Jamani Watanzania wenzangu, huku ni
kuchanganyikiwa ingawa kunatia moyo kwamba watu bado mnautaka Muungano wetu.
Mfumo wa serikali tatu kama shirikisho ni sera ya vyama vyote vya upinzani na baadhi ya Watanzania na hata CUF wamekuwa wakiihubiri kwa miaka yote hadi pale Maalim Seif alipobadilika na kuanza kuuhubiri muungano wa mkataba kana kwamba kuna miungano isiyokuwa na mikataba.
Hoja ya muungano wa mkataba inataka mambo ambayo yakitekelezwa huu muungano hautakuwepo na ndicho ambacho watu wa Tume - akina Warioba - huwa wanawauliza wanaoutaja muungano wa mkataba kwamba wanamaanisha hivyo au vinginevyo.
Mfano wa muungano wa mkataba unaotolewa eti ni EU na hiki kilichosemwa na Chadema hakina sura ya EU bali sura ya shirikisho kama yalivyo mashirikisho ya nchi nyingi duniani, mfano Nigeria, Sudan, Ujerumani, India, Kanada, Brazil, Marekani, n.k. Mashirikisho haya pamoja na hili la Chadema yana "sovereign state" moja yenye serikali zaidi ya moja LAKINI huu muungano wa mkataba unaosemwa eti utakuwa na sovereign states zaidi ya moja na hakutakuwa na serikali ya shirikisho bali mfumo kama wa EU ambao ni kama huu wa AU na huu si muungano kamili bali ushirikiano tu.
Hii ni tofauti kubwa mno na kama watu hamuijui, basi ni kweli kwamba hata mnachokidai hamkijui.
Tofauti ya shirikisho la Chadema na haya ni kwamba shirikisho la Chadema lina serikali kuu dhaifu mno inayozungukwa na serikali mbili zenye nguvu. Huwezi kudumu katika mfumo wenye serikali kuu dhaifu kiasi hiki na pengine tujiulize kwa nini serikali za mashirikisho mengine duniani hazina hii sura? Kumbukeni Muungano wa Kisovieti, kwamba pale ulipokuwa na serikali ya shirikisho dhaifu ndipo hapo ulipovunjikilia mbali.
Huo muungano wa mkataba unaodaiwa bila kueleweka na hata wanaousema ni mwepesi kuliko mfumo uitwao "confederation" ambao huziunganisha nchi katika masuala ya ulinzi na sera za nje/uhusiano wa kimataifa, kama zile jamhuri za iliyokuwa USSR. Mkishakuwa na sovereignty states zaidi ya moja, na hamna vitu hivi viwili vya pamoja, basi mnaweza kweli mkawa kama EU au AU iwapo mtakubaliana kushirikiana lakini huo si MUUNGANO tunaoutaka siye wengine; sisi tunataka NDOA kamili.

|
No comments:
Post a Comment