WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, July 14, 2014

WARIOBA KAA PEMBENI -TENDWA

tendwa_76647.jpg
Dar es Salaam. Aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuacha kuitetea Rasimu ya Katiba kwa maelezo kuwa kazi yake ilikuwa ni kuiandaa na siyo kushawishi kila mtu akubaliane nayo. (MWANANCHI)(FS)

Amesema kazi sasa imebaki kwa Bunge Maalumu la Katiba, ambalo linaijadili rasimu hiyo na kutoa mapendekezo yatakayofaa na kuyapitisha, baadaye wananchi kupiga kura ya ndiyo au hapana kupitisha Katiba Mpya.

“Isingefaa Jaji Warioba kuingia katika Bunge la Katiba na kutoa ufafanuzi kuhusu suala lolote lile. Hivi sasa hayupo katika Bunge hilo, lakini matamko anayoyatoa ni ya kuitetea,” alisema Tendwa katika mahojiano maalumu na gazeti hili.

Tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipotoa rasimu ya pili ya Katiba Desemba 30 mwaka jana, Jaji Warioba amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akitoa ufafanuzi wa sababu za tume hiyo kupendekeza masuala mbalimbali, likiwemo la muundo wa serikali tatu.

Jaji Warioba alianza kushambuliwa kwa kasi kuanzia Machi 21 mwaka huu, baada ya kuwasilisha rasimu ya Katiba katika Bunge la Katiba.

Watu wa kada mbalimbali, akiwemo Rais Jakaya Kikwete walipingana na kilichopendekezwa na tume yake kwa maelezo kuwa kuna mambo yanatakiwa kuangaliwa kwa kina, kauli ambayo kila uchwao inapingwa na Jaji Warioba, huku akisisitiza kuwa kilichomo katika rasimu hiyo kimetokana na maoni ya wananchi.

“Jaji Warioba ameshamaliza kazi yake ya kuandaa rasimu ya Katiba. Anatakiwa kukaa kando na kuacha kutetea rasimu ya Katiba kwa sababu muda wake umekwisha na sasa ni zamu ya Bunge la Katiba,” alisema Tendwa na kuongeza;

“Awaache wajumbe wa Bunge hilo kuichambua rasimu na siyo kuwashawishi wakubaliane na rasimu yake,” alisema msajili huyo wa zamani.

Tendwa pia aligusia suala la maadili ya viongozi nchini, kwamba kwa muda mrefu wameshindwa kufuata maadili na kuchukulia suala hilo kama utamaduni wa kuheshimika wakiwa katika nafasi zao.

Amesema sheria ya maadili ya viongozi nayo inatakiwa kufanyiwa maboresho ili iweze kuwabana viongozi wafuate maadili.

“Hata katika uhakiki wa mali za viongozi, wanafanya shughuli hiyo bila utaratibu maalumu, unaweza kudhani ni maofisa za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),” alisema Tendwa.

Akitolea mfano jinsi alivyosumbuliwa wakati wa ukaguzi wa mali zake, alisema sheria hiyo inatakiwa kueleza mbinu za kufanya uchunguzi wa viongozi kuliko ilivyo sasa, ambapo hata ukijua mali za kiongozi huwezi kuziweka wazi.

source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment