Kuna mwanasiasa mmoja
mkongwe aliwahi sema katika moja ya mikutano yake kuwa; “Msishangae,
tuna viongozi wenye sura mbili, wapo wanaofikiri kwa kutumia matumbo yao jinsi
ambavyo wataneemeka na kujinufaisha wenyewe, hawa ni wale wabinafsi lakini wapo
viongozi ambao wanatumia ubongo katika kufikiri jinsi ambavyo watatumia uwezo
wao wote katika kuwatumikia wananchi, mimi ni miongoni mwa hawa,”
Mwannasiasa mwingine naye
aliwahi sema kuwa “Mawaziri ni lazima wajenge umoja na wakubali uwajibikaji wa pamoja.
Katika uwajibikaji wa pamoja, hakuna wa kuwaruka wenzake.”
Na aliendelea kusisitiza
kuwa “uadilifu si usomi, bali ni tabia akisema hivi sasa bungeni
kuna vijana wengi tu waliosoma kuliko enzi zao, lakini linazidi kupoteza hadhi
yake. Alisema viongozi wanaochaguliwa wanapaswa waache baadhi ya mambo ili
kulinda hadhi yao...Huwezi kuwa mbunge au jaji halafu unakwenda baa unalewa
hadi unaning’iniza miguu juu.”
Naungana na mheshimiwa
mmoja mabaye aliwapa rai wabuge au wanasiasa wenzake kuwa “Lazima
wanasiasa wa Tanzania tubadilike, kulaumiana na kunung’unika tu hakutusaidii.
Leo wananchi wananung’unika na viongozi wananung’unika, kinachotakiwa ni
kutafuta majibu.”
Lakini tukiangalia mbali
kwa faida ya Taifa letu a tukiangalia utendaji wa wanasiasa wetu hasa wakiwa
bungeni, kuzomeana, kulaumiana, kunyosheana vidole, hakutatuvusha
katika maisha bora tunayoyafikiria kwa faida ya Taifa letu, nafikiri
itastusaidia sana kama tafakari ya maisha bora itaanzia kwa waheshimiwa wabunge
ambao wanabeba dhamana kubwa ya maisha ya watanzania;
Katika maisha ya kawaida
ya binadamu na wabunge wetu wakiwa ni sehemu ya binadamu hawa ni ukweli ambao
haufichiki kuwa hata waheshimiwa wabunge wana vibanzi au mapungufu ambayo
wanayaona kwa wenzao na sio kwao, tukifanya tathimini ya kichama; na kujihesabu
wao kama chama wako safi na wana hoja ambazo zinakidhi haja na wenzao
wananamapungufu kihoja au katika kuleta utatuzi wa tatizo; matokeo yake mchango
wa mbunge mwingine hugeuka kichekesho kebei na hatimaye kuhatarisha mwenendo wa
mjadala.
Bunge imara linajengwa katika
msingi wa uwazi kwa kukosoana na kuheshimiana kihoja; ushindani na uchambuzi wa
hoja ni sehemu muhimu sana katika kusaidia Taifa kusonga mbele; wabunge wote
hawawezi kamwe kuwa na mtazamo wa pamoja; Mwenyezi Mungu ametujalia vipaji
tofauti katika kufikiri na katika kutatua matatizo; Waheshimiwa wabunge wetu ni lazima wajifunze kujenga bunge lenye
ushindani wa hoja kama sehemu ya kutatua
matatizo mbalimbali. Tutaweza kushinda tu kama tutafanikiwa kujenge jamii
inayotafakari na si jamii ya kulalamika kila wakati na kuishia kutukanana bila
aibu.
Tunafahamu kuwa Bunge
ndicho chombo cha kutunga sheria na muhimili mkuu sana wa uchumi kutokana na
michango yao bungeni hasa wakati huu wa bunge la Bajeti. Bunge linatakiwa liwe
na uwezo wa kuchangia na kuandaa mazingira yanayofaa kwa maendeleo yetu. Lakini
Kama Bunge halina uwezo wa kuyaangalia matatizo ya nchi hii na
kuyatafutia ufumbuzi, basi, kuna tatizo kubwa katika jamii yetu, kuna tatizo
kubwa ambalo kama tukibweteka, litatutafuna sisi na vizazi vijavyo.
- Je ni kweli kuwa wabunge wa chama tawala wanatanguliza maslahi ya chama chao kabla ya kuangalia na kuwakilisha matatizo na hoja za wananchi waliowapigia kura?
- Je ni kweli kuwa wabunge wa upinzani ndio wabunge wanafanya jitihada kubwa za kuleta hoja za maendeleo bungeni?
- Au wote kwa pamoja na wabunge wetu wanaamini kuwa wao wanaostahili kula kwanza kisha wananchi wale baadaye?
- Je kama hivi ndivyo baadaye hiyo ikifika kunakuwa hakuna zaidi ya makombo na ukoko uliobakia?
Nafikiri linalowezekana
leo lifanyike leo kwani hakuna kesho katika maendeleo ya binadamu kwani sisi
tunaishi leo na sio kesho; kesho inabaki katika hazina ya Muumba wetu tu;
Baba wa Taifa aliwahi
kusema kuwa “Kupanga
ni kuchagua”. Je wabunge wetu wanapanga nini kwa maasilahi ya jamii?
inatupasa kuwakumbusha waheshimiwa wabunge watambue kwamba chochote wanachokipanga na
kukitekeleza ambacho hakiongezi uhuru na umoja wetu wala hakina manufaa kwa
walio wengi sio kitendo cha maendeleo.
Kwa nini kila kikao cha
bunge Bunge kinachofanyika tunaendelea kuona kuwa Bunge letu Tukufu linakuwa ni jepesi mno katika kuwapigania
wananchi? Hoja nyingi zinazotolewa hazilengi sana katika kumnufahisha mwananchi
kumwondoa katika tope alilonaswa la umasikini?
Je tunafaidika nini kama
waheshimiwa wabunge baada ya kujadili hoja kwa kumletea maendeleo mwananchi wa
kawaida wanajadili hoja namana ya kukomoana wao wenyewe; kama bunge letu litaendelea hivyo basi
itatupasa kuamini kuwa baadhi ya mambo yanayofanywa na Bunge hili hayana tija
kwa maendeleo ya Taifa letu. Wabunge Wasisahau kuwa Wabunge wanapokuwa bungeni
wanatumia fedha za walipa kodi. Je hilo linawauma na wanaojiona wanafiki na
waongo pale wanaposhindwa akutimiza wajibu wao? Kama inawauma na kuwakereketa
ni vyema basi kila wakiwa bungeni lazima watumie kwa tija pesa ya mlipa kodi
mnyonge ambaye hakwepi kodi ili kumnufaisha huyu anayewakilishwa na kumfanya
aweze kuishi vizuri huko bungeni wakati wote wa kikao cha Bunge.
Nafikiri kama wabunge Kuna
haja ya kuweka mbele mjadala wa maslahi
ya taifa letu. Tumeshaona na kusikia tabia mbaya wa baadhi ya mabunge ya
wenzetu kupigana bungeni, kutukanan lakini hapa kwetu kwa waheshimiwa wabunge
kuiga tabia hii nafikiri sio jambo njem; majadiliano ya amani kuhusu hoja
mbalimbali za kumkomboa Mtanzania sitasaidia zaidi katika kuleta umoja wa
kitaifa na itatusaidia kama taifa kuweka maslahi ya taifa letu.
Inafurahisha pale
tunapowaona waheshimiwa wabunge bila kujali chama wakikubaliana hoja za msingi
ambazo zinasaidia kujenga uzalendo wa kutetea maslahi ya ya watanzania ambayo hayafungamani na chama chochote cha
siasa wala dini. Bunge letu likiweza kufanya kazi yake katika msingi huu kuondoa
taswira ya BUNGE LENYE SURA MBILI NA MBAYA ZAIDI
LINALOANGALIA MASALAHI BINAFSI YAKUWANUFAISHA WAO NA KUTOKUMJALI MTANZANIA WA
KAWAIDA AMBAYE NDIYE AMEWACHAGUA NA UNASALITIWA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
No comments:
Post a Comment