Katika
kelekea kusherekea miaka hamsini ya uhuru
kama wadau wengi walivyowahi kusema kuwa
"ANGALAU sasa Watanzania tunaweza kujivunia muvi (filamu) za
nyumbani”
Kanumba aliwahi kusema
kuwa “Filamu za kitanzania zina historia ndefu tofauti na wengi wanavyofikiria.
kuliwahi kuwepo na filamu kama vile Fimbo ya Mnyonge (1974), Harusi ya
Mariam(1983) na Yomba Yomba(1983) na nyinginezo ambazo ziliwahi kutamba sana
enzi hizo. Baadaye idara ya filamu ikapotea kabla ya kupigwa kikumbo na sanaa
ya maigizo” aliendelea kusema kuwa
"Mabadiliko
yapo,tena makubwa sana.Kwanza utaona kwamba mimi nilipoanza nilianzia kwenye
kucheza tamthiliya na hivi sasa nimeacha kucheza tamthiliya na badala yake
nacheza filamu peke yake. Hivi sasa ili aone ninachofanya inabidi ununue filamu”.
Maneno haya ya Msanii
maarufu wa tasnia ya filamu Tanzania Kanumba yanaukweli ndani yake na
yanaashiria kuwa kumekuwapo kwa maendeleo ya ukuaji wa tasinia ya filamu kutoka
hatua moja hadi nyingine katika kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru;
Wasanii wote wa Filamu wa
hapa Nyumbani wake kwa wanume wanahitaji kupongezwa, kwa kuthubutu katika
kufanikisha ukuaji wa tasnia ya filamu Tanzania; wasanii kama Steve Kanumba, Vincent
Kigos (Ray), Blandina Chagula (Johari), Emmanuel Myamba (Pastor), Jacob Stephen
(JB), Aunti Ezekiel, Steve Mangere (Nyerere), Irene Uwoya, Jackline Wolper Wema Sepetu Monalisa nimewataja baadhi na
wengine wote ambao wanaendelea kukuza fani hii ya filamu Tanzania. Binafsi ninafahamu
ugumu wa technolojia na mazingira ambayo yana mchango mkubwa sana katika ubora
wa tasnia hii ya filamu. kweli kazi ni ngumu.Pia nawapongeza si kwa sababu
eti wanatengeneza film nzuri ,Hapana ,ni kwa sababu wachache waliojitokeza katika
fani hiyo wamethubutu katika kuleta mapinduzi makubwa sana ya tasnia hii;
Tasnia ya filamu Kwa taifa linaendelea kuwa ni kioo cha
jamii, basi kuna kila sababu ya Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia wasanii
ambao ndiyo kioo cha jamii yetu; Nia ya wasanii ni
kufikisha ujumbe kwa jamii,ujumbe ambao utaibadilisha jamii, utaielimisha kwa kupitia maudhui hayo ya kuburudisha. Ujumbe ambao utaleta mabadiliko chanya
kwa jamii na siyo mabadiliko hasi, ambayo yanaliengua taifa katika mhimili wa
kujisifu kupitia tamaduni zetu wenyewe.
Sina uhakika
kutika kipindi hiki cha miaka 50 Wasani wetu wa tasnia ya filamu wameshawahi
kujiuliza maswali haya
·
Mimi ni nani?
·
Thamani yangu ya usanii katika tasnia ya
filamu inatokana na nini?
·
Je ni mambo gani ambayo yamejitokeza katika
kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru na maendeleo ya filamu Tanzania
·
Ugumu wa soko la filamu katika kipindi hiki
umekuwaje?
·
Je wasanii wa filamu wamekabiliwa na Ukosefu
wa creativity katika filamu zao?
·
Je namna gani kama wasanii mnakuza vipaji
vyenu au mnabaki kuutafuta umaarufu baada ya kutafuta njia ya kujiendeleza na
kukuza vipaji vyenu ili kazi zenu ziwe bora zaidi kwa faida yenu na taifa kwa
ujumla wake?
