KWA NINI TUMEUINGIZA UFISADI KATIKA UTAMADUNI WETU WA UTENDAJI KAZI ZA
SERIKALI?
Ufisadi kwa uchambuzi wa
haraka haraka ni vitendo vya utapeli, udanganyifu mkubwa unaoleta hasara kubwa
kwa nchi.
Chimbuko la ufisadi ndani
ya nchi yetu ni matumizi mabaya ya madaraka hususa katika matumizi ya pesa za
uma na viashiria vyovyote vinavyhohusishwa na matumizi mabaya yanayolenga
manufaa binafsi hususa kwa wale ambao wamekabidhiwa madaraka na wana access
katika rasilimali ya ya Taifa kulingana na nafasi zao.
Kama mwana zuoni mmoja
alivyowahi sema “Ufisadi na rushwa ni adui namba moja wa haki ya wananchi
katika kudai uwajibikaji wa viongozi kwa sababu vitendo hivyo viovu vinaharibu
kabisa dhana nzima ya uadilifu katika uongozi na hivyo kuhatarisha maendeleo ya
uchumi, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa”.
NINI HASA
KINACHOCHEA UFISADI?
Tanzania ni moja ya nchi
za Kiafrika ambazo baada ya kupata uhuru wake ziliweka utaratibu wa kupata
viongozi wake wa kuongoza taifa kwa kutumia mfumo wa chama kimoja cha siasa.
Wakati huo chama kilikuwa kinaweka misingi thabiti ya uongozi ili kuhakikisha
kuwa anayependekezwa na chama kugombea uongozi ni mtu mwadilifu anayeweka
maslahi ya taifa mbele. kwa ufupi chanzo cha ufisadi ni:
- maslahi binafsi na ya vyama vyao
- kutotosheka na kile wananchopata kama gawio lao stahiri linalotokana mishahara na marupurupu mengine ambayo yameainishwa kisheria
- vitendo vya rushwa, wizi, ukwapuaji au udanganyifu mkubwa wa kupindukia wa fedha na mali za umma unaofanywa na kikundi kidogo cha watu.
- kuwawezesha kubaki madarakani kwa gharama yoyote ile hata kama kwa kufanya hivyo kutaathiri kwa kiwango kikubwa uwezo, heshima,
JE UFISADI
KWA SASA NI SEHEMU YA UTAMADUNI WETU KIUTENDAJI?
Kwa nini tunaweza kusema
kuwa ufisadi umekuwa kama utamaduni wetu?
Kama nilivyoonyesha hapo
juu Fisadi mtu au kikundi cha watu ambao anafuja/wanafuja mali za umma bila
aibu wala huruma. Ni yuko tayari kuishi maisha ya hali ya juu bila kusutwa na dhamiri yake.
Dr. Avazaeli Lwaitama yeye
anaelezea ufisadi “Ufisadi, kwa maana yenye mashiko
kisiasa, ni kushiriki kwenye vitendo vya kupata kipato cha siri kama malipo kwa
kutumia cheo chako serikalini au katika chama tawala kufanikisha malengo
yakujitajirisha kinyume cha sheria ya mtu au kakundi ka watu”.
Ufisadi unapokuwa ni
sehemu kubwa ya utamaduni kwa taifa ni jambo la hatari kubwa sana. Hii ni kwa
sababu rushwa, wizi na udanganyifu wa kutisha havitaishia kufanywa na watu
wenye mamlaka serikalini peke yake, bali vitendo hivyo husambaa na kujengeka
kama tabia ya wanajamii kwa sababu mienendo, vitendo na tabia za watawala
huigwa kirahisi na watawaliwa.
Kimsingi ufisadi huwa unaikumba nchi endapo chama tawala kwa wakati husika, hasa kama viongozi, makada na wanachama wake wanajali zaidi maslahi yao binafsi na ya chama chao kuliko maslahi ya taifa lao.
Kimsingi ufisadi huwa unaikumba nchi endapo chama tawala kwa wakati husika, hasa kama viongozi, makada na wanachama wake wanajali zaidi maslahi yao binafsi na ya chama chao kuliko maslahi ya taifa lao.
ATHARI ZA UFISADI
NINI?
Kwa hiyo, kama sote
hatutaki ufisadi uhatarishe demokrasia ya vyama vingi, amani, mshikamano na
maendeleo ya taifa letu, ni vema makundi yote muhimu katika jamii yajitoe
mhanga kushinikiza uwajibikaji dhidi ya tuhuma za ufisadi zinazoikabili nchi
hivi sasa ili hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha kuwa wanaotaka kupeleka
taifa kubaya hawaogopwi na wanawajibishwa.
