WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, March 25, 2012

SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA


JE TAIFA LINANUFAIKA VIPI NA SENSA KILA MIAKA KUMI (10)?

Sensa inatumika kutoa habari za hesabu (takwimu) kuhusu watu wote wanokaakatika nchi husika.Habari hizi zinatumika na serikali, mikoa na tawala za mitaa, biashara na jumuia za mahali na nyinginezo kusaidia katika kufanya maamuzi kuhusu mipango ya elimu, afya, kazi, usafiri na hudumu nyingine nyingi.

Kama viongozi wahusika wa kuendesha shughuli nzima ya senza wanavyotuambia kuwa  “Msisitizo wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu ni kutoa kiunzi na miongozo ya kujumuisha vigezo  vya idadi ya watu katika mchakato wa maendeleo ili, hatimaye, mienendo ya idadi ya watu iwiane na mienendo mingine ya kijamii na kiuchumi”.

Kwa maneno mengine Sensa ni utaratibu wa kupata na kurekodi habari kuhusu idadi ya watu fulanifulani. Ni utaratibu wa mara kwa mara na hesabu rasmi ya idadi ya watu hao.


Swali la msingi hapa ni hili?

Je ni kweli kuwa  Vilevile, sera hii ilitoa miongozo itaskayo  weza kutoa  vipaumbele katika programu ya idadi ya watu na maendeleo?

Je  senza ikifanywa vizuri inaweza kuharakisha na kufikia maendeleo endelevu na usawa wa  ndani ya jamii?

Ukweli utabaki pale pale kuwa Takwimu hizi  kweli zititafutwa na kuzingatiwa zitatusaidia sana katika kupanga maendeleo ndani ya jamii jamii zetu? Ni dhahiri kuwa takwimu hizi zinaonesha uwiano wa idadi ya watu ndani ya jamii zetu hasa katika huduma muhimu zinazotuzunguka, kama vile  huduma ya hospitali zilizopo nchini. 

Je sensa ni chanzo cha maisha bora?

  • Nia ni kuisadia Serikali ili iweze kupanga mipango ya maendeleo na kutunga Sheria, na kuandaa Sera kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wake kwa kutumia takwimu sahihi.

  • Pia husaidia katika kutoa mwelekeo wa siku zijazo yaani 'forecasting'.

  • Maendeleo endelevu na kuondoa umaskini

  • Kuongeza na kuboresha upatikanaji na ufikiaji wa huduma bora za kijamii

  • Kuwa na mgaosawa, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, haki ya kijamii na maendeleo kwa watu wote

  • Mpangilio mzuri  baina ya idadi ya watu, matumizi ya rasilimali na mazingira

Lengo kuu la Sera ya idadi ya watu ni kuiwezesha Tanzania kufikia kiwango cha maisha kilichoboreshwa na kufanikisha ubora wa maisha ya watu wake. Vipengele muhimu vya ubora wa maisha ni pamoja na afya na elimu bora; chakula cha kutosha na makazi bora mazingira imara; mgaosawa; ubora wa kijinsia, na usalama wa watu binafsi. Aidha,  Sera ina lengo la kuelekeza ubunifu wa Sera za Kisekta, na mikakati na mipango mingine inayohakikisha maendeleo ya watu. Malengo mahsusi ya sera hii ni kufanikisha  yafuatayo.

Sasa nini tuzingatie kuelekea katika kipindi cha sense 2012?

Inafahamika kuwa sense ni swala la kimataifa kwani katika kila nchi zoezi hili hufanyika kwa umakini kwa mbinu tofauti kulingana na level ya uchumi ambayo nchi husika wamefikia:  kwa hiyo watafiti wote duniani hutumia takwimu zilizofanyika nyuma na kueleza ni nini kifanyike kuboresha zaidi huduma au kukuza uchumi wa nchi kwa manufaa ya umma. Hakuna nchi duniani ambayo haitumii takwimu za nyuma kwa ajili ya kujipima kimaendeleo.  Kitaalamu hakuna takwimu ambazo zinapitwa na wakati.  

