Pamoja na mapendekezo hayo, wengine walitaka umri wa kugombea urais ushushwe na kuwa miaka 35, badala ya sasa ya miaka 45.
Wakitoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba mjini Dodoma jana, wabunge hao pia walitaka viti maalumu vya ubunge vifutwe, badala yake wanawake warejee kugombea ubunge majimboni.
Katika mkutano huo, zaidi ya wabunge 36 walitumia nafasi hiyo kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali yenye masilahi kwa taifa, waliyoona yanafaa kuingizwa kwenye Katiba Mpya, ambayo mchakato wa ukusanyaji maoni ya uundwaji wake, unaendelea.
Muungano
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alitaka muundo wa muungano ubadilishwe na kuwa wa Serikali tatu, badala ya uliopo sasa aliosema una kasoro nyingi.
Moja ya kasoro hiyo ni wawakilishi kuruhusiwa kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, huku wabunge wa Bara wakiwa hawana uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi.
“Mwenyekiti, tuwe na Serikali tatu katika muungano, vinginevyo kila mmoja abaki na chake," alisema.
Pia alitaka viti maalumu vifutwe, badala yake wanawake wawekewe majimbo ya wilaya, ambayo watagombea na wenzao.
Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo naye alitaka muundo wa muungano uwe wa Serikali tatu pamoja na kuruhusiwa kwa mgombea binafsi katika nafasi mbalimbali.
Alisema kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wasitokane na wabunge kwa sababu hawataweza kufanya kazi kwa ufanisi na ni mgongano wa kimasilahi.
Mbunge wa Mkanyangeni (CUF), Mohamed Mnyaa alitaka kuwapo na Serikali tatu katika muungano.
Alisema kama Tanzania Bara watakataa kuita nchi yao Tanganyika basi wanaweza kuiita jina lolote hata Mzizima.
“Muungano uwe wa Serikali tatu, Tanganyika wawe na nchi yao na sisi tuwe na Zanzibar yetu, kama bara hawataki kuiita nchi yao Tanganyika basi wanaweza kuiita hata Mzizima,” alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Chakechake, (CUF), Mussa Haji Kombo alitaka muundo wa Muungano uliopo ubadilishwe badala yake uwe wa mkataba.
Mwananchi
Meza kuu ilivyokuwa katika mkutano huo.
Mbunge wa Dole Mhe. Sylvester Mabumba akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano wa kukusanya maoni ya Wabunge kuhusu Katiba Mpya mjini Dodoma leo Jumamosi, Novemba 3, 2012. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba, Makamu wake Jaji Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
Mbunge wa Bunda na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano) Mhe. Steven Wassira akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano huo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akitoa maoni yake katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Warioba akiongea kabla ya kuanza kwa mkutano wa mkutano wa kukusanya maoni ya
Wabunge kuhusu Katiba Mpya mjini Dodoma leo Jumamosi, Novemba 3, 2012.
Kulia kwake ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na kushoto ni Makamu wake Jaji
Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
Ohio Street,
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (00 757 500800,
Website: www.katiba.go.tz
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
Ohio Street,
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (00 757 500800,
Website: www.katiba.go.tz
No comments:
Post a Comment