JE TATIZO LA UCHAFU WA MAZINGIRA UNAOKABILI MIJI YETU NI SEHEMU
YA UTAMADUNI WETU?
Tatizo la uchafu wa miji
yetu ukiongwozwa na jiji la dare s salaam limeendelea kuwa ni kero kubwa sana katika
jamii yetu; kama wananchi wengi na wanaharakati wameendelea kusema kupiga
kelele na kuandika kuwa “ Kama kuna suala
ambalo linakera pia ni uchafuzi wa mazingira. Sio kwamba huwa ni kero tu,
lakini uchafu huleta magonjwa mbali mbali na hatimae vifo ambavyo mara nyingi
ni vya kujitakia.”
Najiuliza leo tatizo letu
kama watanzania ambao tumesherekea miaka 50 ya uhuru wetu kwa amani na utulivu
lakini kwa upande mwingine sherehe zilizozungukwa na uvundo wa taka kila mahali
sisi kama watanzania tumekosa nini au ni nini tunashindwa kufanya ili hata
kupunguza tatizo hili?
Je serikali yetu na
viongozi wake hawalione hili, na hali wakeri? Au wao wanaishio katika nchi
nyingine tofauti nah ii tunayoilalamikia? Au wako kwenye ya kufikirika ambako
wao uchafu hauwakeri na wanashindwa kuusimamia?
Je ni tatizo la pesa za kusiamamia
usafi au zile kidogo zinazopatika zinatumika bila kuangalia kipaumbele? Je miji yetu lina itaweza kuandaa
utaratibu mzuri wa kuwa na Vifaa Vya Kuwekwa Takataka hii itakuwa na mwanzo
mzuri wa kuanza kuwaelimisha wananchi utaratibu na kuwezesha Kila mtu
kuweza kutupa taka taka Popote Alipo. Wananchi wasipoweza kutafutiwa utaratibu wa
kuweza kuwa na ukahika wa wapi watupe takataka tutawapa sababu ya kutoana kama kuna sababu ya Kujali Usafi Wa Miji miji
husika. Je Usafi Wa Miji Yetu Tanzania Inahitaji Pesa Za Kigeni? Tufanye Nini Ili Tutunze Usafi Wa Miji Yetu
JE TATIZO
LA KUKITHIRI KWA UCHAFU JE VIONGOZI WETU
WANAHUSIKA?
viongozi hawawezi kukwepa jukumu
lao katika hili Tusijaribu kuwavua wajibu viongozi wetu. Uchafu unaanzia kwao. Je
uongozi wa miji yetu kwa nini usiwajibishwe? Kwa nini tunawalaaumu viongozi
wetu ? kwa falfasa ya kirahisi tu tunawaona viongozi wetu wanaonyesha kabisa
haw anjali kwani wao wanaangalia sasa na sio chanzo. Watasimamia usafi kwa ajili ya kiongozi mwingine anayekuja
wa nchi tofauti kusafisha
mazingira na kupamba mji, lakini, baada ya hapo uchafu unabaki pale pale. Hii ni
aibu kwetu. Je hata kuweka vifaa vya kutupa taka ndani yake inashindikana? je
hata kutunga sheria ndogo za kuwajibisha wachafuzi wa mazingira inashindikana?
Elimu ya usafi wa
mazingira yafaa iwashirikishe watendaji wote kuanzia ngazi za chini katika
serikali za mitaa, kata hata tarafa. Kama taifa tunahitaji wananchi waelemishwe
vya kutosha kwa wananchi kuhusu usafi wa
mazingira. Kwa mfano uchafu katika jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake ni moja
ya matatizo makubwa na ambayo ni dhahiri uongozi wa jiji hili unaelekea kuwa umeshindwa
kulipatia ufumbuzi.
JE NINI
KIFANYIKE KATIKA KUTATUA TATIZO HILI KWA JUMLA;
Je tunazo sheria
za kusimamia usafi wa mazingira?
Je sheria zetu
zinawabanaje wafanyabiashara ndogondogo ambao
wamekuwa wakijiendeshea shughuli zao mahali popote wanapojisikia na sehemu
ambazo si rasmi na kufanya kuacha taka ngumu katika maeneo ya biashara zao?
Je miundo mbinu yetu
inafanya kazi vizuri au hatuna mfumo taka
unaoeleweka? Je gharama za kusafisha vyoo vilivyojaa mwananchi wa
kawaida amaweza kumudu? Kama hawezi kumudu sheria zetu zinawaruhusu kusafisha vyoo
vyao/au kuzibua wakati wa mvua?