Sera inatoa miongozo ya kushughulikia masuala ya idadi ya watu kwa namna jumuishi. Hivyo, inatambua mahusiano baina ya mienendo ya idadi ya watu na ubora wa maisha kwa upande mmoja na ulinzi wa mazingira na maendeleo endelevu kwa upande mwingine. Utekelezaji wake utatoa upeo mpya kwa programu za maendeleo kwa kuhakikisha kwamba masuala ya idadi ya watu yanashughulikiwa kikamilifu

Sensa italenga katikakulenga kujua umaskini wa kipato cha mtu mmoja na idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi. Itasaidia Serikali kwenye mipango yake mbalimbali, ikiwamo kutathmini Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKKUTA) na MKUZA, Zanzibar.

Je ni kweli sababu ambazo serikali kuhusu maazimio ya sensa zinakidhi haja?

Sense ikitumika vizuri kwa kuangalia uwiano wa  idadi ya watu vinaathiri maendeleo na ustawi wa mtu mmoja mmoja, familia, jumuiya katika ngazi ndogo na katika ngazi ya wilaya, mkoa na taifa zima katika ngazi ya jumla. Athari na miitikio ya shinikizo la idadi ya watu zinahusiana katika ngazi zote.

Je sababu ambazo zinaelezwa kuhusu  umuhimu wa sensa katika nchi yetu unaendana na lengo lake; 

Kuna baadhi ya wanaharakati wanaoona kuwa “Sababu zinazotolewa na Serikali kuwa zitasaidia kufanya maamuzi sahihi si kweli, kwani Sensa nne zishafanywa na hakuna maamuzi yalofanywa kwa kuzingatia hizo Takwimu za Sensa. Kama madawati hayatoshi, Mikopo kwa wanafunzi haitoshi, Madawa Hakuna, Mahospitali hayatoshi, Miundombinu karibia yote haiendani na idadi yetu. Nadhan serikali ingejikita zaidi kutafuta vyanzo vya mapato badala ya kuchezea mapato kwa miradi isiyo na tija”.

“Jambo ambalo ni changamoto kwetu ni hoja ya kwamba, pamoja na jitihada hizo, taasisi za tafiti hazijaleta matumaini makubwa hususan upande wa uchumi… miongoni mwa sababu zinazochangia kutopungua kwa umaskini wa wananchi wengi ni pamoja na kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu ambalo haliendani na kiwango cha ukuaji wa uchumi,”

Je sensa inasaidiaje na tatizo wa watu kuhamia mijini?

Kuongezeka kwa watu mijini ambako kunasababishwa na wengi wao kuhama kutoka vijijini, kunaathiri shughuli za uzalishaji za kilimo katika maeneo ya vijijini na hivyo kupunguza kipato na hatimaye kuongeza umaskini kwa wananchi wa vijijini,”

Msongamano wa watu na magari mijini, shida ya maji na miundombinu ya barabara na maji ni ushahidi tosha kwamba idadi ya watu haiendani na ongezeko la kukua kwa uchumi na huduma nyingine za kijamii.

Je takwimu zinazopatikani  kweli ni sahii kwa asilimia 100 au zina mapungufu mengi?
 
kama mtaalam mmoja wa sense alivyo wahi sema “tulipata shida sana kupata takwimu sahihi za walemavu wa ngozi wakati ule kulikuwa na mauaji makubwa ya ndugu zetu hawa, ilibidi tutume watu wakawahesabu lakini bado kulikuwa na changamoto kubwa”.
Changamoto nyingine inayowakabili wataalamu hao wa kutenga maeneo ni pamoja na baadhi ya maeneo kutofikika kwa urahisi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo miundombinu duni ya barabara, baadhi ya maeneo kuwa misitu minene yenye wanyama wakali pamoja na miinuko mikali na mabonde katika maeneo mbalimbali hali inayowafanya wataalamu hawa kufika kwa taabu katika maeneo hayo ili kupata vipimo sahihi.

