WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, March 8, 2012

DADA SHAMSA FORD STAR WA MOVIE NA SIKU YA WANAWAKE


SIKU YA WANAWAKE DUNIA


Ni ukweli ambao haufichiki kuwa katika dunia hii tunayoishi hakuna kiumbe chochote chini ya jua ambacho hakina mama,hakuna binadamu yeyote ambaye hajui umuhimu wa mama,hakuna asiyejua uthamani wa mama katika maisha yetu ya kila siku; malezi bora yanapatikana kutoka kwa mama, na kwa malezi yake bora mimi leo nimefikia katika khali hii ambayo ninairingia; Asante sana Mama wewe ni shuja wa maisha yangu; Asannte sana Mke wangu wewe ni chachu ya maendeleo yangu;

Siku ya leo dunia inasherekea mwaka wa 101 tangu sherehe hizi zilipoanzishwa rasmi: Hii ni siku ambayo wanawake walisimama kidete kudai na kutetea haki zao: msimamo huu wa wanawake ulikuwa ni changamoto kwa dunia na kwa mfumo dume; msimamo huu ulileta  changamoto kwa  Serikali mbali mbali na hata kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na hasa yale yanayotetea usawa wa jinsia, hii pia iliwahusisha mashirika ya kidini katika kupigania haki hizi wa wanawake.


SIKU HII INATUFUNDISHA NINI?


  • ·   Siku hii inatukumbusha  ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike  ndani ya jamii yetu na ubaguzi wa wazi wazi wa upendeleo unaofanya kwa watoto wa kiume;
·  

  •   Siku hii inatufundisha kuwa  wanawake, wananafasi sawa na wanaume katika ushiri kati ka maswala mbali mbali ya kijamii na kisiasa na kiuchumi na wanaweza kufanya vizuri sana kuliko wanauame;



  • ·   Siku hii inatumbusha kuwa wanawake wanaamini hawana silaha nyingine ya kupambana kuleta mabadiliko kuliko  umoja wao.Wanawake ni wajenzi wa amani na wanawake katika nchi mbali mbali za Kiafrika wamekuwa mstari wa mbele kulinda na kudumisha misingi ya amani na utulivu, lakini mchango wao haukupewa uzito unaostahili kutoka katika Jumuiya ya Kimataifa.

SERIKALI INATAKIWA IFANYE NINI KATIKA KUTATUA KERO ZINAZOZUNGUMZWA SANA?
·    
  • Serikali inatakiwa iendelee kuhakikisha kuwa inaandaa mazingira mazuri yatakayo hakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi ya kushiriki   katika  kuleta maendeleo ndani ya jamii,  bila kubaguliwa  na kumpendelea mwananume kutokana na mfumu dume ambao umetawala dunia kwa kipindi kirefu.
·      
  •   Serikali uhakikishe kuwa wanawake washirikishwe katika maamuzi ili kuendelea kuwajengea  uwezo wa  wa kuchangia fikra zao ambazo jamii tunaamini kuwa ni za msingi sana kwani mwanamke ni kiongozi bora sana akipewa nafasi.
·  
  •  Serikali kwa kushirikiana na asisi zisizo za kiserikali ijiepushe kutoingiza ubaguzi na unyanyasaji, na kuendelee kupinga kwa nguvu zote mila potovu zinazolenga kumnyanyasa mwananmke na mtoto wa kike.

NINI JUKUMU LA  WANAWAKE KATIKA KUJILETEA MAENDELEO YAO?
·  
  •   wanawake wanatakiwa wao wenyewe wajithamini na kujiheshimu kwa kujilinda na anasa zinazosababisha maafa ambayo yanatokana na tabia ambazo jamii inaziona ni chafu.
·  
  •  Baadhi ya Wanawake wamekua wanavaa nguo zisizo na heshima  na hii inaharibu  kwa kiasi kikubwa heshima ambayojamii imewapa; ukilinganisha pengine na wanaumenakulingana na mfumo wa maisha yetu kosa la mwanamke linaonekana haraka zaidi kuliko wanaume ambao wanaonekana pengine wamefanya kosa sawa.
·    
  • Wanawake wamekuwa wanakwenda na wanaume hovyo bila kutumia kinga na matokeo wana athirika na maradhi mbalimbali pamoja na kushika mimba nje ya ndoa au hata wakiwa na umri mdogo na hivyo kuwasababishia matatizo kiafya na kimalezi.
·       
  •  Wanawake wamekua wauwaji wakubwa wa watoto na hii inatokana kubeba mimba hovyo bila ya kuwa na uwezo wa kuwalea.
·  
  •  Wanawake wanatakiwa wapendane na sio kuchukiana miongoni mwao, tumeendelea kuona jinsi wananwake wanavyochukiana hadharani,mifano mingi ya chuki hizi tunaweza kuiona kwa wasanii wetu wa kike.na hivyo chuki kama hizi huleta ufa mkubwa wa mshikamano miongoni mwa wanawake.
  • katika kusherekea siku hii ya leo dada yetu Shamsa Ford anawakumbusha akina dada au mama au mabinti nini kifanyike kwa maisha yaliyo bora; 

Binafsi  nimefurahishwa sana na maelezo ya Dada  Shamsa Ford ambaye ni mchezo filamu mashuhuri; ameweza kujieleza vizuri sana, nini majukumu ya wananwake kwa maendeleo yao; nafikiri kama wanawake wengi watakuwa na fikra kama zake kuna uwezekano wa kulisukumu  gurudumu hili kwa haraka sana

Hebu msikilize na ninaamini kuwa utafanikiwa kupata wazo nzuri ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa jamii yetu.


wanawake wakipewa nafasi wanaweza kabisa kufanya maajabu katika kujiletea maendeleo yao;

No comments:

Post a Comment