WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, July 12, 2015

NI MAGUFULI MAGUFULI

 DKT. JOHN POMBE MAGUFULI NDIE MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM

1
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake Amina Salum Ally, akiibuka na kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro, akipata kura 59.
2
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana na Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
3
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana wakipitia moja ya magazeti ya kila siku wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mjini Dodoma.

6
45

No comments:

Post a Comment