Kutokana na utaratibu wa kufanya kazi kwa kuchelewa na kwa kukosa uthubutu hupelekea kushindwa kufanya kazi zao  mapema kwa kuwa na maandalizi yatasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuepuka zima moto ilimradi kazi imalizike na kukosa takwimu sahihi kwa wakati muafaka.

  • Je changamoto ya nyumba zakulala wageni au nyumba za makaazi zinazokaliwa na watu wengi wakati wa sensa   zinahesabiwa vipi? mathalani  nyumba moja kuwa na wapangaji wengi, kunasababisha viongozi wa eneo husika, kutojua idadi ya kaya zilizopo katika eneo husika.

Usahuri wa kawaida tu kama Taifa lazima tuhakikishe kuwa idadi ya watu itakayo patikana mwaka huu igeuke kuwa changamoto ya maendeleo na  kuwahakikishia wananchi wanapata maisha bora; Tusigeuze Sensa kuwa Mradi wa kujinufaisha tu

Lazima tujenge uadilifu katika kufanya kazi hii kwani ni kazi ambayo ni nyeti kwani wataalamu wetu wa kuhesabu watu wanaweza tu kuamua kuto kwenda kijiji fualani kutokana na tatizo la suafiri;

Tuhakikishe kuwa wote watakao husika katika zoezi hili serikali tunaiomba ijitahidi kuwahudumia  stahiki zao wasitumie kizingizio au kujenga kiburi cha kushindwa kufanya kazii zao kwa umakini kwa sababu Fulani ambyo inaweza kushughulikiwa;
Kwa naman yeyote ile sense ni muhimu toka enzi za babu bau zetu kama nukuu hii inavyoonyesha;

  • Je taarifa za sensa zinakusidiwa vile vile kutumika kwa kazi nyingine zinazolenga manufaa Chanya wa ukuaji wa Taifa?

Wakati sensa hutoa njia muhimu ya kupata taarifa za takwimu kuhusu idadi ya watu, habari hii wakati mwingine husababisha dhuluma, kisiasa au vinginevyo, ikiwezeshwa kwa kuunganisha utambulisho wa kibinafsi na takwimu za faragha

Hitimisho

Ni ukweli ambao lazima tuukubali kuwa  pamoja na juhudi kubwa, Ofisi ya Sensa haijawahi kuwa na uwezo wa kuhesabu kila mtu binafsi, kupelekea utata kuhusu kama kutumia takwimu mbinu ili kuongeza idadi kwa baadhi ya makusudi, kama vile hoja juu ya jinsi ya kuboresha ukusanyaji wa zoezi nzima kwa malengo yalikusudiwa kimaendeleo. Nahitimisha kwa kujiuliza maswali yafuatayo: 

  • Je katika hali hii taifa lifanye nini? 

  • Je matatizo ya kushindwa kuboresha maisha bora ya mtanzania chanzo na ukosekanaji wa takwimu sahihi za idadi ya watu? 

  • Je kutokana na ukosefu wa taarifa sahii watendaji wanatumia mwanya huo kujinufaisha wakitumia udhaifu wa ukusanyaji takwimu?

1 comment:

  1. nakubalia nawe katika mengi ambayo umeyaeleza bado sensa haijawa mkombozi wa maisha bora ya mtanzania; mimi naona ni kama tu ni utimizaji wa wajibu wa serikali ili kujiosha macho katika macho ya kimataifa; mbona pamoja na sensa bado mahosiptali yetu, shule zetu hazina vifaa; vipi kuhusu barabara mbona hazilingani na uwiano wa watu? bado tuna kazi nzito mbele yetu; pengine siku moja itafika

    ReplyDelete