Je ushuru amabao wananchi
na wafanya biashara unatumika katika kufanya usafi au matumizi makubwa ya
ushuru huo unatumika kwa matumizi ya kiofisi?
Kama mwanaharakati mmojai
alivyowahi andika kuwa “ Swala la uchafu
kukidhiri Dar ni watu kutowajibika Ufisadi tu watu wanalipa ushuru lakini
Halimashauri ya jiji wanatupia tumboni.Kama jiji Chafu basi hata watu wenyewe
usafi wao binafsi ninawasiwasi mno.Hata hivyo usafi si kila mtu anaweza. Uchafu
na harufu mbaya katika jiji hilo umekuwa ni jambo la kawaida, hali hiyo
inalitofautisha jiji hilo lenye hadhi Tanzania na majiji mengine makubwa
duniani.”
Waziri wetu Mkuu
Mheshimiwa Mizengo Pinda (Mtoto Wa Mkulima) baada ya moja ya ziara zake za
kutembelea Jiji la Dar es Salaam aliwahi
sema kuwa “hali
hairidhishi, Hali hii isipochukuliwa hatua haraka na kupewa kipaumbele
kamwe magonjwa ya milipuko kama vile kichocho na kipindupindu hayatodhibitiwa
na watu wataendelea kupoteza maisha kwa vitu ambavyo kama kuna mkakati mzuri
vinaweza kudhibitiwa”.
MTAZAMO KWA
UJUMLA
Tunaweza kufanya miji yetu
kung’ara kama kila mtu atajitahidi kuwajibika na kujijengea utamamduni mpya wa
kutunza mazingira, na kukataa tabia ya kutupa taka ovyo na kila mtu kuwa mlinzi
wa mwenzake na kumkemea yeyoye ambaye atakuwa na tabia ya kutupa taka ovyo;
Wananchi wawajibike kwa
upande wao na viongozi wetu nao wawajibike kwa upande wao kwani wao ndio msingi wa kufanikisha zoezi nzima kwa
kuweza kufacilitate utaratibu,
·
Kuandaa sheria ambazo zinatekelezeka;
·
Kuandaa vifaa vya kuwekea taka katika
sehemu mbalimbali za jiji ili kuwarahisishia wananchi kutupa taka na kuwapunguzia wananchi ushawishi wa kutupa
taka ovyo;
·
Viongozi waandae magari yanayotakiwa kwa
ajili ya kubeba taka na sio magari ambayo baada ya kuondoa tatizo la taka,
yanaongeza uchafu kwa kutupa uchafu kila yakiwa yakipita na taka.
·
iko haja ya kuwekwa kwa sheria kali za
kudhibiti kwanza utupaji taka hovyo kama ilivyo katika miji mingine ya kitaifa
na sheria hizo zisiwe mapambo, bali zitumike kwa vitendo kwa wahusika
kuchukuliwa hatua ikibidi kutangazwa ili iwe ifundisho.
·
Viongozi waweze kuona aibu ya miji yetu
kuwa michafu na inanuka
Kama tatizo la uchafu
litaendelea kuwa ni tatizo sugu kwa taifa letu swala hili litakuwa ni aibu kwa
taifa zima na si kwa wakazi miji husika; kama taifa tuweze kuwatumia wataalamu
waliopo kuwaomba kuaandaa mikakati bora ya utupaji taka ikiwa ni pamoja
na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka ambayo hayapo katika maeneo
ya makazi ya watu.
Nafikiri sio jambo la busara kuendelea kutupiana lawama, ni vyema kwa pamoja serikali na wananchi wakakutana kama wadau na kujadiliana namna ya kuondokana na aibu hii. Kwa kufanya hivyo tutaweza kuliepusha Taifa na magonjwa ya mlipuko na kulijengee taifa usalama wa afya za wananchi.
Nafikiri sio jambo la busara kuendelea kutupiana lawama, ni vyema kwa pamoja serikali na wananchi wakakutana kama wadau na kujadiliana namna ya kuondokana na aibu hii. Kwa kufanya hivyo tutaweza kuliepusha Taifa na magonjwa ya mlipuko na kulijengee taifa usalama wa afya za wananchi.
Naamini kuwa usafi hauhitaji
kwenda shule au ufadhili kutoka nje;
bali yatupasa kubadilisha tabia na utamaduni wetu; tunaweza kubadilisha tabia
zetu na kubadilisha maisha yetu ya kutoka kuzungukwa na uchafu na kuwa taifa
safi na litakalo heshimika kwa utunzaji wa mazingira.
TANZANIA
BILA UCHAFU INAWEZEKANA
No comments:
Post a Comment