Na
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina.
Mahakama
ya Wilaya ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar leo imepunguza masharti ya dhamana
kwa Viongozi saba wa Jumuiya mbili za Kiislamu Zanzibar, wanaokabiliwa na
mashtaka ya kusababisha vurugu na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya
barabara mjini Zanzibar, leo tena wameshindwa kupata dhamana.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa
uwamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mh. Ame Pinja, baada ya
kukubali maombi ya Mawakili wa Watuhumiwa waliomba kupunguzwa kwa masharti hayo
kwa wateja wao.
Watuhumiwa
hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimam ZanzibarSheike Farid Hadi Ahamed na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselemu na wenzao watano.
Inspekta
Mhina amesema kuwa kutokana na uwamuzi huo, kila mshitakiwa sasa atatakiwa kuwa
na wadhaminiwa wawili ambao ni watumishi wa Serikali na kwa kila mmoja awe na
kiasi cha shilingi 500,000 tofauti na mashrti ya awali ya wadhamini watatu na
kwa kila mmoja kwa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mmoja.
Hata
hivyo pamoja na kupunguzwa kwa masharti hayo, hakuna hata mshitakiwa mmoja
aliyedhaminiwa kutokana na kukosekana kwa wadhamini ambao ni watumishi wa
serikali.
Inspekta
Mhina amesema kuwa Watuhumiwa hao ambao wanakabiliwa na kesi tatu tofauti za
kuzusha ghasia na kupelekea vurugu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar,
wamerudishwa rumande hadi desemba 4, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.
Amesema
wakati wote mahakama hiyo ikiiendelea, hali ya ulinzi nje na ndani ya
Mahamakama uliimarishwa vya kutosha ambapo Makachero wa Jeshi la Polisi pamoja
na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wale wa vikosi.vya Ulinzi vya
Zanzibar
No comments:
Post a Comment