Au amani bora
hujengwa na watu au inashushwa tu kama neema kwetu kama taifa kutoka Kwa
Mwenyezi Mungu?
Je yale yanayofanyika hivi
sasa sehemu mbali mbali ya nchi yetu na wanachama mbalimbali wa vyama vya siasa
na kusababisha vurugu kwa kivuli cha demokrasia, ni sehemu ya kudumisha amani
yetu? Je wananchi na wananachama wa vyama husika wanaelewa nini wananchofanya
au ni kufuata tu mkumbo bila kuelewa kwa undani kwa nini kitu fulani kinatokea
na kwa nini mimi nikipiganie? Je ni kwa sababu kiongozi wangu ndio amesema
nifanye hivyo? Au kwa vile rafiki yangu amefanya hivyo?
Nionavyo mimi Kama
wananchi na wananchama wa vyama mbalimbali watendelea kufuata kila jambo kwa
mkumbo kwa kweli Watabaki wamefungiwa katika hali ya hasara, bila uwezo wa
kushindana; watakuwa wakitumika katika uchumi na utamaduni wa utandawazi kwa
masilahi ya wachache na kuwajengea umaarufu watu wachache na pengine kwa undani
na hawatakuwa na masilahi na wengi. Na
wataendelea tu kudumaza vichwa vyao na
kuwatia ganzi ya usikivu na utiifu, badala ya kuwapatia ujuzi na kuwapa nyenzo
wanazohitaji kuwafanya wabunifu na watu wa fikra, watabaki kama tulivyo leo:
wenye mapungufu, tusiotimilika, usiowashindani, na, kama kundi, maskini
kiuchumi.
Lakini siyo lazima iwe
hivyo. Maamuzi tunayofanya leo yanaweza kuwasaidia wananchama kuwa watetezi wa mawazo yao wenyewe, pamoja na
mitazamo na misimamo yao. Wananchama wanahitaji kuwa na ufahamu na ujuzi
unaoweza kutumika katika mazingira yanayobadilika. Wanahitaji uhodari na imani
ya kuamini silika zao. Wanahitaji nidhamu ya kufikia kilele cha uwezo wao.
Pengine vyama vyetu vimejikita
katika mawazo yaliyokuwa sahihi kwa wakati uliopita. Wengi wetu tumezoea
kufikiri kuwa siasa na vyama vya siasa ni sehemu tu ya propaganda ambayo wanasiasa wanajifunza kutoa propaganda pengine
kwa kukariri kilichoandikwa ndani ya
ilani ya chama husika hata kama hawaelewi na hawawezi kupambanua vizuri. Kwa
kufanya hivyo nafikiri tunalenga kuwajengea hofu ya kuvunja sheria na madhara
yake. Ikiwa hivyo basi vyama vyetu vinajiendesha kwa kuwatisha na kuwajengea wachama
nidhamu ya woga ili wafanye yanayotarajiwa kutoka kwao nafikiri ina madhara
makubwa kwa kuzingatia kuwa;
1 Kila
mmoja anakubali kuwa watu wazima wana nafasi muhimu katika kuelekeza makuzi yamawazo
yao ndani ya chama.
2 Tatizo
ni wengi wa wananchama hawa wanatoka
katika katika mazingira ambayo
hawafahamu sana elimu kuhusu haki zao za msingi ndani ya vyama vyao na nje ya
vyama vyao wamebakia kuwa na kiwango kidogo sana cha uwezo wanaohitaji ili
kufanikiwa katika kueelewa na kumbambanua maswala mbali mbali ya kisiasa.
3 mara
nyingi inawezekana kuwa viongozi wa vyama wanaweza kulazimisha utiifu kwa muda mfupi na kujenga
chuki na uasi kwa muda mrefu miongoni mwa wananchi wa jamii moja.
Wananchama wengi wa vyama kutokana na
kukosa elimu ya uraia wanabaki kuwa
wananchama watiifu na waoga wanajifunza kuendana na njia zilizozoeleka za kuwa
na za kufikiri na, kwa hiyo, hawaendelezi stadi za lazima kuleta majibu muafaka
kwa matatizo mapya.
Je, huku siyo kuwa
tunashindwa, licha ya kudhani tumefanikiwa kuwaelimisha wananchama wetu?
Kutokana na mahitaji yetu ya haraka ya watu wabunifu na wenye fikra? Je tunajifunza nini kutokana na migomo,
machafuko ambayo yanasababisha watu kujeruhiwa katika kipindi hiki
tunavyoelekea kusherekea miaka hamsini ya uhuru wetu?
Nafikiri kama tutafanikiwa
kuwafanya wananchama wetu wawe na elimu
ya uraia na itasaidia Kukuza utambuzi:
kujifunza wajibu wao katika kuhusiana na wengine. Ukuaji kimaadili:
Kupitia miundo ya kidemokrasia na uwajibikaji, kuwa mfano mzuri wa kuigwa, na
sera endelevu, elimu bora ya uraia huendeleza uwezo wa wananchi kushiriki kutekeleza sera hizo na kuonyesha
hali ya kujali kama raia. Elimu bora hupalilia viwango dhahiri vya maadili ambavyo
huwasaidia wananchi kujijengea ndani mwao mfumo wa maadili kwa maisha yao yote.
Kama tutafanikiwa kuwa na Vyama
bora vya siasa vitasaidia sana kuleta haya yafuatayo;
• kujenga nidhamu chanya ndani
ya chama chake na vyama vingine,
• kudumisha kuheshimu na utu wa kila mwananchi wa taifa letu.
• kuimarisha amani ambayo
sisi kama taifa tunaipigania kuilinda kwa nguvu zote.
Ni ukweli kuwa katika kipindi hiki cha miaka
Hamsini ya uhuru, wananchi walio wengi wamebaki kwenye kifungo cha mzunguko wa
hali ngumu na umaskini wa kujua haki zao za msingi kwa ukosefu wa elimu bora ya
uraia. Wananchi wengi wamebaki kuwa wapokeaji na watekelezaji wa sera za
viongozi wao hata kama sera hizo haziwanufaishi wao wananchi.
Kupitia elimu ya uraia
tunajifunza kuwa Kuongoza ni
kuwasiliana. Ili uongozi uwepo,
tunahitaji walao watu wawili ambao kwa kiasi fulani wanashirikiana na
kuhusiana. Kwa maneno menginekatika duru
za kisiasa tunahitaji chama zaidi ya kimoja ili kuleta ushindani wa
kimaendeleo;Hakuna awezaye kuongoza akiwa katika upweke. Kwa hiyo, uongozi ni mojawapo ya aina za
mawasiliamo. Kuna uhusiano mkubwa kati ya jinsi mtu anavyoongoza na jinsi
anavyowasiliana na wengine;
Je katika kipindi hiki cha
miaka hamsini tumeongoza vipi? Au tumewasiliana vipi katika kuliletea taifa
hili tija ya maendeleo kwa kigezo cha amani na utulivu?
Hayati Mwalimu Nyerere katika harakati zake zote za
uongozi alijua anahitaji sana hali ya
amani, utulivu na ushirikiano katika kujenga nchi mpya, nchi huru. Mwalimu
alitambua vile vile nchi ilikuwa na makabila mengi zaidi ya 120 yaliyokuwa na
lugha, mila na desturi zinazotofautiana, na ingekuwa vigumu kuongoza watu
wasioelewana kifikra, na tofauti nyingine nyingi.
Alijua tofauti hizi zingeweza kuchochea chuki na hivyo kuondoa matumaini ya kuwa na amani na maendeleo. Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alifahamu kuwa watanzania kuelimishwa juu ya haki zao ili waweze kuzidai si kuvunja amani, amani ya kweli ni ili ambayo imejengwa katika misingi ya ukweli, haki na democrasia ya kweli. Amani ya kweli ni uwepo wa haki na uwajibikaji wa viongozi.
Alijua tofauti hizi zingeweza kuchochea chuki na hivyo kuondoa matumaini ya kuwa na amani na maendeleo. Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alifahamu kuwa watanzania kuelimishwa juu ya haki zao ili waweze kuzidai si kuvunja amani, amani ya kweli ni ili ambayo imejengwa katika misingi ya ukweli, haki na democrasia ya kweli. Amani ya kweli ni uwepo wa haki na uwajibikaji wa viongozi.
Kwa hiyo tunakila sababu
ya kuhakikisha kuwa amani ambayo tunayo tunaendelea kuilinda kwa nguvu zote;
tunawaomba wapinzani waendelee kutufunua kuikosoa serikali pale ambapo inakiuka
na inashindwa kuwajibika; ni ukweli kuwa mengi tulikua hatuyajui tunafikiri
kila kitu kinachofanywa na serikali ni sawa. Analisho kwa vyama vya upinzani
tunaomba chonde chonde tupitisheni katika barabara sahihi ya kudai haki zetu au
unapoiwajibisha serikali, tunatamani sana amani ambayo tunayo iendelee kuwako
kwa miaka mingine hamsini inayokuja, vurugu na hasira zitahatarisha amani yetu;
MUNGU IBARIKI
TANZANIA NA TUENDELEE KUKUMBUKA KUWA “Bila ya UPENDO miongoni mwa Watanzania,
taifa hili halitakwenda popote. Tutabaki tu kuwa nchi ya manyang’au”. NA ISIYO
NA AMANI YA KWELI.
No comments:
Post a Comment