NANI ATAWEZA KUONDOA UTAMADUNI HUU NDANI YA SERIKALI YETU?
Kiongozi
ambaye anaweza kuwa katika msitari wa mbele wa kupambana dhidi ya ufisadi ni
yule aliye msafi kabisa mbele ya ufisadi. Ni mtu yule ambaye haogopi vita hivi
maana hajawahi kushiriki katika ufisadi kwa njia yoyote ile. Tena awe ni
mzalendo, mkweli na mtu mwenye utu ambaye amejikomboa kutoka kwa vishawishi vya
tamaa za ulimbikizaji wa pesa na mali za binafsi ambazo anazitumia kuwatawala,
kuwadanganya, kuwanyonyanya na kuwanyanyasa wengine.
Swali katika taifa letu je tuna mtu kama huyu?
Mtu ambaye anaweka
masilahi ya kitaifa mbele na anaeishi ili kuishi ili kuboresha maisha ya kila
Mkenya kwa kutumia mamlaka aliyo nayo kupigania uhuru, usawa, haki na ukombozi
wa taifa lake, huyo anaweza kutegemewa kuongoza mapambano dhidi ya adui
ufisadi. Aidha, shujaa wa vita dhidi ya ufisadi anahitajika kuwa jasiri, mtu
ngangari, ambaye wakati wowote ako tayari na mbioni kuutafuta na kuupiga vita
popote ufisadi popote pale unapojitokeza, hata kama u miongoni mwa watu
anaohusiana nao kiukoo, kikabila, kidini, kisiasa au kirafiki. Je, nani katika
serikali inayotawala anaweza kuwa shujaa wa kupambana dhidi ya ufisadi kwa
kutumia vigezo hivi?
Wadau wa amani ni wale
wanaojitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya kutafuta mafao ya wengi, kulinda na
kudumisha: haki msingi za binadamu, utu na heshima yake. Lakini, maadui wa
amani ni watu wanaoelemewa na ubinafsi, uchu wa mali na madaraka, kiasi kwamba,
hata dhamiri zao nyofu zimekufa.
Nyerere alikuwa mkali na
alipitisha sheria ya mtu yoyote aliyepatikana na hatia ya kula au kulisha
rushwa afungwe na halafu atandikwe viboko 24. “Viboko 12 apigwe akiingia
gerezani na 12 akitoka, akamuonyeshe mkewe,” alisema Nyerere.
Pengine hiyo ilikuwa
hukumu ya kimabavu lakini hukumu kama hiyo inaashiria ujasiri wa kiongozi
na Serikali yake kupambana na rushwa. Daima ujasiri katika uongozi wa nchi
huwa unaanzia juu. Pindi kiongozi akishindwa kuwa na ujasiri mapambano kama
hayo hayawezi kufanikiwa. Tabasamu za jukwaani wakati wa kuzungumzia masuala
mazito ya ufisadi huchukuliwa na wanamtandao wa rushwa kuwa ni mzaha au
kwa lugha ya kileo usanii tu.
Kama wanaharakati wengi
walivyowahi kusema kuwa, “mpaka
atapopatikana Sokoine wa pili, kiongozi atayefanana na Marehemu Edward Moringe
Sokoine kwa nia, ujasiri, vitendo na uadilifu”. Kiongozi wa aina
hiyo ni yule ambaye ukimuangalia utajua kweli huyu ana uchungu na taifa lake na
watu wake. Kiongozi wa aina hiyo atasaidiwa na sheria na uhuru wa Mahakama
katika mfumo wa utawala bora utaohakikisha kwamba wananchi wote ni sawa mbele
ya sheria. Hivi sasa vyombo vya sheria haviaminiki kwa vile vinaonekana kwamba
navyo vimeambukizwa ugonjwa wa rushwa.
Tatizo sugu la rushwa ni
kubwa mno na haliwezi kumalizwa kwa siasa hizi za ahadi hewa na kuwakumbatia
viongozi wabovu na wasiojali kabisa wananchi wa Tanzania. Je Muswada wa
kutenganisha biashara na siasa umefanikiwa kwa kiasi gani?
Katika hali hii ya
uzalendo ya kuipenda nchi yake na kujitoa muhanga kwa ajili ya wanyonge wa taifa
lake Mwalimu Nyerere alikuwa mfano katika mapambano haya kwa dhati kabisa na
bila kujali masilahi binafsi mpaka anaachia madaraka kwa msingi huu name naungana
na wanazuoni walio wahi sema kuwa
- “ Acheni Mwalimu Nyerere aitwe Mwalimu hakuna kama yeye enzi hizi na kama yupo ajitokeza hadharani na kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi na kiuchumi”.
No comments:
Post a Comment