·
Kwa nini
wasanii wetu wanakuwa wagumu wakianza kufanikiwa wakatenga pesa na kwenda kujiendeleza kama Chuo
cha sanaa bagamoyo?
·
Ni kweli kuwa Wasanii wengi hujibweteka na vipaji vyao
wanapoanza kufanikiwa na kuanza kufanya anasa nyingi na kuanza kujidhalilisha na kuanza kupoteza
utu wao na fani yao na hatimaye "kufulia"
Kama wasanii wetu
watafanikiwa kuyajibu maswali haya, hii itawasaidia kutambua kwamba thamani ya
mtu haitegemei watu wengine wala wanavyosema, hata si umbo alilo nalo, bali ni
hali ya ndani. Thamani ya mtu ipo ndani ya utu wake, yaani nafsini mwa mtu
mwenyewe.
Je ni ushauri gani wasanii wetu wanatakiwa waufuate ili
kuimarisha sanaa zao na maendeleo yao?
· shauri wajiendeleze kimasomo na
kuijishughulisha na maswala ya maendeleo kuliku ubishoo usiokuwa na maana.
· Suala la kuigiza uhalisia mimi naamini ni kitu kinachowezekana
· Ni vema kuiga hekima na busara za waliondelea na kuacha yale yasiyofaa
· Ili filamu iuze nakala nyingi siyo lazima wahusika wavae nusu uchi au waonyeshe matendo ya aibu, bali ni umahiri wa kuigiza,kipaji na nidhamu katika uigizaji.
· Wasanii wetu wanatakiwa kukuna vichwa sana na kubadilika kulingana na dunia inavyokwenda.
· Kupunguza matendo ya ambayo yanakiuka maadili na kuacha tabia za uhuni kwa wasanii wote wa kike na wa kiume heshima ya kila mtu sio uhuni ni maadili mema, na kuwajibika kwa ajili ya mafanikio yao binafsi.
ni ukweli kuwa katika kipindi hiki cha miaka 50, Mimi nafikiri kosoro ambazo zimeelezwa, waigizaji wetu na waongazaji wa filamu wazichukue kama changamoto. Ni kweli kuwa kwa sasa Soko limetanuka bado lakini Safari bado ni ndefu japo kwa wasanii angalau inatia moyo. Kwa hili pengine ushahidi tunao kutoka kwa Kanumba na Ray ambao wamewashukuru wateja wao kwa kuwawezesha kumiliki usafiri wa gharama kubwa kupitia kazi zao.
Wasanii wote wakumbuke kuwa maendeleo yao yataendelea
kupatikana tu kama watakuwa tayari kubadilika; tunazipenda kazi zenu lakini
lazima ziwe katika kiwango bora cha kuangaliwa kulingana na maudhui ya
kufundisha na sio kuwa kazi ambazo kila siku wanatuonyesha kitu kimoja chenye
maudhui yanayofanana.
Kuelekea miaka 50 ya uhuru
ni vyema wanafilamu wetu mkabadilika kwa masilahi yenu wenyewe na taifa kwa
ujumla; mbembwe nyingi ambazo hazina tija hazitawasaidia sana kujinasua kwenye
ugumu wa maisha ya kisanii bali creativity katika utendaji na uandaaji wa filamu zenu ndio silaha pekee
ya mafanikio yenu;
MUNGU IBARIKI TASNIA YA FILAMU TANZANIA IENDELEE KUSONGA MBELE
This blog very interesting but you can also try these ..www.jigambeads.com and ..www.tanzaniakwetu.com for popularity and more advert to advertise. Thanks
ReplyDeleteAsante sana kwa ushauri niaitahidi kufanya hivyo bado wewe kama unanafasi ya kunitangaza basi nitashukuru sana ili wengi wanufaike nashukuru sana kwa ushauri huu mzuri
ReplyDelete